Sitakuja kusahau nilipokamatwa navuta nyumbani, nililetewa mchungaji alieniombea lisaa akidai nina pepo

Sitakuja kusahau nilipokamatwa navuta nyumbani, nililetewa mchungaji alieniombea lisaa akidai nina pepo

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Ilikuwa saa tatu usiku, nakumbuka nilikuwa room nimechill kisha nikaamua niende nje nijiburudishe kidogo. muda huo wazazi walikuwepo sebuleni wakitazama TV, hivyo nilipaswa kuwa mwepesi, nitoke haraka kimya kimya kisha nirudi bila wao hata kugundua.

Basi nikaenda nje nikajibanza katikati ya gari mbili kulikuwa na kagiza hapo, nikawasha, nikapiga pafu mbili nasikia mtu kwenye giza anasema, "Mungu wangu ! Mungu wangu !" ni kwa dakika mfululizo, ilikuwa mama yangu! Akaniuliza kama nimekuwa mwendawazimu, kisha kama mnavyozijua tabia za wanawake akakimbia ndani kuitangazia nyumba na kupigia kila mtu simu kuwaambia navuta !

Mzee alinifuata mkuku kama kifaru hakunipa nafasi ya kujieleza alinilamba ngwala vile navyoshuka bila balance akanishushia makofi mazito mawili, nilitaka nikimbie akanikwida tunaangaliana uso kwa macho, acheni tu !, baada ya dozi ndogo tukarudi ndani yowe za mama na makaripio ya mzee yalitawala, usiku ulikuwa mrefu.

Yani kuanzia siku hio nyumbani palikuwa ahera, mama ananifuata ananusa nguo, nikitoka kidogo mzee ananipiga maswali ya kipolisi nilipotoka na ikibidi anaenda kuhakikisha, naletewa simu kwenye line yupo ndugu au mjomba naambiwa niongee nae kwenye loud speaker huku wao wanakandia, ufunguo wa chumbani waliutoa, It was hell !

Siku ya siku nakumbuka nimeitwa sebuleni nakuta wameleta mchungaji kwa jinsi alivyo ni wa mchongo tu, kufupisha story alisema nina pepo, nakumbuka niliombewa lisaa yani mchungaji shati alilovaa limelowana jasho kwapani, sauti anayokemea utadhani anapiga yowe ya kuibiwa, Toka wewe pepo 😂

Ilibidi nizuge tu maombi yalisaidia ila kama mnavyoijua addiction ni kitu kilicho kichwani hakuna dawa zaidi ya maamuzi binafsi, nilizidisha tu ubunifu wa kujificha, nilikuja kuacha kwa hiari
 
Kama ulikua una vuta hii kitu walikukosea sana , ila kama ni tumbaku ulikua namapepo kweli🤔
1738096975992.jpg
 
Nakumbuka nikiwa kijana mdogo nilikamatwa nikivuta. Ilikuwa saa tatu usiku, nakumbuka nilikuwa room nimechill kisha nikaamua niende nje nijiburudishe kidogo. muda huo wazazi walikuwepo sebuleni wakitazama TV, hivyo nilipaswa kuwa mwepesi, nitoke haraka kimya kimya kisha nirudi bila wao hata kugundua.

Basi nikaenda nje nikajibanza katikati ya gari mbili kulikuwa na kagiza hapo, nikawasha, nikapiga pafu mbili nasikia mtu kwenye giza anasema, "Mungu wangu ! Mungu wangu !" ni kwa dakika mfululizo, ilikuwa mama yangu! Akaniuliza kama nimekuwa mwendawazimu, kisha kama mnavyozijua tabia za wanawake akakimbia ndani kuitangazia nyumba na kupigia kila mtu simu kuwaambia navuta !

Mzee alinifuata mkuku kama kifaru hakunipa nafasi ya kujieleza alinilamba ngwala vile navyoshuka bila balance akanishushia makofi mazito mawili, nilitaka nikimbie akanikwida tunaangaliana uso kwa utosi kijasho kinanitoka sio kitoto ananikaripia najiona nimekuwa nikizubaa kofi, baada ya hapo tulienda sebuleni yowe za mama na makaripio ya mzee yalitawala.

Siku ya siku nakumbuka nimeitwa sebuleni nakuta wameleta mchungaji kwa jinsi alivyo ni wa mchongo tu, kufupisha story alisema nina pepo, nakumbuka niliombewa lisaa yani mchungaji shati alilovaa limelowana jasho kwapani, sauti anayokemea utadhani anapiga yowe ya kuibiwa, Toka wewe pepo 😂

Ilibidi nizuge tu maombi yalisaidia ila kama mnavyoijua addiction ni kitu kilicho kichwani hakuna dawa zaidi ya maamuzi binafsi, nilizidisha tu ubunifu wa kujificha, nilikuja kuacha kwa hiari
Wachungaji mwendokasi hao..kama nakuona ulivyokuwa unasukumwa kichwa..🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom