MAHELO. E.B
Member
- Aug 13, 2013
- 27
- 6
Inasikitisha, watuhumiwa dhidi ya MAUAJI ya Stephano Bahati (14/05/2010), aliyekuwa Katibu wa CCM kata ya Isamilo jijini Mwanza wote wameachiwa huru. Kibaya zaidi aliyekamatwa (Jumanne Osca) akikimbia baada ya mauaji hayo nae kaachiwa huru baada ya Jaji kukataa ushahidi wa Mkemia wa serikali kuwa damu iliyomwagika ofcn alipochomewa kisu marehemu hadi kufa ilikuwa inafanana na damu iliyokuwa kwenye nguo ya muuaji (ndugu Jumanne Osca) pamoja na mnuso wa mate yake.
Kesi ilimhusisha aliyekuwa Meya jiji la Mwanza (Biyondo) baada ya bwana Jumanne Osca kudai kuwa alikodiwa kuua kwa ahadi ya kulipwa donge nono la pesa.
Baada ya Jaji kuwaachia huru imekuwa kama tamthilia na kusababisha gumzo kuanzia ndani ya hiyo Mahakama kuu iliyopo Jijini Mwanza hadi maeneo mbalimbali ya mjini kati.
Wananchi wengi wamesikika wakisema wajipange kuiadhimisha kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa (Mwl. J.K. Nyerere) wakidai alizikwa na sheria zote za nchi hii. Sheria zilizobaki ziko chini ya sheria mama iitwayo MONEY LAW (sheria pesa).