Elections 2010 Slaa kufyeka wizara, kufuta ukuu wa Mkoa

Mkulima

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2007
Posts
1,236
Reaction score
1,546
Slaa kufyeka wizara, kufuta ukuu wa Mkoa

Imeandikwa na Halima Mlacha; Tarehe: 26th August 2010

MGOMBEA Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa, amesema iwapo atashinda kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, ataunda serikali tatu ikiwamo ya Tanganyika.

Mwanasiasa huyo pia amesema, atapunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu na manaibu wao, na atafuta cheo cha ukuu wa mkoa.

Slaa alisema, cheo cha ukuu wa mkoa hakina maana kwa kuwa viongozi hao wanatoa ushauri tu, wapo wengi na wanatumia magari, nyumba na fedha za serikali kwa kazi hiyo.

Kwa mujibu wa Slaa , Baraza la Mawaziri kwa sasa lina mawaziri 45 ambao ni wengi kulinganisha na idadi ya watanzania.

Alisema, kuna nchi nzima ina wananchi milioni 45, na ametoa mfano kuwa, katika nchi ya Uingereza kuna wananchi milioni 300 na mawaziri 14.

“Sioni kazi ya Manaibu Waziri wanakuwa wengi tu na kutumia magari ya gharama kubwa VX zenye thamani ya Sh milioni 200 bila kazi yoyote ya maana,”

Alisema atapunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri na kufuta baadhi ya vyeo ili kupunguza matumizi makubwa ya Serikali ambayo robo tatu ya bajeti ya nchi hugharamia uendeshaji wa Serikali hali ambayo imekuwa ikididimiza zaidi nchi kiuchumi na ataanza kupunguza utitiri wa ofisi zisizo za lazima.

“Tutaweka mfumo katika Serikali za mitaa na mikoa ambao utawafanya viongozi kuwajibika, tutatumia baraza la madiwani kuwafikia wananchi na kikubwa meya wa madiwani atachaguliwa na wananchi na si kama mfumo wa sasa uliopo,” alisema.

Pia amesema, bado Katiba ya Tanzania imeonekana kuwa kikwazo kikubwa katika utendaji wa viongozi nchini hivyo serikali yake itaibadili Katiba hiyo na kutoa madaraka zaidi kwa wananchi na kufuata mfumo wa uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa zamani wa Zanzibar Abeid Amani Karume.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Habarileo Dar es Salaam jana, alisema kwa sasa hali ya muungano iliyopo ya kuwa na serikali mbili haijawa na ufumbuzi wa kutosha kwa kuwa, serikali moja ya umoja imeizidi ukubwa serikali nyingine hivyo inafaa kuwa na serikali ya Tanganyika ili kuleta usawa.

“Sisi Chadema kama wapinzani hatutaki muungano uvunjike tunataka udumu, lakini hatuoni sababu ya kuwa na serikali mbili za nini? Sasa hapo muungano uko wapi, na hali hii ikiendelea hata kero za muungano haitokuwa rahisi kuzitatua, ndiyo maana sera yetu tutakayokuja nayo itakuwa na mfumo wa serikali tatu,” alisema Dk Slaa.

Alisema katika Serikali hizo tatu mbili zitakuwa kubwa na moja ya umoja itakuwa ni Serikali ndogo ambayo hapo baadaye chama hicho kitakuja na fomula ya namna ya kuisaidia Serikali hiyo katika kushughulikia masuala ya muungano.

Alitoa mfano kuwa, hali ya sasa visiwani Zanzibar ya makubaliano ya Serikali ya Umoja na kubadilishwa kwa Katiba ya visiwani humo.

“Kama Zanzibar ni nchi ya muungano na Katiba yao inatambua Serikali ya Umoja basi na Katiba ya Muungano ingebadilishwa na kuitambua serikali hiyo,”

Alisema, iwapo Chadema kitashinda katika uchaguzi huo, wanafikiri kubadili mfumo wa uongozi uliopo kwa kuanza na Katiba na kuondoa mamlaka makubwa aliyopewa Rais.

Alisifu mfumo wa Mwalimu Julius Nyerere ambao ulishirikisha wananchi na ulijikita zaidi katika kuondoa maadui wakubwa ambao ni ujinga, umasikini na maradhi hali ambayo sasa imebadilika.

Kwa mujibu wa Slaa, ameongezeka adui mmoja, ambaye ni rushwa na akadai kwamba hali hiyo imesababishwa na uongozi mbovu.

