Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Bila shaka Dr Slaa anamaananisha kura ya urais. Kwani akishinda hiyo si ndo amechukuwa nchi? Katika nchi za Kiafrika power iko Ikulu -- na siyo Bungeni. Mutharika alitawala Malawi miaka mitano with a hostile Parliament na kuleta maendeleo makubwa. Last year wananchi walimpa kura nyingi mno na upinzani ukatokomea kunakostahili.
Tusisahau pia Mrema mwaka 1995 alikuwa tishio kubwa sana kushinda kura ya urais hadi CCM wakaingia hofu, na kama siyo Nyerere kuingia kuwakampenia na pia kutumia faulo kubwa siku ya uchaguzi kupitia Tume yao ya uchaguzi katika mkoa wa Dsm ambako Mrema alikuwa na ngome kubwa CCM, huenda ingeaanguka.
Kumbuka pia wakati ule kulikuwapo ulazima wa mgombea wa urais kupata asilimia 50+ ili kushinda ama sivyo kuna re-run kati ya top two.
lakini kutokana na hofu hiyo kutoka kwa Mrema, wamebadilisha hiyo na kwamba Rais sasa anaweza kuchaguliwa hata kwa asilimia 30 tu ya kura, hata iwapo jumla ya kura za wapinzani wake watamzidi kwa kura! Hivyo ndivyo CCM inavyojihakikishia ushindi, na siyo kupendwa na watu.
Tatu, ajabu inaweza kutokea kwani wewe unaweza kupanga mambo yako, lakini Mwenyezi Mungu pia an mipango yake. Chochote kinaweza kutokea hapa katikati katika medani ya kisiasa kabla ya uchaguzi na kuleta mshgangao mkubwa. Ndo maana sasa hivi ukiwatonesha CCM kuhusu uifisadi wanalia hovyo kama watoto wadogo badala ya kukabiliana vilivyo na hoja hiyo. Sijui kwa nini wanaiogopa hiyo hoja -- mara maadili, mara matusi -- ilimuradi hawana nerve ya kuijibu kwa ufasaha.