unashangaa nini matokeo kupinduliwa?
Mosi, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.
Pili, Viongozi wake wote wa juu ni Wanajeshi
Mwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu: Luteni Yusuf Makamba
Naibu Katibu Mkuu: Kapteni George Mkuchika
Katibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john Chiligati
Meneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman Kinana
Tatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania
Nne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."
Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.
Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni ya utawala wa kijeshi.
Kumbuka mlienda kupiga kura ili kutimiza haki yenu ya kikatiba, narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.
Haya kazi kwenu