SoC03 Sitokusikiliza tena! Umenidanganya mambo mengi

Stories of Change - 2023 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Ni miaka mingi imepita toka nikupe dhamana ya kuniwakilisha mimi mwanachi wa kawaida maneno yako matamu yalinipa faraja nikahisi kweli haya ni matunda ya uhuru wangu, Haukusita kunipa ahadi nyingi zenye matumaini ooh! Utahakikisha napata maji , Utahakikisha napata huduma nzuri za afya na utahakikisha umeme ni wa uhakika, Kauli zako wakati unasema ni ngumu mtu kubaini kwamba huna unalo maanisha isipokuwa ni uongo na uzandiki tu mbele yangu.

Wewe ni hodari wa kusimama kwenye majukwaa unaimba wimbo wa maendeleo kila baada ya miaka mitano huku unaniacha mimi nikifa na njaa ni lini utatimiza ahadi zako ili nami niishi kwa furaha kila iitwapo leo sioni maendeleo bali ninacho kiona ni ukoloni mambo leo, Eeeeh! Muogope MUNGU dhamana niliyokupa ya kuniwakilisha mimi itendee haki kwenye michango usimami kuniongelea mimi maskini nisiyejua kesho yangu nakushangaa wewe kwenye vikao unalala na ukiamka kuchangia sioni cha maana bali ni mizaha.

Hivi kweli unania ya dhati ya kutusemea sisi Watanzania? Au nia yako ushibishe tumbo lako, Utembelee usafiri mzuri na uchukue posho ambazo ni kodi yangu kisha uende vyuoni kudanganya dada zetu huku unawachezea kwa zinaa.

Huku jimboni hautokei basi nimeamua kukwambia pengine utasikia, Barabara bado sana ,Elimu sitaki sema wahitimu ni wengi sana ajira bado ni changamoto Eeeeh! Embu fungua mdomo wewe utasikika, Mimi huko nilipo ni mbali sauti haiwezi fika waambie wenzako waliopata nafasi ya kuwa na vyeo viwili wasipime maisha ya watanzania kwa kujiangalia wao. Bali wayapime maisha ya watanzania kwa kutuangalia sisi.

Ndio sisi bodaboda, Mama nt`ilie, Fundi viatu na sisi wasomi tusio na kazi wamuangalie mfanyakazi wa kiwandani, Mfanya usafi maofisini, Machinga mitaani ,Fundi seremala na Mpiga debe stendi za Makumbusho na Ununio, Muangalie kijana wa Kitanzania baada ya kumpa elimu isiyo na tija umemtelekeza mtaani, Umemwacha anateseka majukumu yamemzonga, Familia inamtegemea hajui afanye nini. Eeeh! Amka simama ongea Eeeh! Amka simama kemea Eeeh! Amka simama tembea Eeeh!

Amka simama waambie hatupo kwenye michezo ya bahati nasibu hivyo wanapofanya maamuzi waiangalie kesho yetu, Kesho ya watoto wetu na watoto wao, Kesho ya wajukuu wetu na wajukuu wao, Kiongozi nakwambia ongea usiogope. Wapi tunashindwa wapi tumekwamaa matatizo hayaishi kila siku rushwa, Wizi wa mali za umma, Ufisadi na unyonyaji nani wakuyasemea haya ikiwa wewe unaogopa?

Eeeeh! Nimegundua yote haya ni sababu ya sheria mbovu ulizozipitisha wewe mwenyewe inakuaje kiongozi mmoja ana nguvu isiyomithilika? kumbe ndio maana waogopa kutuongelea wananchi sababu unajua ukisema ukweli utakosa teuzi. Usiogope mungu yupo na wenye haki usijali teuzi zao wewe ni muhimili unaojitegemea lakini cha ajabu sioni nguvu yako naona kivuli chako sioni mwili wako, Usikubali dharau wewe una mamlaka usikubali kupelekeshwa wewe sio gari la taka.

