Jamaa kasaidia kutoa elimu kwa wasiojua, ila kuna wanaojua zaidi wanakuwa wakali!
Alichojaribu kusema ni kwamba hutalipia huduma ya maongezi, utakacholipia ni internet tu. Kwa wale wanaolipa flat rate na wanaotumia internet za kazini au za bure yes, wataongea bila gharama. Cha kukumbusha ni kwamba hakutakuwa na gharama iwapo unayetaka kuongea naye pia ana skype, otherwise kwa kuongea na mtu mwenye simu (also known as skype out) utalazimika kulipia kila dakika. Kuongezea zaidi ni kuwa skype out ina gharama ndogo sana kama unampigia mtu aliyeko Marekani.
Weekend njema...