Siyo kila mchezaji mkubwa anaweza kuwa kocha mwenye mafanikio

Unaandika halafu unakataa kuwa havipo haya hii kauli umeitoa wewe au sio wewe au uliandikiwa na mtu?

Ili mchezaji aweze kuwa kocha mzuri inabidi awe na IQ kubwa ya kimpira yeye kama mchezaji kwanza. Kupima IQ ya kimpira inabidi uwe na jicho la kuangalia mchezaji anavyocheza uwanjani. Naangalia uwezo wa kucheza position zaidi ya moja uwanjani, uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na ya haraka akiwa na mpira, anavyojiposition anapokuwa hana mpira, uwezo wa kuusoma mchezo na kuiendesha timu uwanjani.
 
Kabla hatujaendelea tafadhali mtoe Method Mogella "Fundi" maana yeye alifariki mapema hata mipango ya kuwa kocha hajaifikiria.
 
Hivi mtibwa wakati inachukua ubingwa mara 2 ilikuwa chini ya kocha yupi?
John Simkoko

Hapa sasa hivi nimetoka kuangalia interview yake, ni kocha mzawa wa mwisho kuongoza timu kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania, zaidi ya miaka 20 iliyopita. Mwisho hapo kwenye video kaulizwa swali position aliyokuwa anacheza, amesema alikuwa anacheza nafasi nyingi, kuanzia beki, kiungo hadi ikibidi alikuwa anacheza kama mshambuliaji.

Kwa hiyo hauwezi kushangaa uwezo wa mtu kama huyu akiwa kocha na hii ni factor mojawapo kubwa.


View: https://youtu.be/aiGMFxUbmQ0?si=efAwvZAhl4Yt-b5f
 
Unaandika halafu unakataa kuwa havipo haya hii kauli umeitoa wewe au sio wewe au uliandikiwa na mtu?
Punguza makasiriko na pia jifunze kujenga hoja maana sijui hata unaongea nini. Soma vizuri mbona vitu viko simple tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…