Sitta: Katiba nzuri ni dawa ya kuua sheria mbovu

Sitta: Katiba nzuri ni dawa ya kuua sheria mbovu

Getstart

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
6,658
Reaction score
2,235
Swali: Unafikiri nini sababu ya kuandaa Katiba Mpya?
Jibu: Katiba nzuri ni dawa ya kuua sheria mbovu. Moja yatatizo la Katiba tuliyonayo sasa ni kuacha mianya na hivyo watu kujifanyiamambo wanavyotaka pia uwajibikaji unakuwa mdogo.
Hii Rasimu ya Katiba tunayokwenda kuijadili inasisitiza zaidiutumishi wa umma. Inawajali watu wote hasa wanyonge.
Tukiwainua wanyonge, nchi yetu itapata baraka na maendeleo.Pia tukiwa na mshikamano na umoja, ni wazi kuwa wanyonge wataona kuwa viongoziwao wanahangaikia matatizo yao.
Vijana, makundi maalumu, wanawake waliopo mijini na vijijiniwana matatizo mengi ambayo lazima kama viongozi,tuyatatue.
Watuhao wanatakiwa kuona kuwa Katiba Mpya inapatikana na hivyo kusaidia kutungwakwa sheria nzuri ambazo zitakuwa na makali ya kutosha kuzuia rushwa na uzembe.
Pia kuwa na sheria ambazo zitasaidia mahakama zetu kutoaadhabu zinazostahiki kwa watu wazembe.
Hivi sasa mahakamazinazingatia zaidi hoja za kiufundi badala ya kuwa na mwelekeo wa kutatuamatatizo halisi yaliyopo. Hukumu nyingi zinazotoka ni za dhulma na mwishowewananchi wanaamua kuchukua sheria mkononi.
Source: Gazeti la Mwananchi (13 Machi 2013)

Maoni Yangu: Ikiwa aliyekuwa Kiongozi wa Bunge na kiongozi mwandamizi ndani ya Serikali anasema na kuamini hivi basi ninaingiwa na wasiwasi wangu dhamira yake kama si unafiki. Sheria mbovu zimetungwa si kwa sababu Katiba tuliyonayo inaruhusu la hasha. Nyingi zipo kulinda maslahi ya serikali iliyoko madarakani. Hivi unahitaji Katiba mpya kufuta sheria zote mbovu zilizokwisha orodheshwa na tume nyingi, ikiwemo iliyoongozwa na Jaji Mkuu, na kulalamikiwa na watu. Katiba Mpya haitafuta au kuzuia kutunga sheria mbovu, kinachohitajika ni dhamira ya wabunge isiyoongozwa na misimamo ya vyama vya siasa au kuegemea matakwa ya Serikali iliyoko madarakani. katiba Mpya haitabadilisha mfumo na matendo ya Polisi ikiwa hatutakuwa na uwajibikaji wa dhati kila sehemu ya maisha yetu!
 
Back
Top Bottom