Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SITI BINT SAAD KATIKA MAISHA YA BIBI TITI MOHAMED
Haya ninayoandika hapa nimeelezwa na marehemu Leyla Sheikh mjukuu wa khiyari wa Bibi Titi Mohamed na shoga yake kipenzi.
Leila alikuwa anakusanya taarifa katika maisha ya Bibi Titi Mohamed kwa nia ya kuandika kitabu cha maisha yake na pia kutengeneza filamu yake.
Haya ninayoeleza hapa ni kabla ya kuundwa kwa TANU na kabla ya kifo cha Siti bint Saad mwaka wa 1950.
Bibi Titi alikuwa mwimbaji wa Egyptian club maarufu ya taarab Dar-es-Salaam nyingine ikiwa Al Watan.
Titi ndiyo kwanza kaolewa na kijana mmoja jina lake Humud.
Humud alikuwa na rafiki yake anaitwa Said Sudi, kijana kutoka nyumba kubwa Zanzibar.
Said Sudi alimwalika rafiki yake Humud aje kumtembelea Zanzibar na akafanya dhifa kubwa nyumbani kwake na akawaalika watu wengine.
Siti bint Saad alikuwepo katika dhifa ile kuburudisha.
Bibi Titi anasema kumwambia Leila kuwa Siti bint Saad akaanza kuimba huku akisindikizwa na vyombo vilivyokuwa vikipigwa na mabingwa wa kuchezea ala za muziki.
Siti bint Saad akimjua Titi kama muimbaji mwenzake kutoka Mrima.
Siti alipokaribia kumaliza ile nyimbo bado beti moja akasogea pembeni akampa ishara Titi aje amalize ile nyimbo.
Bibi Titi wakati ule alikuwa bado hajapewa jina hili la "Bibi" akauchukua ule ubeti akamalizia huku ala zikinung'unika.
Bibi Titi anamwambia Leyla, "Mwanleyla hukuwepo lakini malaika wako walikuwako."
Jana katika kueleza historia ya Bibi Titi nilikileta kisa hiki wakati naeleza kuwa Bibi Titi kaandika maisha yake kabla hajafariki.
In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa kipande hiki cha video ya Titi na Siti bint Saad video ikitoka.
Katika picha wa kwanza kulia ni Siti bint Saad na picha ya pili aliye katikati pembeni ya Julius Nyerere ni Bibi Titi Mohamed na picha ya tatu ni Leyla Sheikh.