NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Nimeshawahi toa mada kama hii siku za nyuma.Kuna jirani yangu mtoto wake binti wa kidato cha pili anapatwa na mapepo kipindi flani flani.Kuna binti ya rafiki yangu naye miaka ya nyuma kama mitano akiwa kidato cha pili alipatwa na hali kama hiii.
Kuna mwingine tena hivyo hiyvo lakini sasa ugonjwa haupo tena ameshakuwa mkubwa na ameolewa huwa nimejiuliza sana ni kwanini hizi hali zinawakuta tu watoto wakike wanaokua?
Nikajiwa na wazo ni HYSTERIA.
Ajabu sasa wanamaombi wa dini hapa ndipo wanapopata dili kuwa ni mapepo hili jambo linani kera mno kuwa kuingiza waumini mkenge hapo nyumbani kila siku ni makelele ya maombi lakini mimi nimeshajua sababu.
Kuna siku aibu ilinitoka kidogo nikamuuliza huyo binti umeshawahi kutembea na mwanamme akaniambia bado kabisa nikaishia hapo nikatingisha kichwa.
Mtu mwingine akiugua malaria ikapanda kichwani nao wanaita mapepo kila kitu kumsingizia shetani iko siku shetani mbele ya mungu atasema jamani vingine sio mimi.
Kuna rafiki yangu mmoja mkristo aliniambia sisi wakristo tumesoma sana kuliko waislam lakini ajabu sasa waislam ni vigumu sana kuingizwa mkenge.
Sisi wakristo ni rahisi mno mfano akaniambia ona babu wa Loliondo alivyoingiza watu mkenge mpaka viongozi wakubwa wa kisiasa.
Kila kitu au tatizo watu hao wa hayo madhehebu kuita ni mapepo inanikera mno kuna mahali namkumbuka kiongozi mmoja wa na nchi yetu alisemaga nanukuu ''AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO'' mwisho wa kunukuu.
Huwa nawaza hivi akitokea muislam akajitangaza kuwa ni nabii watamfanyia nini?