calory
Member
- Apr 29, 2013
- 31
- 6
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amebadili kauli yake ya awali, kwamba katiba mpya iondoe viti maalumu kwa kuwa wabunge wa viti maalumu hawana umuhimu wowote.
Kauli hiyo ambayo aliitolea Busega mkoani Simiyu, na kunukuliwa na vyombo kadhaa vya habari, imekuwa inapingwa na wananchi kadhaa, hasa wabunge hao wa viti maalumu.
Juzi akiwa mjini Tabora, Sitta alikanusha habari hizo akisema zinalenga kumchonganisha na wabunge wenzake. Alienda mbali na kudai vyombo hivyo vinaathiriwa na washindani wake kisiasa, hasa wanaotafuta urais.
Nimebaini kuwa upotoshwaji huo ni sehemu ya mkakati wa kundi la kisiasa ambalo kinara wake anatafuta urais huku akibebwa na marafiki matajiri, alisema.
Kauli hii mpya ya Sitta inaweza kulinganishwa na kilichomtokea mke wa Lutu kwenye simulizi za Kibiblia, aliyegeuka jiwe la chumvi baada ya kugeuka nyuma kutazama mji wa Sodoma ukiungua, kinyume cha ushauri wa malaika na msimamo wake wa awali.
Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge wa zamani na mbunge wa Urambo Mashariki, alisema kuwa amebaini upotoshwaji huo ni sehemu ya mkakati wa kundi la kisiasa ambalo kinara wake anatafuta urais wa nchi kwa udi na uvumba.
Waziri huyo machachari ambaye amekuwa na kauli nzito dhidi ya wapinzani wake kisiasa, alisema kuwa katika uchunguzi wake amebaini upotoshaji mkubwa na wa makusudi juu ya mambo aliyotamka na kunukuliwa kuhusu wabunge kutotembelea majimbo na yale yaliyohusu hatima ya wabunge wa viti maalumu katika katiba mpya.
Kwamba amebaini kuwa mhariri wa gazeti hilo lililomnukuu anapokea malipo ya kila mwezi pamoja na bonasi kwa kazi maalumu kutoka kwa mwanasiasa mmoja japo ambaye hata hivyo hakumtaja jina.
Njama hizi ni mwendelezo wa vita dhidi yangu kutoka kundi la wanasiasa nililolitaja ambalo limepania kununua urais wa nchi yetu, alisema.
Source: Tanzania Daima