Siyo mikoani, ni mikoa mingine

Joined
Feb 1, 2011
Posts
21
Reaction score
5
Watu wengi hurejea mikoa mingine ya Tanzania kama "mikoani", mathalani, mabasi yaendayo mikoani. Nadhani hii siyo lugha sahihi kwa sababu ina maanisha Dar es salaam ni Taifani. Unaposema mikoani kwani Dar es salaam siyo mkoa? Sema mikoa mingine inaleta maana nzuri zaidi.
 
wanakosea kusema mikoani wakimaanisha mikoa mingine. nakubaliana na wewe. Nadhani dhana ya kuibuka kwa msemo huo ni kutofautisha dar es salaam na huko bara (bahati mbaya dar nayo naiona kama bara tu-kwani wazanzibari ndivyo wanavyoichukulia). Na hata tungesema dar sio bara, basi tanga na mtwara nazo zisingekuwa bara. Na kama dar sio bara je ni wapi?-kisiwani? bila shaka sio. Nadhani "mikoani" wanamaanisha "upcountry" kwa kiingereza. Japo neno mikoani bado sio tafsiri sahihi-kwa maoni yangu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…