Sitta ajiingiza BoT

Mkuu Bongolander/Ogah,

Kwa kawaida huwa ninaheshimu sana mawazo yako, lakini recently sijui kama kuna mtu ameiba code yako mkuu!
 
Mkuu Bongolander,

Kwa kawaida huwa ninaheshimu sana mawazo yako, lakini recently sijui kama kuna mtu ameiba code yako mkuu!

Nakupata mzee ES, i did not mean to offend, ni maoni tu maybe nimetoa kwa ufupi kwa sababu hapa bongo sasa usiku, usingizi tena. Lakini ninachoona kwanza ni kuwa hawa jamaa lazima wakubali wajibu wa pamoja, kabla ya watanzania hawajaanza kusema kwenye kindi hili fulani hakuwepo na fulani hakuwepo. For sure si kweli kuwa kila mtu ndani ya CCM ni fisadi, na ukiangalia kwa undani unaweza kuona wazi kuwa watu waliomstari wa mbele kwenye true fight against against graft wanatoka CCM na serikalini, kina Slaa wanatumiwa tu kama midomo ya kusema waliyoandaa wengine.
My point is, CCM ambacho ni chama tawala kime-foresee the whole thing from the very begining to now. Kwa hatua hii hatuwezi kuanza kusema huyu hapana huyu ni yeye, at this moment chama as collective entity lazima kikubali responsibility kwanza, and then kijisafishe na tujue ni kiungo kipi kilikuwa na matatizo.
The point i am trying to make is, at this moment, in order to clean the house we must first admit that it is dirty. Tukisema fulani ni fulani na fulani hayumo inakuwa kama utoto. Personally naona spika Sitta kama anafanya mchezo, au anajaribu kujikosha kwa kusimamia na kujaribu kuficha ufisadi, kwa aliyowafanyia Slaa na Zitto.
 
mama weee.. mbona timu ya Taifa ilipoinyuka (I know you haven't heard that world for long time) Burkinabe tuliambiwa ni matunda ya sera "nzuri za CCM". Mkitaka kusiwa kwa maua, hamna budi kusiwa kwa miiba yake pia!
 
Inawezekana Mzee alivyo sema alikuwa kapata wanzuki iliyowekewa anitbiotics zile zenye rangi mbili, kwa sababu wenye kuongoza ni serekali ya CCM, appointment za viongozi zinafanywa na serekal;i iliyo chini ya chichiemu, report za uchunguzi zikitoka zinakaliwa na serekali ya chichiemu, chichiemu inavikao vyake iwe cha halmashuri kuu au ya kamati kuu etc lakini hatukuwahi kuwasikia wakiliongelea hili suala au kulilaani, na kuwaadhibu wale wanachama wao waliohusika na hii kadhia.
Sasa leo wanataka kukimbia kivuli chao.
Pili hili suala la BOt lilifikishwa Bungeni, lakini wenzetu wakalipinga kisiasa ( kwa kuwa Chichiemu wako wengi Bungeni) badala ya kusikiliza hoja iliyowakilishwa. Na kinara wa ubabaishaji huu alikuwa Muheshimiwa Chupika wa Bunge Letu Haramu oh no tukufu.
Au yeye chupika na wenzie watuonyeshe juhudi walizo chukua kulipinga hili jambo, kama sio Donors, waliosema No msaada wala Nkopo mpaka tujue nini kilicho tokea BOT
 
Mkuu Bongolander/Ogah,

Kwa kawaida huwa ninaheshimu sana mawazo yako, lakini recently sijui kama kuna mtu ameiba code yako mkuu!

Duuuhh Mkuu FMES!!!!..............haya bwana...........what a damage!!, Invisible shahidi wangu
 
Serikali ya SISIEMU imejaa uvundo utoao harufu kali isiyovumiliwa hata kidogo.
Sisi tulioko nje ya tunaona serikali yote ya SISIEMU inanuka. KWa vile serikali inaundwa na chama cha SISIEMU, pia tunhisi chama hicho kiinanuka uvundo wa uoza.

Kwamba kuna wana SISIEMU 10 au 1000,000. wenye kutoa harufu hiyo kali ya uvundo, au Wana SISIEMU wote mmeozeana mnanuka na kunukiana hiyo ni siri yenu wenyewe huko ndani na sera zenu zisizo tekelezeka.

