JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,744
Endapo baadhi ya matatizo yatatokea katika gari lako hasa matatizo ambayo yanagusa mifumo ya muhimu katika gari lako basi mfumo wa kompyuta wa gari lako utaizima baadhi ya mifumo ambayo si ya muhimu ili kulifanya gari lako lisiendelee kupata uharibifu mkubwa zaidi.
Dalili kuu kwa gari yako kuingia katika Limp mode ni gari kuwa na RPM ndogo(siyo zaidi ya 4500) na pia gari kuwa na speed ndogo kwa sababu gearbox huwa inaishia gear namba 3 au gari huwa inastack kwenye gear namba 3 tu hata ukanyage accelerator mpaka mwisho.
Mifumo mingine ambayo inaweza kuzimwa gari inapoingia kwenye Limp mode ni AC, Radio, n.k.
Mifumo hii niliyotaja hapa chini ni baadhi ya mifumo ambayo kama ikiharibika inaweza kupelekea gari lako kuingia kwenye Limp mode,
1. Engine
2. Gearbox
3. Brake system
4. Battery
5. Na mingineyo.
Lengo na kuandika uzi huu ni kuonesha kwamba si kila tatizo kwenye gari ni la kulibeba kama lilivyo. Limp mode hufanya gari yako ioneshe kwamba ina tatizo la gearbox(automatic). Sasa kama hiyo Limp mode imesababishwa na matatizo ambayo si ya gearbox, unaweza kujikuta umebadili gearbox hata 10 na zote zikawa zina tatizo lilelile.
Kufanya Diagnosis kuna umuhimu sana unapopata tatizo lolote lile regardless ni tatizo gani kwenye gari lako.
MWISHO.
Car Diagnosis, Engine service, Repair, Check engine, na mengine mengi.
Karibu Ofisini kwetu Dar es salaam, Sinza Kijiweni.
0688 758 625 au 0621 221 606