Elections 2010 Slaa: Umasikini hauondolewi kwa bajaji

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
7,619
Reaction score
4,299
Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Dr. Willibrod Slaa amesema umasikini wa watanzania hauwezi kuondolewa kwakuwanunulia Bajaji (Pikipiki ya matairi matatu) iliyotolewa naJakaya Kikwete kwa ajili ya wajawazito wakati yeye akitembelea gari la Sh 400 milioni. Dr.Slaa amesema bajaji sio msingi wa kuwaondolea umasikini wa Mtanzania na kwamba yeye binafsi hawezi kuahidi chochote kwa kuwa si ofisa miradi ambayo ipo katika michakato na inasubiri utekelezaji, ni kuchezea akili za watanzania.
 
pata picha mama mjamzito amepanda kibajaji ilihali kikwete anatembelea gari la mabilioni. Kama kweli wananchi wanataka kufaidi rasilimali zao basi wampigie kura dr Slaa
 
Kweli kabisa jamaa yangu yaani inaumiza roho sana! Kinachonishawishi mimi kumpa kura yangu Dr.Slaa nikwamba yey kasema iwapo wananchi wakimpa ridhaa ya kuongoza hii nchi ni ataupiga vita umasikini uliokidhiri kwa watanzania ambao kiongozi wa awamu ya kwanza aliupiga vita lakini viongozi waliomfuata baada yake wameshindwa! Kweli tunaweza kuundoa umasikini kwakuwapatia wajawazito Bajaji??? Natumaini kunaahadi moja kaisahau na tusishangae atakapoitoa kwa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kwamba wakimchagua atawafungulia BABU SEA NA PAPII KOCHA! Hashindwi huyu jamaa kwakua kuna ahadi ameshazito natumaini atakua ameshazisahau. Tafakari wewe Mtanzania!!:A S 13:
 
toka ambulance ya combi enzi zile mbaka kibabaji tena baada ya kuuza dhahabu kwa saana tu , wenyewe watakwambia tumepiga hatua kwenda mbele pato la taifa limeongezeka, tumeongeza urefu wa barabara zenye lami, tuna vodacom ambao wapo kwenye tax holiday nk nk i ndiyo tanzania ya mtoto wa chalinze, babuye chifu wa chalinze mpaka mlogolo
 
Mfa maji haishi kutapatapa jamani huyo JK ndo anazama sasa haishi kutapatapa na kutoa ahadi za uongo. CCM Kwishney
 
dk%20slaa%2021.jpg
DK Slaa

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema umasikini wa Watanzania hauwezi kuondolewa kwa kuwanunulia bajaji akibeza ahadi hiyo ya ununuzi wa pikipiki za magurudumu matatu iliyotolewa na Jakaya Kikwete kwa ajili ya wajawazito huku yeye akitembelea gari la Sh400 milioni.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Songea katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi ya Majengo huku akishangiliwa na wananchi waliokuwa wakipasa sauti kuimba "rais, rais, rais".

Dk Slaa alisema bajaji si msingi wa kuwaondelea umaskini wa Mtanzania na kwamba yeye binafsi hawezi kuahidi chochote kwa kuwa si afisa miradi na kwamba kuahidi miradi ambayo ipo katika michakato na inasubiri utekelezaji, ni kuchezea akili za Watanzania.

Mbunge huyo Karatu anayemaliza muda wake alisema CCM imefikia mwisho na ndiyo maana inaahidi ahadi zisizokuwa za msingi ambazo yeye hawezi kuziahidi kwa wananchi na kuwa Chadema itashugulikia matatizo ya msingi ambayo marehemu Baba wa Taifa aliyashugulikia.

Aliyataja mambo ya msingi ambayo atayashughulikia iwapo wananchi watamchagua kuwa rais kuwa ni umaskini uliokithiri kwa Watanzania ambao kiongozi wa serikali ya awamu ya kwanza aliupiga vita lakini viongozi waliomfata baada yake wameshindwa kushugulikia.

Alirejea tena ahadi yake ya kupunguza bei za vifaa vya ujenzi na kuwafanya wananchi wajenge nyumba bora za kuishi, akiahidi kuwa miaka mitano ijayo Tanzania itakuwa na nyumba zilizoezekwa kwa bati.

Alisema jambo jingine la msingi ambalo atalishugulikia ni elimu na kufafanua kuwa msingi wa umaskini wa Mtanzania unatokana na kutopata elimu na hivyo serikali yake itahakikisha inasimamia ili watoto wote wapate elimu ya awali kwa kuwa elimu ya Mtanzania imekuwa ikididimia kuanzia chini.

