MSAJILI wa Vyama Vya Siasa John Tendwa amesema hatosita kukifuta chama chochote cha siasa ambacho kitaonekana kukosa wanachama wanaofikia 2,000 kama sheria ya usajili wa vyama vya siasa inavyotaka.
Kauli hiyo ya masikitiko kwa baadhi ya vyama aliitoa wakati akizungumza na mwandishi wa Nifahamishe ikiwa ni baada ya kutoa cheti cha usajili wa muda kwa chama kipya cha kisiasa cha Peoples Democratic Movement (PDM) ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Alisema sheria ya usajili wa vyama vya siasa inamruhusu Msajili kusajili vyama vingi kwa lengo la kukuza demokrasia lakini pia inampa mamlaka kukifuta chama ambacho kinakosa sifa.
Msajili alisema sheria inakitaka chama kuwa na wanachama wasiopungua 2,000 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ambapo nane ni Bara na miliwili kutoka Unguja na Pemba.
"Nawahakikishia nyie PDM na vyama vingine kuwa kama hamtatimiza masharti ya kuwa na wanachama 2,000 katika mikoa 10 ya Tanzania sitosita kuwafuta," alisema.
Msajili huyo wa vyama vya siasa nchini alisema kuwa kwa sasa ofisi yake ipo kwenye mchakato wa kutembelea mikoa ili kuangalia uhai wa vyama vya siasa nchini.