SKELETONI MASOZER ndo mala ya kuusikia huu ugonjwa

Joined
Jan 4, 2019
Posts
34
Reaction score
38
Shemeji yangu alikuwa anasumbuliwa na kifua yaani kinauma kiasi kwamba mpaka tukaogopa

Baada ya kwenda hospital akafanyiwa vipimo vya mionzi X-ray ili kuangalia kama kuna shida lakini hapakukuwa na shida yeyote kifuani

Swala ambalo hata mimi sikuweza kuamini kwa maumivu ambayo anayo pata yaani anasema akijinyoosha kwa nguvu au kugeuka kifua huwa kinamuuma na kinakuwa kama kinashtuka na huwa kinatoa sauti mfano wa kidole unapo kigosha

Sasa basi baada ya dactari kuangalia majibu yake ya X-ray akasema kwamba majibu yapo normal isipo kuwa ni MASOZER kwenye mifupa

SKELETONI MASOZER
akapewa dawa ambazo ni Calcivita na gm75 baada ya kutumia dawa hizo lakini hari kama imepungua lakini bado anasumbuliwa na tatizo hilo.

Msaada ambao naomba mnisaidie wana JF ni kutaka kujua hili tatizo kiundani zaidi na huwa linatokana na nini na labda ni dawa gani tena ambayo anaweza akatumia tena.

Najua humu kuna madaktari, msaada wenu kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…