Sitathubutu tena kushika simu ya mwanamke

Boko halal

Senior Member
Joined
May 14, 2014
Posts
175
Reaction score
124
Nina mpenzi ambaye tumedumu nae kwa muda wa miaka miwili tena wakati mwingine tumeishi pamoja kwa kipindi cha mwaka mmoja ila sikuwa napekua simu yake maana niliaminii ni mtu mzima anajua akitendacho.

Baadae tukatengana kutokana na majukumu ya kazi, ni miezi kama mitatu imepita hatujaonana ingawaje kipindi chote tumekuwa tukiwasiliana huku tukisaidiana mambo mbali mbali sasa ni jana nimemsurprise huyu binti huko anakoishi nilikuta yupo nyumbani akanipokea kwa bashasha akidai amenimiss huku akilaumu kwani sikumpa taarifa.

Simu yake ilikuwa imeharibika whaatsap akaniomba nimtengenezee sasa baada ya kudownload ile app nika backup data aisee nilichokutana nacho huko ni siri yangu maana usiku wangu ulikuwa mrefu wenye mawazo mengi sitawahi msahau na sitamsamehe .

Nashukuru Mungu nimepima niko vizuri yaani wanaume watatu.
 

unatakiwa urudi baada ya miezi mitatu ukapime tena.

.
 
Achana na mambo ya kukagua mambo ya watu.
Maliza mambo yako kwanza.
 
umeshapima uko fresh au sio. haina noma
 


Bora hata huyo Watatu Tu!
 
Siku hizi ukikuta mwanake ana wanaume watatu ujue huyo ni very decent

standards zimeshabadilika

Hata mimi nimeshangaa dogo analia wanaume watatu tu!!!
 

Wewe mwenyewe unawanawake wangapi? Anzia hapo kwanza. Ukiwa na mmoja ndio umind ukikuta mwenzio ana zaidi yako. Hata hivyo, wewe ulikuamini umtengenezee hiyo whatsapp sasa kilichokufanya utafute zaidi ni nini? Hapo umevunja uaminifu kwa kweli
 
Ulikuwa umemchoka ndo maana ukakagua simu yake.
Waswahili wanasema ukimchoka mkeo au mumeo we pekua simu yake.
 
Tuambie hiyo siri yako, tofauti na hao vidume watatu ili tukupe ushaur kwi,kwi,kwi
 
fukuza kaka uyo,hakufai.kuwa kama magufuli...ukiona kakosea leo fukuza kesho wapo wengi sana hawa.
 
Kipimo peke yake ambacho kidogo kinaweza kuonyesha uaminifu wa mwenzio ni kupekua simu na usikute madudu. Unless labda ni kakajambazi au dadajambazi ambao wanacover track zao vizuri. Believe me. Na sign moja wapo anafuta SMS papo hapo. Na ukienda kwenye log. Sent items na received ni nyingi na inbox hamna kitu.
 
lakini unajua yale yanakuwaga maongezi ya kwenye simu tu sio ukweli....

Nilikua nasoma article moja wanasema hiyo pia ni cheating, cos amount ya time, emotions, feelings unazotumia nao was meant kwa ur partner na sio wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…