Elections 2010 Slaa kuzuiwa kugombea urais?

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,887
Reaction score
7,673
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuwa Dokta Slaa ameanza kampeni kabla ya Muda.
Ni kinyume cha sheria maana kila anapopita anaeleza atakayowafanyia Watanzania pindi akichaguliwa kuwa Rais. Kwakuwa lengo la Mwanasiasa huyo ni kuomba ridhaa ya kudhaminiwa hakupaswa kuanza kutoa ahadi za yale atakayoyafanya maana kwa kufanya hivyo ni kuanza kampeni.

Je, Rais Mtarajiwa hawezi kuwekewa pingamizi hasa ukitilia maanani Mavuvuzela (Mtikila, yule wa TLP, NCCR na TPP maendeleo) nao ni wagombea wanaoweza kutumika kirahisi na WEVI hawa wa Chama Cha Mapinduzi kutimiza azma hiyo? Si kwamba mavuvuzela hayo yanaweza kutangulia kumwekea pingamizi Rais Slaa/ Samahani, namaanisha Rais Mtarajiwa Dokta Slaa?
 
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuwa Dokta Slaa ameanza kampeni kabla ya Muda.
Ni kinyume cha sheria maana kila anapopita anaeleza atakayowafanyia Watanzania pindi akichaguliwa kuwa Rais. Kwakuwa lengo la Mwanasiasa huyo ni kuomba ridhaa ya kudhaminiwa hakupaswa kuanza kutoa ahadi za yale atakayoyafanya maana kwa kufanya hivyo ni kuanza kampeni.
?

Kwanza wana JF, hii hoja ilitolewa na chadema[kama sijakosea mnyika] kuwa CCM mkutano mkuu, na ule wa kuwatambulisha wagombea Dodoma Zanzibar etc haikuwa kampeni? Tume ya uchaguzi haikuwa na jibu, msajili hakuwa na jibu, wala Werema hawakuwa na jibu. Kwavile Chadema wamewasha moto basi Tume, msajili na Mwanasheria mkuu inaonekana wameshatumwa. Kwahiyo kabla ya kuuliza chadema wajibu hoja za mikutano ya utambulisho ya CCM tena akina JK na Shein wakitumia resource za serikali kama magari,ndege na ulinzi hata kabla kampeni.
Lakini pia tukumbuke Dr Slaa hajachukua fomu kwahiyo sijui kwanini vyombo vya dola viwe na wasi wasi. Hana kitu kinacho m-bind as presidential candidate.
Huko nyuma nimewahi kuandika kuwa Uwanja wa mapambano sio ''level field'' haya ndiyo niliyokuwa nayaongelea. Subirini PCCB wakianza kazi watakamata kila jimbo isipokuwa Monduli na Igunga, Nzega,Lushoto,Vunjo na Bagamoyo.
 
Wakifanya hivyo tuuu yatawakuta yale ya ZITO KABWE. Watakuwa wamemfanyia kampeni ya bure na kukuza jina lake saba mara sabini . Let it come!!!
 
Naona mwanasheria mkuu wa serikali naye kaamua kukomalia hilo. Kwa kuwa tayari amekuwa threat lazima yataibuka mengi. Mbona siku zote walikuwa hawasemi, badala yake wamesubiri hadi siku ya mwisho ya kutafuta wadhamini ndo waseme hayo? Ila Kiravu anaonekana kutetea sasa sijui tusubiri. CCM hawakosi visa.

Gazeti la habari leo limeandika hivi:
MCHAKATO wa Chadema kupata wadhamini kwa ajili ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano, umeelezwa kukiuka utaratibu na kuonekana kuanza kampeni kabla ya wakati.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini, wamesema wanashindwa kutofautisha mchakato wa udhamini na kampeni za chama kutokana na jinsi mgombea huyo, Dk. Wilbrod Slaa na viongozi wenzake, wanavyozunguka nchini na kufanya mikutano ya hadhara.

"Tunashindwa kuelewa kinachofanyika hasa ni nini kati ya kutafuta wadhamini na kufanya kampeni, mikutano mingi ya hadhara huku na huko badala ya kutafuta wadhamini matawini," alisema mchambuzi wa masuala ya siasa ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

Dk. Slaa amezunguka sehemu mbalimbali nchini akitumia helikopta kutafuta wadhamini huku akifanya mikutano ya hadhara ambayo amekuwa akiihutubia sambamba na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mwanasheria Mabere Marando na viongozi wengine.

Akizungumzia mchakato huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kuwazuia Chadema kufanya wanavyofanya sasa kwa kuwa hawajachukua fomu ya kugombea urais.

"Hatuwezi kuwabana hawa kwa sababu taarifa tuliyonayo ni kwamba wanatafuta wadhamini na si kampeni, kwa sababu kampeni hazijaanza," alisema Kiravu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alisema naye anashangaa kuona Chadema inafanya kana kwamba kampeni zimeanza.

