Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Imekuwa ni jambo la kawaida sana Kwa shirika la utangazaji la TBC, kukata matangazo mbashara ya Bunge na kutuletea matangazo mengine.
Kwa mfano hivi leo, weshakata mara mbili, matangazo mbashara ya Bunge na kutuletea matangazo mengine, likiwemo hili la sasa hivi la kuteletea semina ya viongozi wa JMAT wa mkoa wa Dar-es- salaam.
Shirika la utangazaji la TBC, linaendeshwa Kwa Kodi zetu wananchi wa nchi hii, Kwa hiyo sisi wananchi ndiyo tunapaswa kuwaeleza hao TBC ni kitu Gani muhimu tunachopenda kukitazama.
Kwa mfano leo, huko Dodoma, ndiyo tunategemea hotuba ya Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, ndiyo anatoa hotuba yake.
Hiyo ni hotuba muhimu sana Kwa Kila mtanzania, kwani hiyo hotuba ndiyo tutakayojua watanzania kama tunaendelea kukamukiwa zaidi Kwa upande wa Kodi.
Hiyo siyo mara ya kwanza, kuondoa matangazo mbashara Kwa TBC na kutuletea matangazo mengine.
Wiki iliyopita, Bunge lilikuwa na hotuba muhimu sana ya wizara ya Maliasili na utalii, lakini badala ya kutuonyesha hotuba hiyo muhimu, TBC walikata matangazo hayo na kutuletea viongozi wakifanya usafi wa mazingira!
Hivi shirika la utangazaji la Taifa TBC, linawezaje kuondoa matangazo hayo muhimu sana Kwa watanzania na kutuletea matangazo hayo mengine, yasiyo na maana kubwa sana kwetu watanzania??
Hata hivyo najua kuwa hata hayo matangazo ya mbashara ya TBC yamerudishwa na serikali hii ya CCM Kwa shingo upande.
Kwa kuwa katika utawala wa awamu ya 5, chini ya Mwendazake Magufuli, alishapiga marufuku Kwa TBC kuonyesha mbashara, matangazo hayo ya Bunge!
Najua kuwa shirika hilo haliko huru katika maamuzi yake, Bali matangazo yake yote ya vipindi, yanaamuliwa na kuratibiwa na hawa watawala wetu wa serikali ya CCM!
Ni vyema shirika hilo likaachwa kuwa huru, badala ya kuingiliwa katika shughuli zake za uendeshaji