Mazao ya kuporomoka kwa elimu chanzo chake ni Nyerere na vibaraka wake, nani alifuta masomo ya History na Geography mashuleni? na nani kayarudisha?
Imebidi nicheke. Unazungumzia hawa Walimu wa toleo la kipindi hiki!! Nina bahati ya kuishi nao ama kukutana nao..Ni msiba! Tena ukiongezea na ugumu wa maisha "product" zitakazotoka baada ya miaka 5 ni balaa mara mbili ya hili tulilonalo.
Labda hujuwi mipango na mikakati ya elimu inavyokwenda sasa hivi. Big Results.
wanafunzi kutokujibu waliyofundishwa kwa maswali ya papo hapo ni kawaida
ndo maana shuleni mtu swali moja anakaa dakika kadhaa au analiacha kwanza anaanza na mepesi
ishu hapa ni general knowledge
wengi ndo aibu hapo
na hili ni aibu ya nchi nzima
wanafunzi na wazazi wao
He he he, basi wewe ulikuwa msongo
Mie nilikuwa nikiona wanafunzi wa special skul nataka nibadilishane nao vimiminika, angalau nibahatishe mtoto mmoja kipanga.
Ilikuwa raha jamani khah!
sijui FaizaFoxy kalishwa limbwata la aina gani na uongozi huu. Dada hasikii haambiwi. Hajui kuwa voda fasta ni zao la awamu hii ya nne? Hajui kuwa katika awamu hii waliofeli ndio wengi kuliko waliofaulu?
mkukuta, mkurabita, ari mpya..., maisha bora kwa kila mtanzania, vision 20-25, kilimo kwanza, vua gamba, na sasa big results now. Hadi muondoke madarakani tutashiba misamiati
Naona umerudi kulaumu na kulalamika (sishangai), niilifikiri utanieleza hizo product nzuri zinazotengenezwa ulizozisema ghafla umerudi kwa Nyerere!!
Kwa mantiki hiyo wanafunzi hawaelewi hayo kwa sababu Nyerere alifuta History na Geography. Hebu tuendelee kwenye mjadala wetu kuhusu "best result" za walimu watakaokuja (achana na wa History na Geography kwa sababu Nyerere "aliharibu").
Nakumbuka tulivyokuwa shule, enzi hizo tupo darasa la tano tulikuwa na Mwalimu wa English, (singa singa) Tukimuita Mr. Singh. Kipindi chake ni lazima aje na gazeti la siku hiyo, siku hizo likiitwa "The Standard" na akifika tu darasani kwenye kipindi chake baada ya Good Morning Sir.,neno lake la kwanza ni "Ok, its now Standard time" na kila siku ni lazima wanafunzi watatu waanze kwa kusoma kwa sauti article moja nzima kila mmoja. Imagine General Knowledge na polishing ya Kiingereza iliyopatikana hapo.
Huenda ukawa sahihi kwamba tulianguka wapi, kosa letu tumeshindwa kutengeneza na hali inazidi kuwa mbaya!
Umeshavimbiwa futari sasa unatuletea mashuzi tu hapa, wewe kwa Nyerere ni sisimizi tu na wala hapatakuwa na FaizaFox day wala Mwinyi day wala Kikwete day, ila ipo Nyerere day na itaendelea kuwepo, na Nyerere ndio symbol ya Tanganyika & Tanzania, huu ndio ukweli ambao hutoweza kuubadili kwa post zako uchwara hapa JF.
Hao waalim unawaona waona leo hii wabpvu ni zao la kuharibiwa elimu na Nyerere na vikaragosi wake. Subiri uone mfumo ulivyobadilishwa na uone miaka ijayo zao litakalotoka.
Kikwete amenza na mashule, kila moto awe na uwezo kusoma Sekondari. Hii haijawahi kutokea kabla yake ni rekodi ya pekee, shule zaidi ya 5000 za sekondato kwa miaka 7 tu. Linganisha na shule chini ya 2000 kwa miaka 45 ya Nyerere, Mwinyi na Mkapa.
Hali kadhali vyuo vikuu, zaidi ya 45 kwa wakati wake tu, linagnisha na vyuo visvyozidi 5 kwa miaka 45 ya hao niliowataja hapo juu.
Bado unalo?
Labda kama unamaanisha Urais wa Miss Tanzania, maana hata Urais wa TFF hana sifa.Kwa misukule tu. Ngoja siku Jerry Slaa akishika Urais uone kama kutakuwa na upuuzi huo.
Mimi na wewe na pengine wengine tulikuwa tunaangalia quality sio quantity. Hata kama watoto wote watapata elimu ya sekondari kama kichwani hamna kitu ni bure kabisa, afadhali hizo resources wangenunulia pembejeo za Kilimo angalau tuondokane na aibu ya njaa!
Hizo fikra zako ni finyu sana. Hakuna nchi duniani inawacha kusomesha watoto wake walio wengi na kusomesha watoto wachache ili ipate quality. Mass education ndio pekee inayoendeleza taifa kwa kuwa na wasomi na si vingine.
Ikiwa mawazo ndio kama hayo yako, tuna kazi, kazi kubwa sana ya kuwaelimisha watu kama wewe.
Kuondoka madarakani, tumpe nani aongoze? Slaa? au DJ? - Wewe kweli umeichoka hii nchi.
Hizo fikra zako ni finyu sana. Hakuna nchi duniani inawacha kusomesha watoto wake walio wengi na kusomesha watoto wachache ili ipate quality. Mass education ndio pekee inayoendeleza taifa kwa kuwa na wasomi na si vingine.
Ikiwa mawazo ndio kama hayo yako, tuna kazi, kazi kubwa sana ya kuwaelimisha watu kama wewe.
Wewe ndiyo umeonyesha ufinyu kabisa wa kufikiri. Sijasema uchache ndiyo "quality", nimesema hapa tunaongelea "quality" na siyo "quantity" unayoipigia debe.
Narudia: "Hata kama watoto wote watapata elimu ya sekondari kama kichwani hamna kitu ni bure kabisa, afadhali hizo resources wangenunulia pembejeo za Kilimo angalau tuondokane na aibu ya njaa!"
Jifunze kusoma bila kuhemkwa. Tulia