Wewe ni mwakilishi wa wanachi wewe unatunga sheria wewe unapitisha bajeti wewe unajadili mikataba hivyo wewe ni wa thamani usijivue nguo ulipo ni sokoni kuna watu wengi, Basi hutaki kuvua nguo wameamua kukuvua kwa nguvu sasa mbona wasimama badala ya kuchutama au wewe sio muungwana?

Nakuomba sana usiogope kuongea sema simamia ukweli waeleze ajira ni tatizo waambie elimu ni mbovu sema ufisadi unafanywa waziwazi sema hospitali mambo sio shwari sema yote haya anayeweza kuyaona ni mtoto wa masikini mtoto wa fukara anaye ishi chini ya nusu dola anayeishi kwa kutoa jasho lake anayeishi kwa kukaza misuli yake huku aking`ata meno auvute mkokoteni, Simama sasa nione faida yako zungumza usiogope niandike historia yako onyesha msimamo ili niyaenzi mazuri yako.

Tekeleza niliyokutuma mimi sijakutuma kukuna tumbo na kupiga miayo mimi sijakutuma kuchukua posho za bure mimi sijakutuma kufanya vituko mimi sijakutuma kupiga makofi ovyo kama kwenye matamasha ya burudani mimi nimekutuma kunisemea shida zangu, Hivyo sema usiogope hiyo ndiyo kazi yako.

Najua Unawasiwasi ukirudi kama nitakupitisha tena usiogope fanya niliyokutuma nitakupitisha tena na tena kumbuka nimekutuma kuwakosoa wakubwa hivi unataka kuniambia hakuna wakubwa wanachokosea kama hakuna wewe una maana gani ya kuwa hapo sasa mbona kila kitu wewe ni ndiyo na aliye kuambia ukisema hapana utakuwa umekufuru ni nani tambua ndio nyingi na makofi kedekede ni dalili ya uwoga na sio sifa za kuendekeza kataa kuwa mtumwa unaelipwa fedha nyingi kubali kuwa mfalme unaelipwa pesa kidogo utu na heshima yako italindwa, Kataa kuwa mtumwa kwa sababu mtumwa ni kama mbwa asiye na kwao.

Nina mengi ya kukueleza ila kwa leo nakwambia adui wa mtu ni mtu hivo kuwa makini na jirani yako jirani akicheka sio lazima nawe ucheke bali muulize unacheka nini? akikupa sababu ya msingi basi nawe cheka akikupa sababu ya kijinga usicheke wala usimcheke mwambie jirani kuchekacheka hovyo sio dalili nzuri hasa katika zama hizi za dunia ya mabalaa hivyo elezaneni ukweli na badilikeni.

Mwisho nikwambie hakuna marefu yasio na ncha na mwenda tezi na homo marejeo ni ngamani usipobadilika ukarudi tena nyumbani kunadi sera zako nakwambia sitokusikiliza tena! sababu umenidanganya mambo mengi.
 
Upvote 5
Ni miaka mingi imepita toka nikupe dhamana ya kuniwakilisha mimi mwanachi wa kawaida maneno yako matamu yalinipa faraja nikahisi kweli haya ni matunda ya uhuru wangu, Haukusita kunipa ahadi nyingi zenye matumaini ooh! Utahakikisha napata maji , Utahakikisha napata huduma nzuri za afya na utahakikisha umeme ni wa uhakika, Kauli zako wakati unasema ni ngumu mtu kubaini kwamba huna unalo maanisha isipokuwa ni uongo na uzandiki tu mbele yangu.

Wewe ni hodari wa kusimama kwenye majukwaa unaimba wimbo wa maendeleo kila baada ya miaka mitano huku unaniacha mimi nikifa na njaa ni lini utatimiza ahadi zako ili nami niishi kwa furaha kila iitwapo leo sioni maendeleo bali ninacho kiona ni ukoloni mambo leo, Eeeeh! Muogope mungu dhamana niliyokupa ya kuniwakilisha mimi itendee haki kwenye michango usimami kuniongelea mimi maskini nisiyejua kesho yangu nakushangaa wewe kwenye vikao unalala na ukiamka kuchangia sioni cha maana bali ni mizaha.

