Elections 2010 Slaa aunguruma Mwembeyanga, LIVE TBC1

Kesho, mtwara lindi na nachingwea ila TAR 28/10 atakuwa kigamboni baada ya hapo morogoro-iringa-dodoma-mbeya kufunga kampeni.
Jiandae na wataharifu ndugu zako katika maeneo hayo
 
Ndugu wananchi,

naomba niwatangazie kwamba, baada ya kushuhudia nguvu ya watu leo katika Uwanja wa Mwembe Yanga Temeke DSM, sina budi kuagiza kila mtanzania akae mkao wa kupokea serikali mpya wiki ijayo itakayoongozwa na Mheshimiwa Dr. W. P. Slaa

sina zaidi, naomba kila mtu atimize wajibu wake wa kupiga na kulinda kura

wenye picha naomba waweke tafadhali kwa faida ya wale ambao hawakuweza kushuhudia live
 
Mkuu Gurudumu, Picha hakuna jamanai mwafaidi nyie tu. Tupeni picha nasie wambali .
 
Tuna shukuru kwa taarifa,ila ni vizuri tukawa tayari kwa aina yeyote ile ya matokeo,kwani mara kwa mara ufikiliavyo akilini mwako juu ya jambo fulani huwa ni tofauti na jinsi utakavyokwenda na kukikuta live na hapo ndipo watu hufa kwa pressure kwani walichokitegemea kiwe kimekuwa tofauti,Hivyo ndugu zangu ni vyema mkaleta mabadiliko lakini pia mtambuwe kuwa kura ni siri ya mtu moyoni,si waudhuliao mikutano wote ni wapiga kura na kwa kuwa hakuna sensa ya kuzuia wewe wa itikadi hii usije mkutanoni itatuwia vigumu kujua,tunachoshukuru ni kwamba sasa wananchi wameanza kubadilika
TUNAWATAKIA KURA NJEMA TUNASUBIRI MATOKEO KWANI SISI HATUNA NAFASI YA KUPIGA KURA​
 
thanks ni kawaida yake maana ndie mtu watanzania wanaemtaka,kila kona ninapopita jina lake haliishi kutajwa
 
TAARIFA NILIYOPATA SASA HIZI KUTOKA ARUSHA, NIKWAMBA WAKATI Dr SLAA (PhD) ANAHUTUBIA MWEMBEYANGA, WATU WENGI WALIKUWA WAMEJAZANA MADUKANI, SEHEMUMBALI MBALI ZENYE WATU KAMA BAA WAKIMSIKILIZA Mh RAIS MTARAJIWA.
 
Nimeingia MCHANA huu Dar es salaam nikitokea Mwanza , na moja kwa moja nikaenda Mwembe Yanga kumshuhudia Dr Slaa akitema Cheche zake , Kwakweli sikutegemea wana Temeke wangejitokeza kwa makundi Makubwea namna ile. UWANJA WA MWEMBE YANGA UMETAPAKAAWATU HADI POMONI.
KWA HALI NILIYOIONA, MWAKA HUU JK NA WALETA MIZAHA IKULU HAWAPONI.
 
Hiyo Slaa amepiga nchi nzima, habari zimeenea haraka kama moto wa upepo. Dr ametoa hotuba Kama vile ilikuwa ya mwisho wa kampeni.

Alikuwa na uhakika, amepangilia hoja, ushahidi na takwimu. Amegusa makundi mengi ya jamii na maeneo yote ya kijiografia.

Amewasilisha sera na mikakati yake na serikali yake juu ya vyombo vyote vya ulinzi na usalama wa taifa

Amejibu kwa ufasaha kabisa hoja za wapinzani wake. Aliongea Kama mkuu wa nchi ambaye hataki ubabaihaji, uswahili, wala uswahiba.

He was in-charge, he lifted every spirit
 
Hali niliyoiona leo kwa kweli inaonyesha jinsi wananchi walivyoichoka serikali ya sisiem, maana kila siku tunaelezwa madudu yanayofanywa na viongozi wa serikali. Haiingii akilini mashimo manne ya choo kujengwa kwa shilingi milioni 700, labda kama tunadanganywa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…