SKONGA: Kipindi 'kinachovua nguo' wanafunzi

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Kila nikipata muda huwa natazama hiki kipindi kinachorushwa katika EATV na host wake akiwa ni Allan Laki. Sina shaka na upeo wa huyu kijana maana maswali yake ya papo kwa hapo kwa wanafunzi yanatoa changamoto ya kutosha. Hofu yangu ni uelewa finyu mno wa wanafunzi ambao huwa wanakutana na maswali ya huyu kijana.

Ni vijana walio kati ya umri wa miaka 14 hadi 22 hivi. Ukiwaona kabla ya maswali ni vijana waliochangamka sana na wenye kujiamini. Confidence zao huanza kupotea pale wanapotupiwa swali la kwanza tu, mathalan tofauti kati ya trekta na katapila. Mwanafunzi anaweweseka. Glacier erosion ni nini. Mwanafunzi anaweweseka wakati amesoma hayo.

Wanafunzi hao ni werevu sana kwenye burudani lakini taaluma zao wako hoi mno. Nini kifanyike? Hili ni suala letu kujadili wote hapa.
 
Wanafunzi hawana muda wa kusoma, mitandao na burudani vimechukua sehemu kubwa ya muda wao, mwanafunzi muda wote yuko online facebook, twitter, whatsapp etc.

Jamii na wazazi nao ndio wa kulaumiwa kwa hili maana hawafuatilii maendeleo ya watoto wao mashuleni na pia kuwahamasisha kusoma kwa bidii.

Tutakuwa na taifa la mamburula miaka michache ijayo maana sio serikali, waalimu, wazazi wala wanafunzi ambao wanaonekana kujali ubora na maendeleo ya elimu.
 
Serikali imekosa mbinu mbadala mwisho wa siku viwango vya ufaulu (wastani) kwa national exams itafikia zero
 
wanafunzi kutokujibu waliyofundishwa kwa maswali ya papo hapo ni kawaida
ndo maana shuleni mtu swali moja anakaa dakika kadhaa au analiacha kwanza anaanza na mepesi

ishu hapa ni general knowledge
wengi ndo aibu hapo
na hili ni aibu ya nchi nzima
wanafunzi na wazazi wao
 
Ukitizama kile kipindi unaweza zaba mtoto wa mtu kituo cha daladala hata hajakukosea.
Unahisi na yeye ni kilaza.



Hahahah....but before you do that remember;

No matter how hot your anger is, it can not cook yams-Nigeria

back to Topic:

Nakumbuka nikiwa sekondari ya Mawezi, Moshi.
Likizo tulikuwa tunakutana na washikaji tuliosoma wote primary halafu wakapangiwa special schools Kibaha, Mzumbe, na Ilboru.
Na wale wa seminary ambapo wanapewa notes na test kila wiki…jamani kuna watu wana raha.
Basi hawa woote tunakutana mtaani tunafundishana weee na kubadilishana knowledge mpaka likizo inaisha…hiyo ndo ilikuwa tuition yetu. Ndiyo si tulisoma wote primary kwahiyo bado ni marafiki.
Na likizo wanakuja nyumbani. Wana interact na sie wa shule za kata tunabadilishana mawazo.
Matokeo form four: Division one (leo hii ningekuwa top ten ya watahiniwa wa CSEE 2012)

A level nikapangiwa Same sekondari. Huko tukawa tunatoroka na kuja kupiga kitabu Moshi sekondari (Old Moshi Sec) wenyewe waliamua kujiita Gold Moshi…dem dayz!
Likizo tena tunakutana na washkaji waliopangiwa Special schools hizo tunabadilishana utirial ma test pepa manini.
Matokeo form six: Division one nzuri tu ya kunipa grades za kusoma Electronic Science & Communication chuo.

Mtazamo wangu:
Ile dhana ya special schools ilisaidia sana kuboresha elimu na kuongeza morali wa wanafunzi kusoma.

  1. Sasa hivi unakuta mwanafunzi anasoma hapo hapo na wale wale aliosoma nao primary hawapati challenges za nje hata kidogo.
  2. Waliofuta special schools hawakukumbuka ule usemi wa, "the world is a book and those who don't travel read only a book" otherwise walidhani kina Nyerere pamoja na umaskini tuliokuwa nao bado walifanya hivyo. Walipeleka hadi watu kusoma nje kwanini???
My call:
Kawambwa & Co. rudisheni special schools kwa maana ile ile ya special schools….
 
He he he, basi wewe ulikuwa msongo

Mie nilikuwa nikiona wanafunzi wa special skul nataka nibadilishane nao vimiminika, angalau nibahatishe mtoto mmoja kipanga.
Ilikuwa raha jamani khah!

 
He he he, basi wewe ulikuwa msongo

Mie nilikuwa nikiona wanafunzi wa special skul nataka nibadilishane nao vimiminika, angalau nibahatishe mtoto mmoja kipanga.
Ilikuwa raha jamani khah!

Teh! Teh! Teh! kwa hiyo ulikuwa unachanganya vimiminika kwa kwenda mbele!! Je ulifanikiwa lengo lako la kupata kipanga?
 
Walikuwa wala hawanioni, maana wale walikuwa wanapenda ma fiziksi na hesabu

Wakati mie nataka tudiskasheni Maiko Jackson, labda sikuwa nawavutia

Walikuwa wanajitenga hao, hadi uwe wa mlengo wao wa kusongoka ndio mnabadilishana vimiminika

Teh! Teh! Teh! kwa hiyo ulikuwa unachanganya vimiminika kwa kwenda mbele!! Je ulifanikiwa lengo lako la kupata kipanga?
 
Walikuwa wala hawanioni, maana wale walikuwa wanapenda ma fiziksi na hesabu

Wakati mie nataka tudiskasheni Maiko Jackson, labda sikuwa nawavutia

Walikuwa wanajitenga hao, hadi uwe wa mlengo wao wa kusongoka ndio mnabadilishana vimiminika

Naelewa usemacho sisi tulikuwa tunawaita "ngwini" wakiona ww mtu wa kujirusha wanakukimbia na kuona unawapotezea muda.
 

Mkuu umegusa kitu kizuri. General knowledge ni tatizo kubwa sana kwenye jamii yetu. Chimbuko lake ndio huko mashuleni na vyuoni. Pawepo na namna ya kipekee kabisa kuhakikisha kuwa mambo ya msingi kitaaluma na kijamii yanaainishwa kisha hayo yaelekezwe kwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na midahalo ya lazima kwa wanafunzi wote mashuleni ili kuwajengea confidence ya kitaaluma na si ya kiburudani kama ilivyo sasa
 
Kipindi kizuri sana big up kwenye ile promo yao napenda yule demu aliyeshangaa na yule dogo anayechana kwenye beat ya big punisher 100%
 

umenikumbusha Mawenzi enzi hizo za kina Bwiru na Mashingia. Unajua mkuu mazingira ya wakati ule yalikuwa conducive. Hakukuwa na mobile phone, fb, twitter, n.k. So aidha wanafunzi tulikuwa wasongo au wahuni wa aina fulani hivi. Leo huwezi kusema hawa dotcom ni wahuni bali waliopotoka na wasiojua future inataka nini. Wazazi wa leo wana kazi ya ziada hasa ukichukulia na hali za walimu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…