Alisema kikubwa ambacho Chadema itazingatia ni mfumo mzuri wa uongozi ambao wamefanyiwa uchunguzi wa kina, mfumo ambao utatumia utajiri wa rasilimali za Tanzania kutunga sera, mipango na mikakati kwa kuisimamia ipasavyo ili kukuza uchum na kuiletea maendeleo nchi hiyo.

“Katika uongozi wa Mwalimu Nyerere alijitihadi kutumia mfumo wake wa uongozi na kupeleka timu ya watanzania nje kupatiwa utaalamu wa kutengeneza magari na hadi sasa yapo magari yaliyotengenezwa Tanzania tena kupitia rasilimali yetu ya chuma, ila kwa sasa inasikitisha kuona mfumo wa Mwalimu kama vile Azimio la Arusha umefutwa,” alisema.

Akizungumzia suala la elimu ya mgombea wake mwenza Said Mzee Said, ambaye ana elimu ya shule ya msingi, alisema haoni kama hilo ni tatizo.

Alisema, hata Katiba ya nchi inazungumzia wazi sifa za kiongozi kuwa ni umri, utaifa, awe na akili timamu na ajue Kiswahili au kingereza sifa ambazo mgombea huyo anazo.

“Kwangu mimi sioni kama elimu ni kigezo kikubwa kwa kiongozi, wapo viongozi wengi tu hawakuwa na elimu kubwa na wameongoza vizuri kama vile Simba wa Vita (Rashid Kawawa) ambaye alikuwa Waziri Mkuu pamoja na Sokoine na wote hao wameacha historia nzuri juu ya uongozi wao,” alisema.

Alisema iwapo katika uchaguzi huo atashindwa kwa haki atabaki kuwa mtanzania wa kawaida na kwamba, Januari mwakani atazunguka nchi nzima kuiandaa Chadema kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Lakini pia bado naweza kuwania nafasi ya Uspika kwani kwa mujibu wa Katiba Spika si lazima awe Mbunge,”
 
Hivi Dr. Slaa na CHADEMA mmecheck usahihi wa mifano mnayotumia?

Argument ya ukubwa wa serikali ni nzuri sana lakini mifano inayotumika haiko sahihi. Mara mbili nimesoma Dr. Slaa akitoa mfano wa UK kuwa na baraza la mawaziri dogo na kutaja namba ya 14 lakini ukweli unapingana na hayo madai yake.

Uingereza ina mawaziri wapatao 100 kama unajumlisha na mawaziri wadogo na sio 14 kama anavyodai Dr. Slaa. Pia Uingereza ina watu karibu 60M na sio 300M anavyodai Dr. Slaa. Hata ukichukulia mawaziri kamili basi wako karibu 30, sijui hiyo namba ya 14 kaitoa wapi?

Mbali na serikali ya UK yenye hao mawaziri karibu 100 pia kuna serikali ya Scotland, Wales na Northern Ireland na kwa ujumla kufanya nchi iwe na baraza kubwa sana la mawaziri.
Baraza la mawaziri la UK linaweza kupatikana hapa:

BBC News - Cameron's government: A guide to who's who
 
Ungelikuwa una AKILI walau kidogo, ungelifahamu kuwa kuna makosa yamefanyika na hapa alikuwa anaongelea USA yenye watu milioni 300 na mawaziri 14 na Hilary Clinton akiwa kama Waziri Mkuu yaani Secretaryof State. Ila kwa sababu Waandishi walikosea na wewe ni MVIVU wa kufikiri, ukaamini ni UK na makosa yamefanywa na Dr. Slaa. Tatizo ni jinga fulani liliandika UK badala ya USA.

Inanikumbusha ile Mtu yuko Marekani anaulizwa ataje nchi inayoanzia jina na U na anasema Utah au sijui. Akiambiwa vipi kuhusu USA, anafungukia kifaa cha kulia. Ovyooooo kabisa Wafuasi wa Mziray.

Ukweli ni kuwa balaza la Mawaziri la Tanzani ni kubwa Mno. na mbaya zaidi ukubwa unapinga na na utendaji kazi wao mbovu.
Ukweli ni kuwa mfumo uliopo wa uongozi wa serikali una kasoro. Waziri anachaguliwa na rais, Katibu mkuu wa wizara anachaguliwa na rais, wakurugenzi wa wizara wanachaguliwa na rais. Kwa hiyo nafasi tatu za juu za wizarani ni political appointment.Haya wakuu wa mikoa DC na NEC inaongeza majimbo kwa vigezo visivyo na tija.
Ukweli ni Kuwa Muungano ni kero na CCM hawakubali ukweli suluisho ni ama serikali moja au tatu au muungano uvunjwe
Dr Slaa kasema machache, Lipumba akichokonoa kidogo kwenye uchumi bado watu hawakubali kuwa CCM ni Kikwazo cha wananch wote.
 
