Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Trump aliahidi kusitisha misaada kwa nchi za Afrika pindi atakapoingia madarakani kutokana na kile kinachosemwa matumizi mabaya ya viongozi wa Afrika ambao wanatumia misaada hiyo kwa shughuli zao binafsi.
Sasa amekalia kiti utekelezaji umeanza, misaada yote imesitishwa kwa miezi 3 ikipitiwa upya kwenye utekelezaji wake na kama ina faida yoyote kwa Marakani, na kama ikionekana ilikuwa inatumika vibaya itasitishwa mara moja.
Kati sehemu zinazotajwa kuathirika vibaya ni upande wa dawa za TB, ARV na Malaria ambako supply yake ikikata tunajua ni kwa kiasi gani magonjwa haya yatashoot na kuzorotesha afya za wale waliokuwa wanatumia dawa hizi lakini hawana uwezo wa kulipia.
Soma pia: Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika
Turudi kwa CCM.
CCM wamekuwa wakipigiwa kelele kwa matumizi mabaya na manunuzi ya vitu ambavyo havina maelezo yanayojitosheleza zilipotoka pesa za kununulia vitu hivyo na hivi karibuni macho yalitupiwa kwenye pikipiki za Samia pamoja na mabasi ya CCM yaliyotumika kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Mabasi na pikipiki ambazo zimeanza kusambazwa hata kabla ya kampeni kuanza. Hakuna maelezo ya kueleweka juu ya wapi pesa za kufanikisha ununuzi wa pikipiki na mabasi hayo zimetoka.
Najua wazee wa CCM wana resouce nyingi, sijui ni chama kikubwa sana na hivyo kinapokea ruzuku nyingi. Nikwambie tu kama pesa zingekuwa zimetoka kwenye miradi yao yao 100% wasingekaa kimya.
Soma Pia: CCM wanatoa wapi fedha za kununulia msululu huu wote wa Mabasi, kama sio Kodi za Wananchi ni nini?
Yaani wangetumia kila njia ya kuonesha CHADEMA na wale wapinga CCM wote kuwa wana hela, hawawezi kuwafikia hata wafanye nini.
Tunaishia kuona picha ya mabasi ya Yutong kusifiwa afu inaisha hiyo ili kuaminisha watu juu ya mabasi hayo na kupoteza mjadala wa kuulizwa kulikoni, ila ukweli umefunikwa sehemu.
Kama pesa miradi, ambza kununulia magari pamoja na pikipiki za samia zimechepushwa kutoka kwenye miradi ya maendeleo, ambapo asilimia kubwa inaonesha hivvyo, si tu kwamba wametumia kwenye matumizi binafsi, lakini pia wamefanya kosa la pili la kuanza kampeni wakati muda sahihi haujafika.
Yaani ni kuboronga zaidi ya kuboronga, wafadhili wanazidi kuona hakuna haja ya kutoa misaada maasa hakuna hata senti moja inaenda kutumika vizuri zaidi ya kuingia kwenye matumbo ya watu.
Soma pia: CCM imenunua Pikipiki nchi nzima na kuweka nembo ya Samia. Fedha za wastaafu na stahiki za watumishi hazipo
Mwisho wa siku siyo Marekani tu watakacha kutusaidia, na hii haitawamiza wao moja kwa moja, zitawagusa wananchi wa hali ya chini ambayo huduma hizo kutolewa bure ndio salama yao vingenevyo hali ingekua mbaya.
Tunahitaji uwajibikaji kwa serikali na hasa CCM, kila pesa inayotumika iwe accounted for na tujue vyanzo vyake, tujue kodi zetu zinatumika kwa mambo gani.