Sitta: Waziri Simba kalikoroga


ikiwa she is the minister and chairman wa most important wing ya ruling part, anyone in the world will take that she is the best. AND THAT IS IT, PERIOD!!!!!!!!!!!!! huwezi ukaseparate kiurahisi hivyo.

Chama chake kimeona anafaa na ni bora kuliko all the womens ndiyo maana kimempa umwenyekiti, and because she is the best of all in her part amepewa uwaziri wa UTAWALA BORA!!! kwa mba SOFIA SIMBA ni BORA kwa satandard za ki si si emu.

Ukibisha, bisha tu kwa sababu ulizaliwa ili uwe mbishi.
 

We unataka waziri Simba awe ignored sababu according to you yule Mama hana dira wala mwelekeo, lakini ni bado waziri wa nchi - tena wizara nyeti sasa kama kuna swala la msingi la kujibu au kuelezea kwa nini spika asisema?

Sioni tatizo la mwandishi na majibu ya Sitta - unless.....una jambo lako chief.

Great job Samwel... nafikiri mkuu hujui chama chao pia kina makundi mawili - thinkers na vipepeo....
 
Ulifuatilia vyombo vya habri vya jana?Soma magazeti ya jana utapata jibu.


AG: Naunga mkono muswada wa Simba ni ule unaompunguzia Rais madaraka
Mwandishi wetu, Dodoma
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema amesema kuwa anaunga mkono muswada wa Sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa wa mwaka 2009 akisema si mbaya.

Muswada huo, uliowasilishwa Jumamosi iliyopita na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba, ulikataliwa na Bunge kwa hoja kuwa unapunguza nguvu za rais na unamweka rais katika hatari ya kuondolewa wakati wowote na Baraza la Usalama.

Lakini Jaji Werema alisema jana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuwa haoni ubaya kwenye muswada huo.

"Muswada si mbaya, lakini umerejeshwa kutokana na wabunge kutaka baadhi ya vipengele, hasa cha ukubwa wa baraza na Usalama na maamuzi ya mwisho virekebishwe," alisema Werema.

"Hakuna haja ya kujinyonga kwa kuwa muswada umekataliwa, zipo 'altenative' (njia) nyingine. Lakini muswada si mbaya, kazi yangu ni kuwasilisha miswada na kuwashauri mawaziri, si kutunga sheria. Wabunge ndio wana wajibu wa kutunga sheria na wametoa mapendekezo urekebishwe... kamati husika inafanyia kazi na utaletwa tena bungeni," alisema Jaji Werema.

Alisema kimsingi walichokifanya wabunge ni haki yao kama watunga sheria, lakini muswada huo hauna tatizo kama ulivyopitishwa katika michakato yote inayohitajika.

Mchangiaji wa kwanza baada ya muswada huo kuwasilishwa, Brigedia Hassan Ngwilizi alisema kuwa Baraza la Usalama linachukua ukubwa wa baraza la pili la mawaziri, jambo ambalo linatishia usiri wa mambo ya usalama wa nchi.

Ngwilizi pia alisema kuwa kipengele kinacholipa baraza nguvu ya kupiga kura ili kupitisha maamuzi makubwa kama ya kwenda vitani, kinamfanya rais, ambaye ni amiri jeshi mkuu, kuwa katika nafasi sawa na watu ambao wanatakiwa kutekeleza maamuzi yake, jambo ambalo linapoteza maana ya dhana nzima ya usalama wa taifa.

Pia kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid alikwenda mbali zaidi na kuuita muswada huo kuwa wa kihaini kwa sababu linawapa wajumbe wa Baraza la Usalama mamlaka ya kupiga kura ya kumuondoa rais.

Waziri Simba alikubaliana na hoja za kuondoa muswada huo.
Naye Simba aliiambia Mwananchi jana kuwa ameridhika na muswada aliouwasilisha bungeni.

Alisema kupingwa kwa muswada huo kumetokana na makosa ya kiufundi baada ya kutopitishwa kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayohusika na suala hilo na badala yake kupitishwa na kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba tu.

Waziri Simba alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana katika mahojiano na Mwananchi ikiwa ni siku mbili baada ya muswada huo kupingwa na wabunge wakitaka kuondolewa kwa vipengere vinavyoingilia madaraka ya Rais.

"Niliusoma, niliridhika na muswada wa Sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa, Siwezi kuleta kitu ambacho sijaridhika nacho," alisema Waziri Simba.

Aliongeza kusema kuwa "kuna tatizo sisi wahusika tuliliona, awali muswada huo haukupitia kamati husika ya Mambo ya nje Ulinzi na Usalama. Kuna tatizo... ofisi ya bunge, ilipaswa kuupeleka katika kamati hiyo ambayo ingepitia kwa pamoja na kamati ya bunge ya sheria na mambo ya katiba."

Hata hivyo, alisema kwa kuzingatia kanuni za bunge na kusikiliza maoni na michango ya wabunge, kwa kutumia busara na taratbu zilizopo aliahirisha hoja hiyo ili atafakari michango ya wabunge.

Wakati huo huo serikali imeahirisha mjadala wa sheria ya udhibiti wa matumizi ya fedha za uchaguzi uliokuwa ufanyike leo hadi Jumatatu ijayo kutokana na marekebisho madogo yanayofanywa katika muswada huo.
 
Hume,
Watu humu wanamshupalia SS peke yake. Kuna AG, BlM na Kamati za Bunge anazoziunda Spika mwenyewe.
 

