Sito sahau siku niliyosahau Konyagi kwenye mkoba wa mke wangu aliyekuwa anaenda kujifungua

FBI CIA

Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
52
Reaction score
43
.
Ni siku ambayo nilimpeleka wife hospital kwa ajili yakujifungua basi bwana tulipo fika pale mapokezi tukapokelewa vizuri wife akapelekwa wodini

Baada ya vipimo madaktari wakaniambia kwamba uchunguzi unaonyesha uchungu haujakolea hivyo apelekwe wodi ya mapumziko

Basi akapelekwa huko.

Kimbembe kilianzia hapo.

Kutokana na sisi kuondoka home haraka haraka tukajikuta tunasahau mkoba wa wife hivyo ikanibidi Mimi nirudi home ili nikachukue mkoba napia niongeze nguo za wife basi nikakodi bodaboda mpaka home nikapanga nguo vizuri nikatoka kurudi hospital sasa nikakumbuka kwamba lazima nitakesha Pale nje nakuna baridi Kali ikabidi nipitie kuna baa moja ipo njiani nikachukua Mzinga wa konyagi nikaenda nikauchimbia kwenye mkoba wa wife nikaondoka zangu nikafika getini nikaomba kupeleka nguo za mgonjwa nikaruhisiwa nikaingia nikampa mokoba wife sasa akaniambia simu itazima muda wowote nikamwambia usijali ukiwa Na tatizo mwambie nesi atakusaidia mawasiliano maana saa hizi muda umeenda

Basi wife akanielewa me nikatoka nilivyo fika mapokezi yule nesi akaniita akaniongelesha ongelesha kwa kuwa tunafahamiana ikapita kama nusu saa me nikamwambia natoka nje kidogo akaniambia sawa sasa ile natoka getini

Hamadi Na kumbuka konyagi Yangu nikatoa simu fasta nikapiga kwa wife haipatikani nikarudi mapokezi nikakuta yule nesi hayupo! Nikatoka nduki kuelekea wodini aliyopo wife bahati nzuri nikakutana nikamueleza ukweli nesi akaenda kunichukulia nyagi Yangu ila hakuna siku niliyo pagawa kama siku ile sipati picha ingekuwaje
 
Nafikiri wodini ingetumika as antiseptic
 
Hey hey, that's not a big issue, fella! After all, your wife wouldn't have sipped the liquor itself. You're very well known as a drunkard. Nobody could touch your bottle of "holy water"!
 
Naomba namba za huyo nesi
 
Kesi ndogo hiyo.....dont stress yourself

ungevunja mguu ....kwa kukimbia hovyo
 
Angenyweshwa dogo baada ya kuzaliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…