Hivi kweli unania ya dhati ya kutusemea sisi Watanzania? Au nia yako ushibishe tumbo lako, Utembelee usafiri mzuri na uchukue posho ambazo ni kodi yangu kisha uende vyuoni kudanganya dada zetu huku unawachezea kwa zinaa.

Huku jimboni hautokei basi nimeamua kukwambia pengine utasikia, Barabara bado sana ,Elimu sitaki sema wahitimu ni wengi sana ajira bado ni changamoto Eeeeh! Embu fungua mdomo wewe utasikika, Mimi huko nilipo ni mbali sauti haiwezi fika waambie wenzako waliopata nafasi ya kuwa na vyeo viwili wasipime maisha ya watanzania kwa kujiangalia wao. Bali wayapime maisha ya watanzania kwa kutuangalia sisi.

Ndio sisi bodaboda, Mama nt`ilie, Fundi viatu na sisi wasomi tusio na kazi wamuangalie mfanyakazi wa kiwandani, Mfanya usafi maofisini, Machinga mitaani ,Fundi seremala na Mpiga debe stendi za Makumbusho na Ununio, Muangalie kijana wa Kitanzania baada ya kumpa elimu isiyo na tija umemtelekeza mtaani, Umemwacha anateseka majukumu yamemzonga, Familia inamtegemea hajui afanye nini. Eeeh! Amka simama ongea Eeeh!

Amka simama kemea Eeeh! Amka simama tembea Eeeh! Amka simama waambie hatupo kwenye michezo ya bahati nasibu hivyo wanapofanya maamuzi waiangalie kesho yetu, Kesho ya watoto wetu na watoto wao, Kesho ya wajukuu wetu na wajukuu wao, Kiongozi nakwambia ongea usiogope. Wapi tunashindwa wapi tumekwamaa matatizo hayaishi kila siku rushwa, Wizi wa mali za umma, Ufisadi na unyonyaji nani wakuyasemea haya ikiwa wewe unaogopa?

Eeeeh! Nimegundua yote haya ni sababu ya sheria mbovu ulizozipitisha wewe mwenyewe inakuaje kiongozi mmoja ana nguvu isiyomithilika? kumbe ndio maana waogopa kutuongelea wananchi sababu unajua ukisema ukweli utakosa teuzi. Usiogope mungu yupo na wenye haki usijali teuzi zao wewe ni muhimili unaojitegemea lakini cha ajabu sioni nguvu yako naona kivuli chako sioni mwili wako, Usikubali dharau wewe una mamlaka usikubali kupelekeshwa wewe sio gari la taka.

Wewe ni mwakilishi wa wanachi wewe unatunga sheria wewe unapitisha bajeti wewe unajadili mikataba hivyo wewe ni wa thamani usijivue nguo ulipo ni sokoni kuna watu wengi, Basi hutaki kuvua nguo wameamua kukuvua kwa nguvu sasa mbona wasimama badala ya kuchutama au wewe sio muungwana?

Nakuomba sana usiogope kuongea sema simamia ukweli waeleze ajira ni tatizo waambie elimu ni mbovu sema ufisadi unafanywa waziwazi sema hospitali mambo sio shwari sema yote haya anayeweza kuyaona ni mtoto wa masikini mtoto wa fukara anaye ishi chini ya nusu dola anayeishi kwa kutoa jasho lake anayeishi kwa kukaza misuli yake huku aking`ata meno auvute mkokoteni, Simama sasa nione faida yako zungumza usiogope niandike historia yako onyesha msimamo ili niyaenzi mazuri yako.

Tekeleza niliyokutuma mimi sijakutuma kukuna tumbo na kupiga miayo mimi sijakutuma kuchukua posho za bure mimi sijakutuma kufanya vituko mimi sijakutuma kupiga makofi ovyo kama kwenye matamasha ya burudani mimi nimekutuma kunisemea shida zangu, Hivyo sema usiogope hiyo ndiyo kazi yako.

