Na bado watu wengi tu wanaendelea kuiaminin serikali ya kisanii namna hii!!!!! Hv hii ni laana nini???????
HIvyo utaona kuwa ziara anayokuja nayo Marekani hususan kuhusu kuliboresha Bunge lengo lake ni jinsi gani ataiinua ofisi ya Spika ili ionekane sawa na kulazimisha kujadiliana na Rais kuhusu mambo mbalimbali badala ya sasa ambapo Rais anaweza kuamua nini kifanyike Bungeni.
Hivyo basi, kauli yake kuhusu Richmond na BoT siyo ya bahari mbaya, he is basically asserting his power as the Speaker and flexing his muscles. Hajafanya kwa bahati mbaya, na akitaka kuwaweza ni pale ambapo atakaporudi na kuamua kuwa mambo haya ni mazito na muda hautoshi kwa mjadala kwa hivyo anaamua kwa "busara zake" (sasa hivi busara ziko kisheria na kiutaratibu) hadi mkutano wa Aprili.
Hapo ndipo Watanzani watatambua embe ni tunda, na nyanya ni kiungio!
Spika ana nguvu mno and you do not want to piss him off. Wawaulize wapinzani.
Sitta amkataza Makinda kujadili BoT, Richmond
Mapema asubuhi Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliwaomba radhi wabunge kwa kushindwa kutoa nyaraka muhimu kwa wabunge, ikiwemo ripoti za Richmond na ya EPA ili waweze kuzipitia kabla ya kujadiliwa kwa maelezo kwa hali hiyo ilisababishwa na sakata la BoT linaloendelea.
Waziri Mkuu alikuwa akitoa ufafanuzi baada ya kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamadi Rashidi kuomba muongozo wa Spika kutaka Wabunge wawe wanapatiwa nyaraka muhimu na kuzisoma kabla ya kuingia bungeni.
Akitoa ufafanuzi juu ya sula hilo Waziri Mkuu alisema kuwa kwa muda mrefu Gavana Mkuu wa BoT, alikuwa mgonjwa na kwamba kutokana na sakata linaloendelea katika benki hiyo mambo hayajakaa vizuri,alisema Waziri Mkuu
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, suala la BOT lilishafanyiwa uchunguzi wa awali na Deloitte Touch, akaja CAG na mwishowe wakapewa E&Y kuchunguza. E&Y walifanya uchunguzi huku Gavana Ballali akiwa hayupo nchini na matokeo ya uchunguzi wao umefikia hatua ya Rais kumuengua Ballali kutoka kuwa Gavana baada ya kupata ripoti hii. Mheshimiwa Waziri Mkuu, mimi sioni tena sababu ya kuendelea kwa Serikali kuu kuchelewesha kuwasilisha ripoti hii Bungeni na sababu ulizotoa hapa za ugonjwa ni irrelevant. Kama Rais alisharidhia na kuagiza Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Polisi na TAKUKURU walifanyie uchunguzi wa jinai, ni vipi utuambie kuwa kwa kuwa Ballali ni mgonjwa hivyo suala hili lina utata? Je tutaamini vipi kuwa Serikali iko makini kama yakataa ama yachelewesha kuwasilishwa kwa ripoti hii Bungeni? Je wananchi watueleweje Mheshimiwa Lowassa?"