Usichanganye masomo ndugu. Anyway haya nakubali yaishe. Nashukuru kunikumbusha kuwa alipewa uwaziri baada ya uenyekiti wa UWT na sio vice versa! Haya sawa.
 
Ndio maana tunalilia vetting ya wateuliwa wa rais ianzishwe kwenye bunge ili kuepuka kuongozwa ma mazuzu pale ambapo tunalazimika kutawaliwa na rais asiyekuwa na uwezo.

Naam; wenzetu wanafanya vetting hadi kwa mabalozi; nafikiri kuna haja ya kufanya vetting kwa kada zote za uongozi wa umma; labda tutawaacha walimu na mdaktari wakuu
 
....Kwa Sofia na siasa za CCM,nataka ukubali yeye anawakilisha kundi kubwa la wanawake kwa kuzingatia yeye ndio mwenyekiti wa ccm wanawake.
So she is the best ever woman a CCM has.
Sorry Gender Sensitive that is opinion

its funny put lakini ndio ukweli... she had the highest votes kutoka kwa wanawake wa CCM, na ndie kinara na mwkilishi wa wanawake woooote wa CCM duniani
 
Naam; wenzetu wanafanya vetting hadi kwa mabalozi; nafikiri kuna haja ya kufanya vetting kwa kada zote za uongozi wa umma; labda tutawaacha walimu na mdaktari wakuu
Mkifanya vetting ya kwelikweli vyeo hivi mtampa nani?
 
Naam; wenzetu wanafanya vetting hadi kwa mabalozi; nafikiri kuna haja ya kufanya vetting kwa kada zote za uongozi wa umma; labda tutawaacha walimu na mdaktari wakuu

Mkuu imeandikwa sehemu kwamba sisi tunafanya "Venting" na sio vetting... please take a note of that... it is venting for us!!!
 
Mkuu imeandikwa sehemu kwamba sisi tunafanya "Venting" na sio vetting... please take a note of that... it is venting for us!!!

Nafikiri Simba anaonewa. Mimi naamini tatizo siyo yeye, bali ni la aliyemuweka. Simba binafsi uwezo wake ndipo ulipofikia na inawezekana angependa kufanya vizuri zaidi. Hivyo, udhaifu wa kazi yake tusimtupia yeye, bali ni udhaifu wa aliye muweka.

Kama Rais anauchungu na nchi, na ana nia ya kuwasaidia wa Tanzania, kitu cha kwanza ambacho atafanya/angefanya ni kuunda baraza zuri la mawaziri.
Ukitaka kujua rais hayuko serious, ni kutazama baraza lake. Hakuna kinginge, otherwise tutamuunga mkono Prof. Mbele anayemsifia rais.
 
Mh. Sitta hapa hakufanya sawa. Hakutakiwa kujibizana na Simba yeye angemwacha tu aongee. Sitta naye anataka kujiangusha kwa kuanza kujibizana nje ya bunge na mtu ambaye amekuwa mpaukaj!!!!!
 
Jamani kuna mtu mwenye details kuwa mswada wenyewe uli-contain nini haswa?? Then tunaweza kuanalyse kama kulikua na umuhimu wa kuukataa kwa maslahi ya nchi. Mwenye undani wake tafadhali tuwekee hapa.

Mkuu walitaka kudesign kitu kama COBRA in UK
yaani madesa mengine mpaka yanaudhi
baada ya kudesa kuwa na uchumi bora unadesa kitu ambacho hata baraza la mawazira linaweza kukifanya
 
Mh. Sitta hapa hakufanya sawa. Hakutakiwa kujibizana na Simba yeye angemwacha tu aongee. Sitta naye anataka kujiangusha kwa kuanza kujibizana nje ya bunge na mtu ambaye amekuwa mpaukaj!!!!!


"Sitta amelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa kwamba kulikuwa na msuguano mkali kati ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na ile ya Katiba, Sheria na Utawala."

Tuna haki kama wananchi kupata clarifictions za haya mambo directly kutoka kwa spika. Mimi sijaona kama ni majibizano bali ufafanuzi na kuweka mambo wazi.
 

sawa mkuu lakini tuangalie jambo moja... hivi kuna haja ya kila kitu kujibu tena kwa kupitia waandishi? kwanini asiandike tu barua!!!

Unajua walimmalizaje huyu mama lile sakata jingine la uropokaji?
 
Tabu yoote hii sio Sophia simba ni JK kwani haoni mama huyu anafaa kwenye mipasho tuu? Technical know how hawezi, but amemwacha tu pale au yeye ndo kamtuma hayo?
 
....Kwa Sofia na siasa za CCM,nataka ukubali yeye anawakilisha kundi kubwa la wanawake kwa kuzingatia yeye ndio mwenyekiti wa ccm wanawake.
So she is the best ever woman a CCM has.
Sorry Gender Sensitive that is opinion

Mkuu Shaycas
Hapa hatumjadili Sophia Simba kama Mwenyekti wa UWT ya CCM,tunamjadili kama Waziri...haina mahusiano na ujinsia wake.
 
Nadhani tusikite ktk kumuonea SS nijuavyo muswada unapita hatua mbalimbali.
hata hapo kwa bunge kama sitta aliyaona hayo basi kwa kujiridhisha angeupitisha kwa hizo kamati misigano hii hata sitta mwenyewe inamwaribia hatuoni hiyo standard i wapi labda spidi.
kumbukeni speed bila umakini(standard) ni maafa chukueni mfano wa madereva
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…