Najua Unawasiwasi ukirudi kama nitakupitisha tena usiogope fanya niliyokutuma nitakupitisha tena na tena kumbuka nimekutuma kuwakosoa wakubwa hivi unataka kuniambia hakuna wakubwa wanachokosea kama hakuna wewe una maana gani ya kuwa hapo sasa mbona kila kitu wewe ni ndiyo na aliye kuambia ukisema hapana utakuwa umekufuru ni nani tambua ndio nyingi na makofi kedekede ni dalili ya uwoga na sio sifa za kuendekeza kataa kuwa mtumwa unaelipwa fedha nyingi kubali kuwa mfalme unaelipwa pesa kidogo utu na heshima yako italindwa, Kataa kuwa mtumwa kwa sababu mtumwa ni kama mbwa asiye na kwao.

Nina mengi ya kukueleza ila kwa leo nakwambia adui wa mtu ni mtu hivo kuwa makini na jirani yako jirani akicheka sio lazima nawe ucheke bali muulize unacheka nini? akikupa sababu ya msingi basi nawe cheka akikupa sababu ya kijinga usicheke wala usimcheke mwambie jirani kuchekacheka hovyo sio dalili nzuri hasa katika zama hizi za dunia ya mabalaa hivyo elezaneni ukweli na badilikeni.

Mwisho nikwambie hakuna marefu yasio na ncha na mwenda tezi na homo marejeo ni ngamani usipobadilika ukarudi tena nyumbani kunadi sera zako nakwambia sitokusikiliza tena! sababu umenidanganya mambo mengi.
Mungu
 
Ndugu msomaji usisahau kupigia kura bandiko hili kwa kubonyeza alama ya ^ kwenye bandiko hili. Asanteni
 
Ni miaka mingi imepita toka nikupe dhamana ya kuniwakilisha mimi mwanachi wa kawaida maneno yako matamu yalinipa faraja nikahisi kweli haya ni matunda ya uhuru wangu, Haukusita kunipa ahadi nyingi zenye matumaini ooh! Utahakikisha napata maji , Utahakikisha napata huduma nzuri za afya na utahakikisha umeme ni wa uhakika, Kauli zako wakati unasema ni ngumu mtu kubaini kwamba huna unalo maanisha isipokuwa ni uongo na uzandiki tu mbele yangu. Wewe ni hodari wa kusimama kwenye majukwaa unaimba wimbo wa maendeleo kila baada ya miaka mitano huku unaniacha mimi nikifa na njaa ni lini utatimiza ahadi zako ili nami niishi kwa furaha kila iitwapo leo sioni maendeleo bali ninacho kiona ni ukoloni mambo leo, Eeeeh! Muogope mungu dhamana niliyokupa ya kuniwakilisha mimi itendee haki kwenye michango usimami kuniongelea mimi maskini nisiyejua kesho yangu nakushangaa wewe kwenye vikao unalala na ukiamka kuchangia sioni cha maana bali ni mizaha.

Hivi kweli unania ya dhati ya kutusemea sisi Watanzania? Au nia yako ushibishe tumbo lako, Utembelee usafiri mzuri na uchukue posho ambazo ni kodi yangu kisha uende vyuoni kudanganya dada zetu huku unawachezea kwa zinaa.

