Sitooa abadan asilan

Acheni ujinga wenu huu. Tafuteni wake muoe. Kama huna mke huwezi kuwa na akili
 
Ndugu usiseme hivyo tafadhali, ipo siku hao unao kunywa nao bia hawatakuja kukusaidia, ipo siku hiyo pesa haitaweza kuwa nunuwa watu waje wakufute machozi wakati unahitaji faraja ya mwandani wako, iko siku hiyo pesa haitaweza kukusaidia kukutoa ndani wala kukusogeza pindi mwili wako hautakuwa hauna nguvu, nikuombe tu umwombe Mungu wako akupe hekima na busara ktk hilo la kuoa.
 
Kuna muda mwandani wako anakusaidia vitu ambavyo hakuna mtu au ndugu yako yeyote wa damu anaweza kukusaidia.

Oeni vijana mpate baraka ambazo Mungu amezitayarisha kwaajili yenu.

Ndoa hufungua hufungua na kurahisisha vile ambavyo umekuwa ukivitafuta na kuvitamani siku zote.
 
Zamani ilikuwa mtu akiwa kwenye ndoa unaona enhee kweli jamaa anafaidi. Kuna vitu ulikuwa ili uvipate aidha kwa mwanamke au mwanaume lazima uingie kwenye ndoa.
Hujaoa lakini unajua mambo mazuri ya ndoa za zamani. Uliyajuaje?

Acha kujifurahisha wewe, kuoa lazima utaoa umri ukifika. Wewe kwa sasa bado ni mtoto ndo maana una mawazo ya kitoto.
 
Vilaza wenzio walikuwa kama wewe, sawa wako 35 wanakuja na Id mpya yena wa kiume wakitafuta mke wa kuoa ..Hayo ni matakwa na hadhi ya kibinadamu .

Kama unabisha haya ila tambua ukichunguza Kuna wimbi la wanaume pia wakihitaji wenza maana nao kilometers zinashaanza kutembea.

Tafuta pesa uhudumie familia huo ndo uwanaume la sivyo utakuja mvulana
 
Endeleeni kuzalisha nje badae mje muwaponde humu single mothers wa watu...kuoa au kuolewa utabaki kuwa na heshima yake hata mje maelfu kusema ndoa sio jambo jema..kuna kazi zingine mtazikosa au vyeo mtavikosa kisa tuu huna ndoa ya kisheria.
Sahihi
 
Kataa ndoa .... Hatuna stress ni uhalisia ... Vijana kataeni ndoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu, chochote kisicho na thamani/umuhimu ubongo wetu umeumbwa kupuuza na kusahau
kama ulivyoshusha mzigo leo asubuhi uka flash fasta ukaondoka ukasahau hujaja kupost JF

Au ulivyokaa kwenye ndinga yako akapita machinga anauza maepo hukununua umesahau hujapost jf

Au ulivyoondoka nyumbani bila kumgongea jirani kumsalimia


Vipi ingekuwa umeondoka hujamsalimia mkeo kitandani? Dhahiri ungesumbuka siku mzima kwasababu ya ugomvi mlio nao ambao akilini unajua hampaswi kuwa na ungomvi,

Ndoa ni kitu kiko akilini mwenu muda wote wanaume wa JF, kukosa ndoa kunawatesa sana, makala na mijadala mirefu ya kuponda ndoa na wanawake kila siku kwasababu ni jambo linasumbua akili zenu

Lingekuwa ni jambo mlilopuuza kusingekuwa na makala hata moja kuhusu ndoa na wanawake nakuhakikishia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…