Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Wakala wa ununuzi wa rada ya Tanzania, Shailesh Vithlani Tuesday, September 08, 2009 9:27 AM
Skendo la ununuzi wa rada ya ulinzi ya Tanzania toka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza imechukua sura nyingine nchini Uingereza baada ya BAE kupewa mwezi mmoja kukiri kosa lake na kulipa faini na kesi hiyo iishe au kufikishwa mahakamani. Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza imeipa mwezi mmoja kampuni ya Uingereza ya BAE Systems ambayo iliiuzia Tanzania rada ya kijeshi, kukiri kosa lake au kufikishwa mahakamani
Ununuzi wa rada hiyo uligubikwa na rushwa kubwa na taifa la Tanzania liliuziwa rada hiyo kwa mamilioni ya dola zaidi ya bei halisi ya rada hiyo.
Mbali na rushwa kutumika katika ununuzi wa rada ya Tanzania, BAE pia inatuhumiwa kutumia rushwa katika kukamilisha uuzaji wa ndege moja ya kijeshi kuiuzia nchi ya Afrika Kusini na uuzaji wa ndege nyingine ya kijeshi ambao haukufanikiwa kwa Jamhuri ya Cheki.
Kutokana na skendo hilo SFO imeipa mwezi mmoja BAE kukiri makosa yake ya kutumia rushwa kufanikisha madili yake na kulipa faini ya mamilioni ya paundi na baada ya hapo kurekebisha mienendo yake.
Kama BAE itashindwa kufanya hivyo basi itachukuliwa hatua zaidi za kisheria na itapandishwa kizimbani. Hata hivyo hatua hizo za kisheria zitakuwa dhidi ya kampuni ya BAE na si viongozi wa kampuni hiyo.
Awali SFO iligundua kuwa mkataba wa ununuzi wa rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems uligubikwa na rushwa kubwa.
Ununuzi wa rada hiyo ulifanikishwa na wakala Shailesh Vithlani ambaye aliifanya Tanzania itoe TSh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wa rada hiyo.
Vithlani inasemekana alipewa dola milioni 12 (zaidi ya TSh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha dili hilo na inasemekana aligawana pesa hizo na maafisa saba wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania.
Vithlani alitoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka na alikamatwa mwaka huu nchini Uswizi alikokuwa akijificha.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3028890&&Cat=1