Huku jimboni hautokei basi nimeamua kukwambia pengine utasikia, Barabara bado sana ,Elimu sitaki sema wahitimu ni wengi sana ajira bado ni changamoto Eeeeh! Embu fungua mdomo wewe utasikika, Mimi huko nilipo ni mbali sauti haiwezi fika waambie wenzako waliopata nafasi ya kuwa na vyeo viwili wasipime maisha ya watanzania kwa kujiangalia wao. Bali wayapime maisha ya watanzania kwa kutuangalia sisi. Ndio sisi bodaboda, Mama nt`ilie, Fundi viatu na sisi wasomi tusio na kazi wamuangalie mfanyakazi wa kiwandani, Mfanya usafi maofisini, Machinga mitaani ,Fundi seremala na Mpiga debe stendi za Makumbusho na Ununio, Muangalie kijana wa Kitanzania baada ya kumpa elimu isiyo na tija umemtelekeza mtaani, Umemwacha anateseka majukumu yamemzonga, Familia inamtegemea hajui afanye nini. Eeeh! Amka simama ongea Eeeh! Amka simama kemea Eeeh! Amka simama tembea Eeeh! Amka simama waambie hatupo kwenye michezo ya bahati nasibu hivyo wanapofanya maamuzi waiangalie kesho yetu, Kesho ya watoto wetu na watoto wao, Kesho ya wajukuu wetu na wajukuu wao, Kiongozi nakwambia ongea usiogope. Wapi tunashindwa wapi tumekwamaa matatizo hayaishi kila siku rushwa, Wizi wa mali za umma, Ufisadi na unyonyaji nani wakuyasemea haya ikiwa wewe unaogopa?

Eeeeh! Nimegundua yote haya ni sababu ya sheria mbovu ulizozipitisha wewe mwenyewe inakuaje kiongozi mmoja ana nguvu isiyomithilika? kumbe ndio maana waogopa kutuongelea wananchi sababu unajua ukisema ukweli utakosa teuzi. Usiogope mungu yupo na wenye haki usijali teuzi zao wewe ni muhimili unaojitegemea lakini cha ajabu sioni nguvu yako naona kivuli chako sioni mwili wako, Usikubali dharau wewe una mamlaka usikubali kupelekeshwa wewe sio gari la taka.

Wewe ni mwakilishi wa wanachi wewe unatunga sheria wewe unapitisha bajeti wewe unajadili mikataba hivyo wewe ni wa thamani usijivue nguo ulipo ni sokoni kuna watu wengi, Basi hutaki kuvua nguo wameamua kukuvua kwa nguvu sasa mbona wasimama badala ya kuchutama au wewe sio muungwana?

Nakuomba sana usiogope kuongea sema simamia ukweli waeleze ajira ni tatizo waambie elimu ni mbovu sema ufisadi unafanywa waziwazi sema hospitali mambo sio shwari sema yote haya anayeweza kuyaona ni mtoto wa masikini mtoto wa fukara anaye ishi chini ya nusu dola anayeishi kwa kutoa jasho lake anayeishi kwa kukaza misuli yake huku aking`ata meno auvute mkokoteni, Simama sasa nione faida yako zungumza usiogope niandike historia yako onyesha msimamo ili niyaenzi mazuri yako.
Tekeleza niliyokutuma mimi sijakutuma kukuna tumbo na kupiga miayo mimi sijakutuma kuchukua posho za bure mimi sijakutuma kufanya vituko mimi sijakutuma kupiga makofi ovyo kama kwenye matamasha ya burudani mimi nimekutuma kunisemea shida zangu, Hivyo sema usiogope hiyo ndiyo kazi yako.

Najua Unawasiwasi ukirudi kama nitakupitisha tena usiogope fanya niliyokutuma nitakupitisha tena na tena kumbuka nimekutuma kuwakosoa wakubwa hivi unataka kuniambia hakuna wakubwa wanachokosea kama hakuna wewe una maana gani ya kuwa hapo sasa mbona kila kitu wewe ni ndiyo na aliye kuambia ukisema hapana utakuwa umekufuru ni nani tambua ndio nyingi na makofi kedekede ni dalili ya uwoga na sio sifa za kuendekeza kataa kuwa mtumwa unaelipwa fedha nyingi kubali kuwa mfalme unaelipwa pesa kidogo utu na heshima yako italindwa, Kataa kuwa mtumwa kwa sababu mtumwa ni kama mbwa asiye na kwao.
Nina mengi ya kukueleza ila kwa leo nakwambia adui wa mtu ni mtu hivo kuwa makini na jirani yako jirani akicheka sio lazima nawe ucheke bali muulize unacheka nini? akikupa sababu ya msingi basi nawe cheka akikupa sababu ya kijinga usicheke wala usimcheke mwambie jirani kuchekacheka hovyo sio dalili nzuri hasa katika zama hizi za dunia ya mabalaa hivyo elezaneni ukweli na badilikeni.