"Nami nashangaa na nimekuwa nikimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuhusu hili lakini sijampata … naona sasa nchi ina kambare wengi, kwa sababu kuna tabia ya kutoheshimu sheria za nchi," alisema Werema.

Aliongeza kuwa hata ustaarabu wa kawaida tu nao haupo kwani Chadema walipaswa kujua kuwa wanachokifanya sicho, kwa sababu udhamini hautafutwi kwa kufanya mikutano ya hadhara na kutoa ahadi na kuomba kura.

Alimshangaa Marando ambaye alisema ni mwanasheria aliyebobea ambaye asingetarajiwa kusema anayoyasema sasa katika mikutano ya Chadema, ikiwamo kuahidi kutoa siri zilizo katika nyaraka za kesi zilizoko mahakamani.

Pia alisema kwa mtu ambaye anakiri alikuwa Idara ya Usalama wa Taifa, asingetarajia kumsikia akitamba kuwa ana mambo mengi ya siri anayoyajua na muda ukifika atayaweka hadharani.

"Ni hayo hayo ninayoyasema kwamba sasa kambare wamekuwa wengi nchini … lakini namsubiri ayaseme tu hayo jukwaani, kwa sababu Sheria ya Usalama wa Taifa iko wazi kabisa," alisema Werema.

Katika hotuba nyingi za Dk. Slaa, amekuwa akibeza utawala wa Rais Jakaya Kikwete akisema umeshindwa kuwasaidia wananchi na pia amekuwa akiomba kura za wafanyakazi akisema Kikwete alizikataa hivyo apewe yeye.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, kampeni zinatarajiwa kuanza rasmi Agosti 20 mwaka huu.
Source: Habari leo
 
Hamkumbuki kipindi kile Mgombea wa CUF alimwekea pingamizi Mgombea wa CHADEMA Mbeya Vijijini? Hata sasa hawa waliopo na watakaoendelea kuwepo wanaweza kufanya hivyohivyo. Na kwakuwa vyombo vyetu vya kusimamia na kuendesha uchaguzi vipo CORRUPT, sitashangaa endapo Slaa atazuiwa kugombea Urais
 
Duuu hoja hapo kuwa hajachukua form...kugombea urais mnamnyoshea kidole mnachemka....hapo amepata ridhaa chama chake tu...
 
Werema atueleze kwanza kwamba ni sheria gani ambayo Chadema /Dr Slaa imevunja? Kwani mtanzania yoyote au chama chochote kama kikiomba kibali (I dunno for what hizi ni draconian laws pia) za kufanya mkutano wa hadhara na kupewa kibali na kuongea .. hii si inalindwa chini ya freedom of expression? Kama Dr Slaa angeongea aliyoyaongea mwaka mmoja uliopita na kusema anatakak kugombea angenyimwa nafasi hiyo? Maana hajachukua bado fomu!
Kwa kweli hapo CCM/Wanamtandao wamechemka.. na wasingemruhusu Werema atoe statement yoyote maana anawaharibia sana... Statement ya Werema inazidi kuongeza nguvu ya Chadema na kufanya CCM kuonekana inaogopa mapema hata kabla kampeni haijaanza....
 
Huyu werema ni mwanachama wa CCM, au ni mwanasheria wa serikali? Au anaogopa Dr Slaa akipata urais kitumbua kitaota mchanga?
 
Werema ni mwanachama wa CCM kama ilivyo kwa Saidi Mwema, Mwamunyange na wengine.
 
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuwa Dokta Slaa ameanza kampeni kabla ya Muda.
Mzittokabwela

Taarifa yako ni ya uongo umeitoa wapi, NEC hawakusema hivyo, hata hivyo umejuaje Dr.Slaa atachaguliwa kugombea wakati hata fomu za NEC hajachukua.

Mzittokabwela NEC (Kiravu) imesema hivi.....
Akizungumzia mchakato huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kuwazuia Chadema kufanya wanavyofanya sasa kwa kuwa hawajachukua fomu ya kugombea urais.

"Hatuwezi kuwabana hawa kwa sababu taarifa tuliyonayo ni kwamba wanatafuta wadhamini na si kampeni, kwa sababu kampeni hazijaanza," alisema Kiravu.

Nashanga wewe unatuletea habari tofauti kabisa plainly opposite na NEC walivyosema, usije ikawa unachanganya Halmashauri kuu ya CCM nayo huitwa NEC-CCM.

CCM walipokuwa wanawatambulisha wagombea wao ikwepo pale pale jangwani walidhani wengine hawawezi.....mkuki kwa nguruwe..... ukiona hivyo ni kiwewe kimewaingia.
 
woga, woga,woga mkuu umetanda ccm! Mwaka huu mtajjibbebba!!!!
 
Nadhani amechanganya kati ya Werema na Kiravu. Ukweli sio NEC ila ipo kauli ya Serikali juu ya Slaa kuanza kampeni kabla ya Muda. Besides, hiyo kauli ya NEC uliyoiquote ni ya lini?
 
