"sitaki kumwona lord eyez nyumbani kwangu".mama ray c

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,551
Reaction score
1,777


MAMA mzazi wa staa wa Bongo Fleva mwenye skendo ya kubwia madawa ya kulevya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Magret Mtweve ametoa tamko kali dhidi ya aliyekuwa mpenzi wa mwanae, Isaac Makuto ‘Lord Eyez’ kutotia mguu nyumbani kwake Kunduchi, Dar.

Mama Ray C alichimba mkwara huo wakati akizungumza na Mpekuzi wetu Jumatatu iliyopita alipoulizwa kama Ray C amerudi nyumbani kwake baada ya kutoweka kitambo.

“Amerudi jana jioni (Jumapili). Nilipomuuliza amesema alikuwa Kariakoo, lakini hataki kuwataja aliokuwa nao wala alichokuwa akikifanya.



“Nimekuwa nikizunguka kwenye makanisa mbalimbali kumuombea njia, naona ameanza kuleta matumaini lakini sitaki kabisa kumsikia mtu anayeitwa Lord Eyez, yeye na wenzake ndiyo waliomsababishia matatizo haya mwanangu,” alisema mama huyo.




 
kweli mtoto asokuwa wako utampachika kila ubaya...mama kiuno usinyooshee watu vidole mchawi mwanao mwenyewe!
 
Mtoto alionja bwimbwi akapagawa maana alianza na Mwisho akawapata nyoka alisia hao Lord Aiz akawa mtaalamu wa kubwia kuliko waliomfundisha!pole mama umaarufu umemponza mwanao!
 
mama kashtuka kujifunika shuka asubuhi!! kumekucha zamaniiii....leo ndo humpendi lord?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…