Sitasahau!!!

Kwa maelezo yako Suzy inaonekana ulipitia ktk hali ngumu ya maisha, lakini bado hujaeleza ilikuwaje ukafanikiwa kutokea.
Kwa ufupi tena tupe picha inaweza kusaidia watu wengine wenye hali mbaya ili wasikate tamaa!!!!!!!! Ubarikiwe!!



nimeona habari ingekuwa ndefu sana!! lakini nitarudi tena na Part II usijali
 
niliapa kuwa sitawasamehe hasa yule wifi yangu, ila leo Mungu amenifundisha kusamehe!!! nawapenda sana! najua dhahabu safi lazima ipite kwenye moto!!

Pole Susy!

Hii hali uliyopitia ndiyo ilikufinyanga ukatoka kitu bomba kama almasi. MOVE ON USIISHI KWENYE YA KALE PLS soma signature yangu!

Mungu anajua namna ya kukulipa ukiwa mvumilivu na mstahimilivu.Hao ndugu waliokutesa sasa wanaumia zaidi maana unawalipa mema badala ya mabaya.Hakuna kitu kinaumiza hivi.ADUI MPENDE!
 
niliapa kuwa sitawasamehe hasa yule wifi yangu, ila leo Mungu amenifundisha kusamehe!!! nawapenda sana! najua dhahabu safi lazima ipite kwenye moto!!
Maajabu kabisa hayo, kweli maana kilicho safi lazima kipitie kwenye moto, uchafu wote utoke kimiminwe na kutoka kitu bora kabisa. Hayo ni madarasa ya Mungu wetu, ili akutumie lazima upimwe viwango, mwenye kuvumilia hadi mwisho ataokoka!!!!!
 
WomanOfSubstance

thanks!!!
 
Lizy hapa ndipo ninajiuliza kwani kipindi kile chote Mungu alikuwa wapi?? lakini leo nakuja kujua jambo tu, ya kwamba hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea!! na Mungu huinua maadui kwa sababu maalum!!
Mungu yupo muda wote my dear!Wakati mwingine anaacha vile ili ujifunze!Mi hua nashukuru magumu yote yanayonitokea maana najua muda ukifika na kila kitu kitakua bora kuliko hata nilivyofikiri!Na inatokea kila siku!Siunaona kama wewe..muda ukifika unapata sawa yako!
 
Hicho kitu safi kabisa, ushauri bomba nimependa hiyo kwenye red!!!!!!!!Ubarikiwe!!!!!!!
 


ha hah aaaaaaaaaa nimeisoma hiyo signature yako!!! Amen!
 

bwana yesu apewe sifa Amen,kama kweli awo waliyowanyia kama nikweli kama ulivyoandka,basi mungu ni mkubwa daima.
 

ni kweli Lizy,

nakumbuka siku moja kaka alisafiri alivyorudi wifi alinisemelea uongo kwa kaka nilichapwa sana na kaka mpaka katibu kata akaja kunichukua na kunipeleka kwake, Lizy wifi yangu alikuwa ni zaidi ya mateso, alinichotesha maji mbali tena wakati wa usiku alafu kijijini siunajua tena hakuna hata umeme sa moja tu kila mtu kajifungia kwenye kibanda chake!!
 
bwana yesu apewe sifa Amen,kama kweli awo waliyowanyia kama nikweli kama ulivyoandka,basi mungu ni mkubwa daima.

hii ni kweli tupu, haina hata chembe ya uongo kaka tena mambo mengi tu sijayaweka humu!!! mambo ya aibu!!
 
Kwenye thread ya Lizzy nilishindwa kuchangia, hii imeniliza na kunikumbusha zaidi hata siku yangu leo imeharibika kabisa.

Nakumbuka maneno haya tu "Washenzi mbwa nyie nani aliwaleta hapa kazi kula ugali wangu tu wakati kwenu mlikuwa mmezoea mlenda"

Nimeshindwa......................kuendelea
 
machozi yamenilenga lenga baada ya kusoma thread hii.........kweli Mungu hamtupi nja wake.
sifa na utukufu ni vyake
 
Dah!Nxt time sitaanzisha thread yenye kuleta hisia sana!Hata hivyo pole mpendwa!Pole sana..ila yote ni mapito!Masumango yanauma kweli..najua uchungu wake ila mwisho wa siku wewe ndo mshindi wao wanabaki kukushangaa
 
Yani nachukia kweli mtu anapomwadhibu mtoto kwa msukumo wa mtu mwingine!Utakuta huyo kaka yako wala hakua na chuki na wewe ila alikua anafanya kumridhisha mke wake!
 
Da Dena!!

huna haja ya kuumia moyo, leo imeshabakia historia tu, leo naishi maisha mazuri, nakula nitakacho, naena nitakapo, navaa nitakacho, naishi nipendavyo, Mungu ameyabadilisha maisha yangu, tena ameyabadilisha sana tu!!!

Hivyo tumshukuru kwa pamoja tumrudishie sifa na utukufu kwa maana yeye huviinua vilivyo vinyonge!!
 
Yani nachukia kweli mtu anapomwadhibu mtoto kwa msukumo wa mtu mwingine!Utakuta huyo kaka yako wala hakua na chuki na wewe ila alikua anafanya kumridhisha mke wake!

nikweli Lizy maana nakumbuka alisema hawa watoto wataishi hivi mpaka lini? ngoja nioe wasome, kaka alioa kwa ajili yangu na ya kaka yangu, alitupenda sana, nakumbuka kaka alikua akija kutoka safari, Lizzy wifi ananiiogesha tena ananivalisha nguo safi ila kaka akiondoka tu, navalishwa gauni nikitembea ****** yote yako nje. na nguo kaka alizokuja nazo wifi anampa mdogo wake.
 

as if am watching movie.anyway everything has a reason in this world.al i can tell you today is jus 4get the past and move on with your lyfe,and praise almight God 4 making you whoever u r today.
 
as if am watching movie.anyway everything has a reason in this world.al i can tell you today is jus 4get the past and move on with your lyfe,and praise almight God 4 making you whoever u r today.

Thanks my dia!!
 
Susy kuna wimbo naupenda sana bila shaka unaujua;

Muombee adui yako aishi siku nyingi............Asije akafa kabla hajaona baraka ambazo Mungu ameweka juu yako. Kwa yanayokutokea ni Mungu anadhihirisha uumbaji wake. Na ww unapaswa kumtukuza na kumsifu maana amekuinua toka kwa watesi wako. Ni watu wengi wamepitia mambo mengi sana, lakini Mungu ni mwaminifu na anawapigania kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…