Mwisho nikwambie hakuna marefu yasio na ncha na mwenda tezi na homo marejeo ni ngamani usipobadilika ukarudi tena nyumbani kunadi sera zako nakwambia sitokusikiliza tena! sababu umenidanganya mambo mengi.
Katiba mpya ndiyo suruhisho CCM nikambi ya kujitoa ufahamu yaani tabia ya unyumbu ambapo wanaofikiri vizuri huahirisha kufukiri kwakulinda masirahi ya kundi fulani, (CCM), ama uoga wa kuogopa viongozi. Herding behavior is an occurrence of thoughtful people suspending their reasoning because of group objective or fear of their leaders
 
Katika mchakato wa kuipata katiba mpya, Nguvu na Ushawishi wa bunge letu ni wa muhimu sana kwa sababu serikali bila kushinikizwa ni ngumu kuruhusu mchakato wa katiba mpya.
Na shinikizo la bunge ndio shinikizo la wananchi hivyo ni muhimu kwa bunge letu kutafakari upya juu ya tija yake kwa nchi hii.
 
Bunge hili linalo wakilisha CCM? hili halikutokana na ridhaa ya wananchi ndiyo maana wa wanalipigia kelele
 
Kosa hiii la kuruhusu chama kimoja kuwakilisha wananchi ni kosa ambalo linaturudia sisi wananchi wenyewe tulikaa kimya na kuruhusu haya yatokee angalau tungesimama kama nchi kupinga , Ila bado tuna nafasi ya kufanya marekebisho uchaguzi ujao.
 
Tunaishi kwenye jamii mfu ambayo haiwezi kupaza sauti inayosikika yaani jamii ya bora liende tumefungwa minyororo na CCM, wao wanadhani wanauwezo wa kufikiri kuliko watanzania walio wengi
 
Dawa ya tatizo hilo ni kutoa elimu kwa wananchi bila kuchoka kusema na kutumia fursa za kufikisha ujumbe bila kujali mwitikio wa wananchi kwa sababu ukiangalia raia wanachukuliaje mambo ya kisiasa utakata tamaa.
Angalau sasa baada ya nguvu kubwa kutumika kufungua watu kuna hatua tumepiga sasa watu wanajaribu ata kuandamana kupinga mambo hadharani japo kwa uchache wao ila ni mwanzo mzuri. Kikubwa ni kutochoka kusema pale unapoona panafaa kusemwa.
 
Ukombozi wa fikra utachukua muda mrefu kutokana na uelewa tofauti wa wananchi
 
unafikiri ni njia gani rahisi ya kutumika ambayo haitachukua muda mrefu katika kuleta mabadiliko ?
Ni kwanjia ya maandishi na kujitolea kuelimisha kama hivi tunavyo fanya mfano mimi nina ubunifu kawanini biashara zinakufa na nini kifanyike, na ubunifu mwingine ni wa jedwari linaloelezea picha halisi ya kwanini biashara zinavyokufa na nini kifanyike na mchawi mkubwa ni serikali nataka nisajili brera baada ya hapo niupeleke COSTECH, naandika pia kitabu cha ujasiriamali ambacho ni fikirishi kinaangaza pia kisichotarajiwa kwenye biashara, (uncertainty in business), kilio kikubwa kiko kwenye major environmental factors namely, National economy and social development strategies of an existing government, social demographic variables ,pollical decisions, technological changes .
 
Ni njia nzuri na hiko ndio cha muhimu lakini pia kujitahidi kuitumia platform hii ya jamii forum vizuri katika kushauri,kukosoa na kupendekeza mambo mbalimbali kwenye jamii na serikali yetu kwa ujumla, Asante kwa mchango wako kwenye bandiko hili na karibu.
 
Back
Top Bottom