Sitta awaomba radhi UKAWA kwa ubabe wa jana: semina za Msekwa na Mapuri zafutwa

Sitta awaomba radhi UKAWA kwa ubabe wa jana: semina za Msekwa na Mapuri zafutwa

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
Hatimaye mwenyekitiwa bunge Samwel Sitta amekutana na viongozi wa UKAWA na kuwaomba radhi kwa ubabe aliotaka kuutumia jana hatua iliyosababisha bunge jusambaratika na Warioba kushindwa kuwasilisha hotuba yake.

Sitta amewahakikishia viongozi wa UKAWA kuwa hatarudia tena tabia ya ubabe na atahakikisha anafanya nao makubaliano kabla ya kuchujua hatua yoyote ndani au nje ya bunge.

Aidha sitta pia amefuta semina ya siku moja ambayo watoa mada aliokuwa amewapanga kuja kuwafunda wajumbe kuhisu muungano ni Pius msekwa na Omar Ramadhan Mapuri.

Msekwa na Mapuri ndio watoa mada ambao sitta aliwaalika waje kuwafunda wajumbe qa bunge la katiba maswala ya muungano kwa madai kuwa wawili hao ndio magwiji wanaojua muungano kindakindaki.

Sasa wawili hao ambao tayari wapo hapa dodoma hawatakuwa na la kufanya licha ya semina inayowahusu Amos Wako wa Kenya itafanyika alhamis kama ilivyopangwa.
 
Ha ha ha wamesoma alama za nyakati
Chezea nguvu ya Mungu.
 
sawa sawa aache kabisa ubabe maana tunataka katiba ya wananchi na yeye ni mtu mhimu sana katika hili
 
Hii ni katiba ya wananchi na sio ya chama chochote cha siasa, mapuri na msekwa ni maccm walewale!
 
samwel akileta ujanja wa mwaka 66 atadhalilika vibaya sana !
 
Tatizo la wanasiasa wa tz ni wanafiki ukwa walidhamiria kukwamisha hotuma ya warioba tangu awali kwa sababu muda aliopangiwa kuongea asingepata nafasi ya kujenga hoja ya serikali tatu ni ambayo dhahiri itavunja muungano
 
Warioba kawa ambia vizuri asiye taka kuchangia basi hataki muungano, na ni vyombo vya dola, polisi na ma jeshi
 
Kama ni ya kutoka moyoni,basi amejisahihisha makosa na ataongoza bunge vzr kama matarajio ya waliompigia kura
 
Waswahili husema "mkunje samaki angali mbichi" hivyo hawa wabunge wazalendo wamefanya vizuri kumkumbusha Sitta kuwa wao sio wa kuburuzwa!!!
 
UKAWA vs CCM. Nshaanza kuona ya Orange vs Banana kipindi kile Kenya...
 
Warioba kawa ambia vizuri asiye taka kuchangia basi hataki muungano, na ni vyombo vya dola, polisi na ma jeshi
CCM wana kiburi watajifanya hawajamuelewa ili serikali mbili zao zirejee
 
Kwa nini asiwaalike watu wenye taaluma ya sheria kama Prof. Issa Shivji?
 
Back
Top Bottom