Ungelikuwa una AKILI walau kidogo, ungelifahamu kuwa kuna makosa yamefanyika na hapa alikuwa anaongelea USA yenye watu milioni 300 na mawaziri 14 na Hilary Clinton akiwa kama Waziri Mkuu yaani Secretaryof State. Ila kwa sababu Waandishi walikosea na wewe ni MVIVU wa kufikiri, ukaamini ni UK na makosa yamefanywa na Dr. Slaa. Tatizo ni jinga fulani liliandika UK badala ya USA.

Inanikumbusha ile Mtu yuko Marekani anaulizwa ataje nchi inayoanzia jina na U na anasema Utah au sijui. Akiambiwa vipi kuhusu USA, anafungukia kifaa cha kulia. Ovyooooo kabisa Wafuasi wa Mziray.

Hata USA haina mawaziri 14; wapo zaidi ya 20 na ukijumlisha na manaibu namba inaenda mbali sana.

Kuwa na baraza dogo la mawaziri ni jambo jema kwa nchi maskini kama ya kwetu ila hii mifano anayoitumia bila hata kufanya uchunguzi wa kutosha ndio naona inamwangusha.

Hata hilo la gari VX kununuliwa milioni 200 nalo huenda ni figure isiyo sahihi.

Kuna haja ya kuanzisha facts check kuwakamata wanasiasa wanaozidisha chumvi kwenye mboga.
 
Acha uongo wewe,

hebu wataje mawaziri 20 wa marekani (kama unawajua). mijitu mingine kwa kupenda ligi bana
 
Niko skeptical sana na huyu Slaa, ati anasema atapunguza gharama za serikali kwa kufanya muundo wa serikali 3?? Hivi sasa zipo mbili unasema zinatumia gharama kubwa sasa arithmetically zikiwa 3 ndio zitapungua?? kupunguza ukubwa wa serikali sio ishu, ishu ni kuwa na serikali yenye idadi sahihi ya watumishi na wanaowajibika na kukidhi matarajio ya watz.

Nways, all in all, sioni matumaini ktk maelezo yake maana mi nilitegemea angezungumzia mambo uchumi zaidi, kwamba ana mikakati gani ambayo sasa haipo. Nimeongea mara nyingi kwamba seruikali lazima iwe na pesa na mipango ya kuwa na pesa, bila hivo serikali haina sababu ya kuwepo maana ni mzigo. Hatuhitaji tena kuwa na serikali ambayo ni baba-suruali...haina pesa, kila siku kuombaombaombaomba.. Angepaswa kutufafanua what have been thought through kwene mambo ya madini, fossil fuels, kilimo, biashara na viwanda, na ultimately jinsi ya kuivuta jamii kutoka kwenye lindi la umaskini wa kutupa.
 
Ungelikuwa una AKILI walau kidogo, ungelifahamu kuwa kuna makosa yamefanyika na hapa alikuwa anaongelea USA yenye watu milioni 300 na mawaziri 14 na Hilary Clinton akiwa kama Waziri Mkuu yaani Secretaryof State. Ila kwa sababu Waandishi walikosea na wewe ni MVIVU wa kufikiri, ukaamini ni UK na makosa yamefanywa na Dr. Slaa. Tatizo ni jinga fulani liliandika UK badala ya USA.

Inanikumbusha ile Mtu yuko Marekani anaulizwa ataje nchi inayoanzia jina na U na anasema Utah au sijui. Akiambiwa vipi kuhusu USA, anafungukia kifaa cha kulia. Ovyooooo kabisa Wafuasi wa Mziray.

Original source inasema UK. Msichanganye mambo.
 
Niko skeptical sana na huyu Slaa, ati anasema atapunguza gharama za serikali kwa kufanya muundo wa serikali 3?? Hivi sasa zipo mbili unasema zinatumia gharama kubwa sasa arithmetically zikiwa 3 ndio zitapungua?? kupunguza ukubwa wa serikali sio ishu, ishu ni kuwa na serikali yenye idadi sahihi ya watumishi na wanaowajibika na kukidhi matarajio ya watz.

Nways, all in all, sioni matumaini ktk maelezo yake maana mi nilitegemea angezungumzia mambo uchumi zaidi, kwamba ana mikakati gani ambayo sasa haipo. Nimeongea mara nyingi kwamba seruikali lazima iwe na pesa na mipango ya kuwa na pesa, bila hivo serikali haina sababu ya kuwepo maana ni mzigo.

