Skudu aliumia kwenye mechi dhidi ya Azam, na ilikuwa ndio mechi yake ya pili kucheza baada ya kucheza dhidi ya Kaizer chief. Baada ya kuumia, akawa anauguza jeraha lake huku timu ya Yanga ikiendelea na michezo yake ya ngao ya hisani, ligi na klabu bingwa. Skudu anakuja kurejea kikosini tayari, kocha ana mwanga kuhusu first eleven yake maana wakati Skudu hayupo kocha alikuwa anaendelea na program zake za kupata kikosi chake cha kwanza na pia utimamu wake badala ya kutoka majeraha anajua kocha.
Kwahiyo tegemea kumuona akichezeshwa kulingana na uhitaji wa kocha kwenye mechi husika, sio Skudu tu kuna wachezaji wengi tu wazuri ambao awaonekani uwanjani mfano Sureboy, n k lakini watapangwa kulingana na kocha anataka nini na kaona nini kwa mpinzani. Mfano juzi kocha kamsoma Namungo kaona kuna uhitaji wa Moloko na Mudathir hivyo kawaingiza na wakaleta impact na goli likapatikana. Kwahiyo kila mchezaji atapangwa kulingana na uhitaji wa kocha katika mechi husika.
N B
Mechi ya Yanga dhidi ya Namungo, Skudu alikuwa katika orodha ya wachezaji wa akiba