“Tanzania ya wakati wa Nyerere, elimu ilikuwa bure na mimi baba yangu alikuwa mfanyakazi kwa mzungu na nimesoma na kuitwa daktari, lakini Tanzania ya sasa si ya Nyerere... tumeshindwa kugawana kidogo kilichopo. ilkiwa mtanichagua kuwa rais, nitatumia raslimali zilizopo kuhakikisha Watanzania wote wanasoma elimu inayowawezesha kupata kazi,” alisema.

Mgombea huyo alitambua mchango uliotolewa na unaoendelea kutolewa na madhehebu ya dini hasa Kanisa Katoliki katika elimu na kusema bila mchango huo wananchi wengi wa Songea wasingepata elimu.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alidai kuwa Kikwete amejialika kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) utakaofanyika mjini Songea kuanzia Jumapili.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Songea, Dk Slaa alisema kuwa Kikwete hajaalikwa ila katumia mabavu yake kuhudhuria mkutano huo.

“Hii ni rushwa ya hali juu ambayo inapingana na Sheria na Gharama za Uchaguzi aliyosaini mwenyewe,” alisema Dk Slaa.

Katika mkutano huo wananchi waliwazidi polisi nguvu na kusogea karibu na jukwaa kumsikiliza Dk Slaa.

Alidai Kikwete ni fisadi kwa sababu ufisadi umemkaa kichwani mwake na rohoni mwake ndio maana matendo anayofanya hayaendani na juhudi za kuacha rushwa kama anavyosema.
“Ndani ya walimu hao kuna usalama wangu wa taifa humo ndani, watasema yote atakayojadili,” aliongezea Dk slaa.

Alidai kuwa usalama wa taifa wamweleze Kikwete ukweli wa hali halisi ya siasa inavyokwenda ili asije pata presha siku ya matokeo.

“Ni aibu siri ya mkubwa inapovuja... ndani yao wameparanganyika na Watanzania wameamua mabadiliko hivyo hakuna anayeweza kuwazuia,” alisema Dk Slaa akimwomba atambue alama za nyakati kwani atatia aibu mbeleni.

Pia alibeza safari za Kikwete kwenda nchi za nje na kurudi na ahadi neti na walimu wa “peace corps” ambao walianza kufanya kazi nchini tangu mwaka 1960.

Alisema ni aibu kwa rais kusifika nje wakati wananchi wake hawaoni cha kumfanya apate sifa hizo kutokana na matatizo waliyonayo.

“Mwanaume gani unasifiwa na jirani yako wakati mke na watoto wako wako ndani wanataabika kwa shida ambazo hawajui zitaisha lini,” alisema Dk Slaa.

Alisema serikali ya CCM inatengeneza mazingira ya rushwa kwa wananchi wake kwani mishahara yao nikidogo sana isiyoweka kidhi mahitaji yao ya kila siku.

Alimponda mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emmanuel Nchimbi kwa kukosa kufanya mambo ya maendeleo katika jimbo lake kwa miaka 10 ya uongozi wake.

Naye Mgombea ubunge wa ubunge Songea Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mbogoro Aswald alisema uchaguzi wa mwaka huu ni vita kati ya uadilifu na ufisadi, giza na mwanga.
Aliwaomba wananchi wasichague chama bali mgombea atakaye waletea maendeleo.
Chanzo: Slaa: Umasikini hauondolewi kwa bajaji
 
Slaa: Umasikini hauondolewi kwa bajaji Saturday, 02 October 2010 07:43 0diggsdigg

Joyce Joliga na Beatusi Kagashe, Songea

naam well said! Hivi piga picha mwanamke mjamzito anauchungu halafu kabebwa kwenye bajaj. Mimi mwenyewe na akili zangu bajaj naziogopa kupanda. Sembuse mjamzito? Bora angesema kila hospital atagawa ambulance kuliko mabajaj. Huyu anataka kunufaisha watu tu bure.
 
KWENYE hiyo PICHA hapo juu RAIS SLAA kashika kitabu gani? Kinahusu nn i mean. People im just interested .
 
God willing, at last Tanzania may get a leader; we have been groping in darkness for over three decades now. A good number of our population was born during the period wa had no progressive leadership. As such most of our people grew up under the darkness of poverty and ignorance to the extent that they really don't know their rights and responsibilities; hence they end up being more poor and more ignorant. I guess Dr. Slaa will break that cycle.
 
Jamani nchi hii ni kubwa.

Kuna sehemu zingine hawaelewi maana ya neno bajaj ni msamiati. Inategemea na hadhira waliohudhuria wakati jamaa anatoa hotuba. Wanafikiri wameahidiwa kitu cha maana.
 
Wamezoea kuwadanganya wananchi hao na sasa umefika mwisho wao. Hana jipya huyo anatapatapa tu hayo ya bajaji ni kama yale ya kutokomeza malaria kwa chandarua na ngao. Ni kwa jinsi gani naitamani 31 oct.............its beyond my imagination. Namuomba Mungu anipe uzima, nguvu na afya niweze kuiona siku hiyo.
 
Back
Top Bottom