Mzittokabwela

Taarifa yako ni ya uongo umeitoa wapi, NEC hawakusema hivyo, hata hivyo umejuaje Dr.Slaa atachaguliwa kugombea wakati hata fomu za NEC hajachukua.

Mzittokabwela NEC (Kiravu) imesema hivi.....

Nashanga wewe unatuletea habari tofauti kabisa plainly opposite na NEC walivyosema, usije ikawa unachanganya Halmashauri kuu ya CCM nayo huitwa NEC-CCM.

CCM walipokuwa wanawatambulisha wagombea wao ikwepo pale pale jangwani walidhani wengine hawawezi.....mkuki kwa nguruwe..... ukiona hivyo ni kiwewe kimewaingia.

Gazeti la Habari LeoMCHAKATO wa Chadema kupata wadhamini kwa ajili ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano, umeelezwa kukiuka utaratibu na kuonekana kuanza kampeni kabla ya wakati.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini, wamesema wanashindwa kutofautisha mchakato wa udhamini na kampeni za chama kutokana na jinsi mgombea huyo, Dk. Wilbrod Slaa na viongozi wenzake, wanavyozunguka nchini na kufanya mikutano ya hadhara.

"Tunashindwa kuelewa kinachofanyika hasa ni nini kati ya kutafuta wadhamini na kufanya kampeni, mikutano mingi ya hadhara huku na huko badala ya kutafuta wadhamini matawini," alisema mchambuzi wa masuala ya siasa ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

Dk. Slaa amezunguka sehemu mbalimbali nchini akitumia helikopta kutafuta wadhamini huku akifanya mikutano ya hadhara ambayo amekuwa akiihutubia sambamba na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mwanasheria Mabere Marando na viongozi wengine.

Akizungumzia mchakato huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kuwazuia Chadema kufanya wanavyofanya sasa kwa kuwa hawajachukua fomu ya kugombea urais.

"Hatuwezi kuwabana hawa kwa sababu taarifa tuliyonayo ni kwamba wanatafuta wadhamini na si kampeni, kwa sababu kampeni hazijaanza," alisema Kiravu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alisema naye anashangaa kuona Chadema inafanya kana kwamba kampeni zimeanza.

"Nami nashangaa na nimekuwa nikimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuhusu hili lakini sijampata … naona sasa nchi ina kambare wengi, kwa sababu kuna tabia ya kutoheshimu sheria za nchi," alisema Werema.

Aliongeza kuwa hata ustaarabu wa kawaida tu nao haupo kwani Chadema walipaswa kujua kuwa wanachokifanya sicho, kwa sababu udhamini hautafutwi kwa kufanya mikutano ya hadhara na kutoa ahadi na kuomba kura.

Alimshangaa Marando ambaye alisema ni mwanasheria aliyebobea ambaye asingetarajiwa kusema anayoyasema sasa katika mikutano ya Chadema, ikiwamo kuahidi kutoa siri zilizo katika nyaraka za kesi zilizoko mahakamani.

Pia alisema kwa mtu ambaye anakiri alikuwa Idara ya Usalama wa Taifa, asingetarajia kumsikia akitamba kuwa ana mambo mengi ya siri anayoyajua na muda ukifika atayaweka hadharani.

"Ni hayo hayo ninayoyasema kwamba sasa kambare wamekuwa wengi nchini … lakini namsubiri ayaseme tu hayo jukwaani, kwa sababu Sheria ya Usalama wa Taifa iko wazi kabisa," alisema Werema.

Katika hotuba nyingi za Dk. Slaa, amekuwa akibeza utawala wa Rais Jakaya Kikwete akisema umeshindwa kuwasaidia wananchi na pia amekuwa akiomba kura za wafanyakazi akisema Kikwete alizikataa hivyo apewe yeye.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, kampeni zinatarajiwa kuanza rasmi Agosti 20 mwaka huu.
Mzitto amekosea tu padogo, hajadanganya!
 
Anachofanya Dr Slaa mimi naweza ita ni extension ya Operation Sangara, yaani Dr na wenzie wanachofanya ni kuwafungua macho watanzania ili waweze kufanya maamuzi sahihi mwezi October! si mnajua ukirusha jiwe gizani ukisikia aaiii ujuwe limempata! hahah CCM jiwe limewapata sasa wanatafuta pa kudekea, CCM is like a spoilt child, kila akigusa basi ni mbio kwa baba kulalamika! Mambo haya walianza wenyewe CCM, what chadema is doing is just giving CCM the test of its own medicine!
 
zito wa chadema, kashakuwa mpinzani wa slaa. duh bora zito atimke tu
ni kitambo sasa tangu nimejiunga na hii forum kama memba, sijawahi ona mwanajamvi kilaza kama MS, yaaaani haelewi hata kusoma na kutafsiri mambo mepesi kama haya, kweli JF inapita kwenye wakati mgumu kama great thinkers wenyewe ndio kama huyu MS, kifupi huyu ndio mwanajamvi mwenzetu mwenye matatizo zaidi kifikra.
 
Ni muumini mzuri wa siasa majitaka
 
Back
Top Bottom