Unaweza kuanzisha serikali tatu zenye watendaji wachache zaidi kuliko wale wa serikali mbili.

kuhusu kuongea mambo ya uchumi, hivi kupunguza matumizi ya serikali sio uchumi? au uchumi unamaanisha nini kwako?
 
Una hakika kuwa original source (habari leo iko sahihi)? original source ndiyo imepelekea watu kuanzisha uwezekano mwingine kwa sababu haiaminiki.
Leteni basi source yenu mnayoiamini..sioni kwanini maelezo yakuwa marefu.
 
Hivi Dr. Slaa na CHADEMA mmecheck usahihi wa mifano mnayotumia?

Argument ya ukubwa wa serikali ni nzuri sana lakini mifano inayotumika haiko sahihi. Mara mbili nimesoma Dr. Slaa akitoa mfano wa UK kuwa na baraza la mawaziri dogo na kutaja namba ya 14 lakini ukweli unapingana na hayo madai yake.

Uingereza ina mawaziri wapatao 100 kama unajumlisha na mawaziri wadogo na sio 14 kama anavyodai Dr. Slaa. Pia Uingereza ina watu karibu 60M na sio 300M anavyodai Dr. Slaa. Hata ukichukulia mawaziri kamili basi wako karibu 30, sijui hiyo namba ya 14 kaitoa wapi?

Mbali na serikali ya UK yenye hao mawaziri karibu 100 pia kuna serikali ya Scotland, Wales na Northern Ireland na kwa ujumla kufanya nchi iwe na baraza kubwa sana la mawaziri.
Baraza la mawaziri la UK linaweza kupatikana hapa:

BBC News - Cameron's government: A guide to who's who
hata hivyo amesema ukweli japo mfano uliotolewa ni wa UK badala ya US kama nilivyonukuu toka facebook ya huyo aliyemhoji hapo Daily news..na ni kweli kwamba hata hapa UK baraza ni dogo kuliko TZ we kinachokuchanganya ni ukubwa wa watendaji kwenye hizo wizara(yaani ministers of state na junior ministers)ambao hata hapa kwetu tungeweza kuwa nao wengi tu kadri ya mahitaji ya wizara,kwa mfano badala ya kuwa na wakuu wa mikoa na mawaziri kibao tungeweza kuwa na mfano waziri wa elimu na manaibu kama watano wanne wasimamie kila kanda na mmoja labda science and technology.hivyohivyo na wizara zingine muhimu na hao wangetokana na makundi ya kitaalam na sio wanasiasa..jeshi la polisi lingeimarishwa na kusogezwa zaidi kwa wananchi, kuwe na magavana wa kanda na wachaguliwe na wananchi wa kanda hizo kazi zao ni pamoja na kuhahakisha hao manaibu waziri wana-deliver according to the budget na vilevile hao magavana wasimamie local gorvnment akisaidiwa na madiwani wa kanda hizo ili kukagua utendaji wa hao maofisa wa kanda na bajeti ya serikali itengwe sawa na ipelekwe kwenye kanda hizo badala ya vote zote za hela kubaki Dar na matokeo yake ndo hayo majumba ya mbezi na masaki!!!hapo hakutakuwa na upendeleo wa kikanda hata kama sehemu fulani ya nchi anatoka rais au waziri mkuu kwani haitawezekana budget ya kanda A kwenda kujenga barabara kanda B tupende tusipende lazima tuanze kupunguza siasa kuongoza frontline services.
 
Hivi Dr. Slaa na CHADEMA mmecheck usahihi wa mifano mnayotumia?

Argument ya ukubwa wa serikali ni nzuri sana lakini mifano inayotumika haiko sahihi. Mara mbili nimesoma Dr. Slaa akitoa mfano wa UK kuwa na baraza la mawaziri dogo na kutaja namba ya 14 lakini ukweli unapingana na hayo madai yake.

Uingereza ina mawaziri wapatao 100 kama unajumlisha na mawaziri wadogo na sio 14 kama anavyodai Dr. Slaa. Pia Uingereza ina watu karibu 60M na sio 300M anavyodai Dr. Slaa. Hata ukichukulia mawaziri kamili basi wako karibu 30, sijui hiyo namba ya 14 kaitoa wapi?