Kutueleza kwamba BOT siyo SISIEMU ni sawa na kusema wamba serikali ya SISEMU na chama cha SISEMU havina uhusiano.

Ondoeni hao wachache mdhanio watoa uvundo na kukifanya chama na serikali yenu kutoa harufu mbaya tuone kama harufu ya uvundo huo itakoma.
Hizi kelele zenu kwamba Wanachama wa SISIEMU hamnuki wote hazisaidii hata kidogo bali zinaonyesha kwamba harufu hiyo mwaipenda na mwailea vile vile.

KWa dhana hiyo kwa nini tusiseme wote mnanuka?
 
Mkjj hiyo timu ya Taifa si afadhali what about mshindi wa big brother ambaye ushindi wake tuliambiwa ni sera nzuri za chama cha mafisadi (CCM)? Yaaani hawa ni vituko kweli mazuri yote yao hata yakiwa yakipuuzi na hayawahusu na and then mabaya yoooote si yao hata kama yanawagusa moja kwa moja.

Sita me si leo tu,muda sasa huyu mzee simwelewi kabisa maana tatizo hapa ni zaidi ya itikadi kwani itikadi haikutoi ubungo unless umeamua mwenyewe. Hivi TZ kama nchi kwa kutokuwa na rais,waziri mkuu na spika si kwa majina bali kwa kokosekana kwa utendaji na hekima ya uongozi (leadership wisdom) tunaelekea wapi??
 
Es naona anaanza kuvamia watu sasa . Ogah pole sana . Kisa CCM inasemwa vibaya duh!!! Nangoja aseme ukweli kule maeneo juu ya Botswana .Anapashwa kusimamia ayasemayo na si kuvamia vamia watu .Nangoja kule aseme hili la Botswana .
 
hIVI HUYU sITTA ANATUFANYA SISI WATOTO. WAKATI SLAA ANAHANGAIKA KUPELEKA HOJA AKAWA WAKWANZA KUPINGA KWA KULETA MIZENGWE,VIONGOZI WA CCM NDIYO WANAOHUSIKA NA HILO SAKATA WATAKE WASITAKE,MBONA MRAMBA YUKO KIMYA SIYO WA CCM HUYO, MR CLEAN AND ANBEN,TANPOWER SIYO WA CCM HAWA? nona Sitta analeta upumbavu tu hapa
 
Halafu alijinadi kwamba ni spika wa Standard and Speed. Tangu ameanza kuongoza bunge mpaka leo sijaona the so called standrd and speed katika leadership yake. Mtu mzima ovyo.
 
Halafu alijinadi kwamba ni spika wa Standard and Speed. Tangu ameanza kuongoza bunge mpaka leo sijaona the so called standrd and speed katika leadership yake. Mtu mzima ovyo.

Ile ilikuwa ni lugha ya kampeni tu, kama ilivyo "Maisha Bora Kwa kila Mtanzania", ama "Tanzania Yenye Neema Inawezekana".
Kauli zote hizo huwa haziendani na ukweli wowote, wala usizipe uzito sana.
 
Halafu alijinadi kwamba ni spika wa Standard and Speed. Tangu ameanza kuongoza bunge mpaka leo sijaona the so called standrd and speed katika leadership yake. Mtu mzima ovyo.

Mtani wangu Mndamba vipi perege na vitoga huko? Kivuko chenu cha mto Kilombero Muungwana si aliwaahindi kuwajengea daraja? Hawa jamaa wote wazushi na serikali yao..hakuna cha standards ,speed wala maisha bora kwa kila Mtanzania maisha bora tutajiletea wenyewe tutakapo amua kupambana na Mafisadi na kugawana utajiri wa nchi yetu hii ni pamoja na kubadili uongozi uliopo wewe Mndamba hakikisha Ngasongwa harudi tena bungeni. Hebu fikiria Mzee Mwanakijiji anakuwa spika na akina Lunyungu, Ushirombo, Zito, Slaa,Mwanamke, ES,Mushobozi, Bubu etc wabunge na Kitila Mkumbo anakuwa Lowasa nchi si itakuwa peponi ? ama nao wanaweza ambukizwa ufisadi? teh tehe teh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…