Elections 2010 Slaa aunguruma Mwembeyanga, LIVE TBC1

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680
Wakuu,

Napenda kuwafahamisha kuwa kesho Dr. Slaa atakuwa viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa LIVE ndani ya TBC1 pia kuanzia saa 10 jioni kwa muda wa masaa 3.

Aidha, baadae atakuwa LIVE katika televisheni ya Agape kuanzia saa 1 jioni.

Mkutano wake leo umejaza watu wengi sana huko Zanzibar tofauti na wengi mnavyoweza kudhani, nitawaletea picha za Zanzibar hali ilivyokuwa.
 
Uuuuuuuwiiiiiiiiiii.......! Sitaki kuamini mapema habari hizo, mbona hiyo itakuwa funiko!
 
Mh yupo Zenji? naomba picha tasavali!
Ila ka ni kweli basi itakuwa funiko bovu
 
Umejuaje wewe ?

Unataka ni-reveal ID yangu mkuu? Taarifa hizi mnaweza kuongea na viongozi wa CHADEMA wakazithibitisha.

Aidha, source kwa sasa sema ni JF!
 
Mkutano wake leo umejaza watu wengi sana huko Zanzibar tofauti na wengi mnavyoweza kudhani, nitawaletea picha za Zanzibar hali ilivyokuwa.

Saa ya ukombozi kwa wazanzibara ni sasa
 
Kuna mtu anaitwa Mtikila jamani mbona kimya?, sijasikia taarifa zake au sharti la kuachiwa lilikuwa afunike domo?
 
hawa tbc usijeshangaa wanachakachua matangazo, nimeipenda hii ya Zanzibar manake najua watu hawakusombwa na magari ili kuonesha kuwa ni wengi kama mafisadi wafanyavyo!
 
Kuna mtu anaitwa Mtikila jamani mbona kimya?, sijasikia taarifa zake au sharti la kuachiwa lilikuwa afunike domo?

Mchungaji si unajua wamemzuia kugombea? Bado anafikiri namna ya kutoka!
 
Mh yupo Zenji? naomba picha tasavali!
Ila ka ni kweli basi itakuwa funiko bovu

Mkuu, bahati mbaya nipo mobile, ningewapa picha za Zanzibar. Mbaya zaidi mpiga picha wa Slaa (Joseph Senga) hakuwepo Zanzibar hivyo media nyingi hazitapata picha.

Am I kidding? Fuatilia posts zangu
 
Mimi sina matumaini na Zanzibar. Slaa arudi kanda ya ziwa. Kuangaika na watu 400000 wakati kagera tu ina zaidi ya 1,000,000 ni kupoteza muda. Hata hizo picha siziamini maana zanzibar ni watu wa kijiwe na wanapenda tu kutafuta maneno. Huwezi kuwategemea. I am a staunch supporter of Slaa (PhD ya Kweli) ila kwa zanzibar aaaaa!
 
Asante sana kwa taarifa hizi basi tujitahidi kusambaza habari ili watu wengi zaidi waweze kumuona. Dr. Slaa ndiyo chaguo letu Watanzania wa kweli na si wale ambao ni wachumia tumbo.
 

Mkuu, kweli ulitaka mgombea uraisi wa Jamhuri asifike Zanzibar?!!!
 
uwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Tanzania yetu
tumpe slaa arudishe heshima
 

Mkuu nakubaliana na wewe kuhusu targets lakini kumbuka kila kura ina-count ni bora tu akafika maeneo yote nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…