Mbali na serikali ya UK yenye hao mawaziri karibu 100 pia kuna serikali ya Scotland, Wales na Northern Ireland na kwa ujumla kufanya nchi iwe na baraza kubwa sana la mawaziri.
Baraza la mawaziri la UK linaweza kupatikana hapa:

BBC News - Cameron's government: A guide to who's who

Hivi ndivyo ilivyoandikwa wakati akihojiwa na Daily News, soma Daily news ya Friday August 27, 2010

He criticised President Jakaya Kikwete for maintaining a huge cabinet. He said the United States with a population of over 300 million has only 14 ministers, while Britain has 20.
 
Unaweza kuanzisha serikali tatu zenye watendaji wachache zaidi kuliko wale wa serikali mbili.
Hayo ni maneno matupu, 2 tangu lini ikawa kubwa kwa tatu? weka basi huo mchanganuo wa serikali ya Dr. Slaa tuongee vitu tangible.
kuhusu kuongea mambo ya uchumi, hivi kupunguza matumizi ya serikali sio uchumi? au uchumi unamaanisha nini kwako?
Sioni kama hizi danadana za ukubwa wa serikali zitakuwa na impact yeyote ya kiuchumi. Rejea upya post yangu uone vitu ninavyodhani ni vya msingi kwenye uchumi.
 
Ungelikuwa una AKILI walau kidogo, ungelifahamu kuwa kuna makosa yamefanyika na hapa alikuwa anaongelea USA yenye watu milioni 300 na mawaziri 14 na Hilary Clinton akiwa kama Waziri Mkuu yaani Secretaryof State. Ila kwa sababu Waandishi walikosea na wewe ni MVIVU wa kufikiri, ukaamini ni UK na makosa yamefanywa na Dr. Slaa. Tatizo ni jinga fulani liliandika UK badala ya USA.

Inanikumbusha ile Mtu yuko Marekani anaulizwa ataje nchi inayoanzia jina na U na anasema Utah au sijui. Akiambiwa vipi kuhusu USA, anafungukia kifaa cha kulia. Ovyooooo kabisa Wafuasi wa Mziray.

Kweli Sikonge,
Maana kwenye mahojiano yake niliyoyasoma kwenye Raia Mwema alisema UK inakaribia watu milioni 70. Hivyo haiwezekani kwenye Raia Mwema akasema inakaribia milioni 70 (maana anajua kuwa haijafika) halafu kwenye daily news/habari leo aseme milioni 300. Kama mtu ametamka kimakosa, waandishi wa habari wawe pia wanafanya check up ya statement za watu wanaohoji. Kuleta statement ambayo imetamkwa kimakosa kwa lengo la kumchafulia mtu, inachafua gazeti zaidi na kufanya lisiaminike. Wasisahau kuwa baadhi ya habari zao hutumika kwenye academic circles.
 
Naona ujumbe wa Dr Slaa apo ni kuwa kanchi ketu kamaskini tena kwa kujitakia basi tubane matumizi ili tukiendeleza resources zetu ndo tuanze huo ufujaji wa fedha za watoka jasho wa TZ.
 
Hata USA haina mawaziri 14; wapo zaidi ya 20 na ukijumlisha na manaibu namba inaenda mbali sana.

Kuwa na baraza dogo la mawaziri ni jambo jema kwa nchi maskini kama ya kwetu ila hii mifano anayoitumia bila hata kufanya uchunguzi wa kutosha ndio naona inamwangusha.

Hata hilo la gari VX kununuliwa milioni 200 nalo huenda ni figure isiyo sahihi.

Kuna haja ya kuanzisha facts check kuwakamata wanasiasa wanaozidisha chumvi kwenye mboga.
tofautisha waziri na naibu waziri, mwenyekiti na makamu mwenyekiti. raisi na makamu wa raisi. sasa Dr slaa amesema mawaziri hajazungumzia manaibu inaitaji logic ndogo kuelewa
 
Apunguze kasi. Atumie watu wanaojua wanachokifanya kabla ya kutoa hizi hotuba. Makosa kama population ya uingereza hayastahili kwa mtu ambaye anataka watu waamini kuwa anastahili kushika uskani wa nchi hii.

Hivi anaamini kweli kuwa yeye atachukua urais na chama chake kitazoea majority ya vitu kwenye bunge? Very likely hata akishinda urais itambidi apanbane na hostile bunge. Sitashangaa kuona vyama vingine vikiungana na CCM ili mradi kuinyima majority Chadema!

Amandla.........
 
Sitashangaa kuona vyama vingine vikiungana na CCM ili mradi kuinyima majority Chadema!

Njaa na uroho wa madaraka ndivyo vinavyozuia mabadiliko siku zote.
 
Back
Top Bottom