Yote tisa, swali moja tu kwa Sitta -Mbona mmeitambua Symbion walirithi wengine wa mitambo ile ile yenye historia ya Richmond??
Mkuu Mkandara, hebu twende taratibu hapa.
RICHMOND ilikua na MKATABA BATILI. DOWANS wakaja kuurithi huo MKATABA BATILI toka kwa Richmond kinyemela. Kumbuka hapa hakuna suala la Mitambo. Ni suala la kurithishana MKATABA BATILI. Ni matter of principle tu kuwa haramu haiwezi kuzaa halali. Na hapa ikumbukwe Mitambo ya DOWANS haikua mipya.
Serikali ilipotaka kununua hii mitambo kutoka kwa DOWANS, wakabanwa na Sheria ya Manunuzi ya Umma inayokataza serikali kununua mitambo
chakavu. Nadahani tuko pamoja mpaka hapo.
DOWANS wakaamua kutafuta mnunuzi wa MITAMBO yao iliyokuwepo Ubungo na sio Kampuni ya kurithisha MKATABA. Hapa ndio SYMBION ilipoingia na kuinunua MITAMBO kutoka kwa DOWANS. Ukumbuke hapa walinunua MITAMBO sio Kurithi MKATABA wa Dowans.
SYMBION ikawa approach UPYA Tanesco, na kuomba MKATABA MPYA ambao una best prices per KWH kati ya mikataba yote ya Tanesco. Tanesco wakaingia mkataba MPYA na SYMBION. Hapa mmiliki wa MITAMBO chakavu ni SYMBION ila anawauzia umeme Tanesco. Hivyo inachonunua TANESCO ni UMEME. Na ndipo mama Clinton alikuja kwenye uzinduzi wake.
Sasa hapa sijui ugumu wa kuelewa kilichotokea unatoka wapi?
Sijui tatizo ni kutokuelewa kilichojiri, au kuchanganya mambo, au kupotosha kwa makusudi au kwa vile ni Samuel Sitta.
Jamani, tujaribu kuwa fair na objective. Hao wasiokua wanafiki waliojazana huko CCM na hawaoni kama haya malipo
ya DOWANS ni wizi wa mchana sijui ndo ma hero wenu au vipi, mi sijui...