Sitasahau biashara ya uchimbaji ilivyonifilisi

 
Kununua kifusi uwe na mtaji .
Na mkemia wako awe vizuri.
Akupe makadirio mazuri na faida.
Unakuta kifusi mil 100 hadi 200

Kuna watu wamelizwa sana na hii biashara ya kununua marudio hasa walioingia kichwa kichwa.

Kukadilia rundo hajui. Tani 75 anakwambia tani 120.

Kuchukua sample kwa usahihi hajui hata akikuta amechanganyiwa mapembulio hawezi kuyatambua. Anachukua kipimo kinasoma juu kuliko uhalisia.

Kupatanisha bei hajui. Rundo la 50mil ananunua 65 mil

Hivyo anashindwa kutengeneza faida na mwishoe anatoka barabarani.

Kuna ujanja sana kwa wenye marundo kama kulinyanyua lundo lionekane kubwa, au kuchanganya mchanga mweupe wa kujengea kama marudio yanafanana na mchanga au pengine kusaga activated carbons na kuchanganya kwenye lundo ili lisome ppm za juu.

Kama unaweza kununua mawe mazuri bora ufungue mwalo wako ili ujitengezee marudio mazuri japo kuna watu wanalia na huku kwenye myalo. Baada ya kazi lundo linasoma 0.6 ppm na gharama kibao.

Kwa kifupi tulia na upate elimu ya kutosha ndipo uamue cha kufanya.
 
huyo wa kamati ya ufundi kama namuona vile anavyokula bata na hela za waganga
 
Shemeji yangu amekuja kunishawishi hapa ameniambia niingie kwenye hii biashara inalipa kumbe anataka kunitupa shimoni.

Inategemea kama anauelewa na uzoefu wa kutosha kwenye tasnia hii na nia ya dhati ya kupiga kazi ili mpate faida.

Kuna watu wanauelewa sana wa hii kazi ila hawana mitaji ya kuwezesha kazi hivyo wakipata udhamini kwa makubaliano maalum lazima mfanye kitu. Ila na wewe unatakiwa uwe na uzoefu wa kutosha ili asikuchenge kitu.

Wengine ni wapigaji tu ukimpa 50mil ananunua mzigo wa 20mil na nyingine anajilipa.
 
huyo wa kamati ya ufundi kama namuona vile anavyokula bata na hela za waganga
 
Inategemea kama anauelewa na uzoefu wa kutosha kwenye tasnia hii na nia ya dhati ya kupiga kazi ili mpate faida.

Wengine ni wapigaji tu ukimpa 50mil ananunua mzigo wa 20mil na nyingine anajilipa.

I know nothing about mines. Yaani ni zero kabisa kwenye hiyo tasnia mkuu hivyo hata yeye alivyokuja kunishawishi kuingia kwenye hii biashara niliwaza sana ila nikamkubalia mdomoni tu huku moyoni nikisema siwezi kuingia kwenye biashara nisiyoijua vizuri .

Labda nipate somo hasa kutoka kwa waliofanya hii biashara kama mleta mada hapo kidogo amenipa mwanga juu ya changamoto za hii biashara hivyo nahitaji pia nipate mtu ambaye alienda mbele zaidi mpaka akafikia mafanikia licha ya kupitia changamoto kama hizi.
 

Kujifunza ukiwa na hela ni mtihani sana unatakiwa uende machimboni ukiwa huna kitu mfukoni labda hela ndogo tu ya kula na ishu ndogondogo ili usiwavutie watu kukupiga kupitia mtaji wako.
 
Kujifunza ukiwa na hela ni mtihani sana unatakiwa uende machimboni ukiwa huna kitu mfukoni labda hela ndogo tu ya kula na ishu ndogondogo ili usiwavutie watu kukupiga kupitia mtaji wako.

Kwa sasa hvi siwezi kwenda maana nina majukumu mengi sana yananikaba ila hivyo nikiacha haya majukumu halafu niende huko kujifunza naweza nikarudi nyuma pia hata kwenye hiki kidogo ninachokitafuta.

Pia unadhani itachukuwa muda gani mpaka kupata elimu nzuri juu ya uchimbaji na uwekezaji huko migodini mkuu.
 
Sema ww akili ushailisha negativity!labda na kila mtu na akili yake!...ukiweka kalasha 2 in a month/2mths ushakuza kifusi chako...!

.......
.......
.......hela iko huku!

Kumbuka kuna watu wanalizwa na huku. Wanatengeneza marundo yenye ppm zero point.

Kikubwa uwe na elimu ya ununuzi wa mawe mazuri yenye dhahabu za vumbi na sio vipande.

Na vilevile komaa mwenyewe usipende kutuma sana watu. Utapigwa vibaya.
 
Nilikuwa nalala kwenye fello(udongo)
Najifunika ngumi
Sometimes nashuka chini
mkuu kuna mambo yangu hayaendi naomba namba ya huyo mtaalamu anayeweza kutabiri hata akiwa mbali naomba kuna kitu anisaidie kuna mabwege wananichezea msaada wako tafadhari
 

Kama unakichwa chepesi na ukapata mtu mzuri wa kukelekeza ambaye hatakuchukulia kama fursa kwenye kipindi cha mwezi 1 hadi 3 utakuwa umepata kitu japo cha kukusaidia kwenye hii kazi. Mafunzo ya huku ni ya vitendo yaani mguu kwa mguu.

Kumbuka kuchomwa kwenye ununuzi wa mawe ni jambo la kawaida hata wazoefu wa miaka na miaka wanachomwa na kutoka barabarani na madeni juu ila wanakomaa wanarudi kwenye gemu.

Mafunzo rahisi ni kununua mchanga wa marudio na kupeleka planti kuozesha. Na kwenyewe lazima upate mafunzo ya mguu kwa mguu.
 
Ila maisha bwanaaa, unaweza kwama sehemu ktk halakati zako za kuwekeza ukajiona ni ww tu ndyo umefeli, kumbe kuna wengine wamefeli mpk na magonjwa ya pressure wamepata na wengine kufa kabisaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hayo machimbo ni cha mtoto njoo kwenye tanzanite utakoma matumizi ya uendeshaji wa mgodi kwa siku inafika mpaka laki tano mpaka laki nane kwa siku moja tuu,, na hapo unakuta mtu ana miaka miwili hajazalisha chochote,,,, umeme wa kuendeshea mitambo kwa siku inafika 100k, mlipuko mmoja wa tundu 20 unagarimu 200k hapo unakuta wanalipua mara mbili kwa siku,,,, mgodi unakuta umeenda chini mita 400 hadi mita 1000,, wafanyakazi unakuta wapo 20 na kuendelea na wanakula kwako kila siku,,, hayo machimbo ya dhahabu bado ni kitoto mkuu njoo mererani uone wachimba madini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hii biashara nilishirikishwa na rafiki yangu mmoja... nikakimbia bila kuangalia nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…