Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Mwanzo mbaya unamwisho mbaya. Sitta amedhihirisha kuwa hawezi kuliongoza bunge la katiba. Pamoja na kuwa ametengenezewa kanuni na watangulizi wake ambao waliongoza bunge la katiba vizuri bila kanuni, yeye ameanza vibaya kwa kuvunja kanuni zilizotungwa na kupititishwa na bunge hilo.
Napendekeza wabunge wa bunge maalumu wamwondoe na wamchague Mheshimiwa Pandu Amer kificho ambaye anaiweza kazi hiyo. Kificho yeye anafahamu kuwa katiba inapatikana kwa maridhiano kama mheshimiwa Mbatia na wengine walivyosisitiza mara nyingi. Ubabe wa Sitta hauendani na maridhiano na hivyo hawezi kuongoza bunge hilo. Baada ya kuchaguliwa Mh. Pandu Amer Kificho kuwa mwenyekiti, inabidi uchaguzi wa makamu mwenyekiti ufanyike ili apatikane mwanamke kutoka Tanzania bara.