Slaa: Warioba asibezwe!

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,906
na Josephat Isango

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba, inawatakia mema Watanzania hivyo iungwe mkono.

Chama hicho kimesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakitaki mabadiliko hapa nchini ndiyo maana kinabeza na kimejipanga kukwamisha baadhi ya mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba mpya.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, katika mikutano ya mabaraza ya wazi ya Katiba mpya.

Alisema viongozi na makada wa CCM wamekuwa wakiibeza rasimu hiyo iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Joseph Warioba kwa kuihofia kuwa inakiondoa madarakani chama chao.

Alisema katika mapendekezo ya tume hiyo imeweka wazi kuwa serikali itakayoingia madarakani italazimika kuchukua hatua kuzuia dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa na upendeleo.

"Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaki maneno hayo yawemo kwenye rasimu ya Katiba, wanajua wanavyotumia vitendo hivyo kuendelea kukalia madaraka," alisema.

Dk. Slaa alisema Katiba mpya si ya Rais Jakaya Kikwete wala Chama Cha Mapinduzi (CCM) bali ni ya wananchi.

"Katiba ni ya wananchi, si ya Kikwete wala CCM, wanaobeza rasimu hiyo wanapaswa waheshimu maoni ya wananchi kwani yaliyomo humo yote ni mawazo yaliyokusanywa kutoka kwa wananchi," alisema.

Dk. Slaa alisema CHADEMA inaunga mkono mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba mpya yaliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Dk. Slaa alisema CCM ina hofu na utawala wake kutokana na vipengele vingi vya rasimu ya Katiba kuminyaminya yaliyokuwa yakikinufaisha chama hicho tawala.

Alibainisha kuwa suala la Katiba mpya halikuwa ajenda ya CCM ndiyo maana viongozi wake walikuwa wakitoa matamko kupinga mchakato wake.

Dk. Slaa alisema katika uchumi tume imependekeza kuwa serikali ihakikishe inachukua hatua za kuwaletea wananchi maisha bora na kuondoa umaskini.

Alisema CCM hawataki wananchi waondolewe umaskini ili waendelee kuwatawala kwa urahisi, lakini CHADEMA inakubaliana na mawazo ya Tume ya Warioba.

Alibainisha kuwa Tume ya Warioba inapendekeza Katiba iseme kuwa rais atakayeahidi jambo ama utekelezaji wake akiingia madarakani asipotekeleza ashtakiwe lakini CCM wanakataa huku CHADEMA wakilikubali.

Dk. Slaa alisema chama chao kinaunga mkono hoja ya serikali tatu, kwakuwa ndiyo suluhu la matatizo ya muungano.

Alitoa mifano ya Sudan na Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia, kuwa muungano wa nchi hizo ulilazimishwa na matokeo yake ulisambaratika.

Alibainisha kuwa rasimu inataka wawekezaji walinde masilahi ya ndani si kuweka masharti hata kwa mambo tunayoyaweza.

"CHADEMA kinaunga mkono tume huru ya uchaguzi, kinakubaliana na nchi kuwa na tume ya maadili ya uongozi na yawe bayana lakini wenzetu wa CCM hawataki," alisema.

Kuhusu suala la udini, alisema uhuru wa miaka 50 unaosifiwa ulipatikana kwa kuzingatia ibara ya 19 ya Katiba iliyopo inayotambua uwepo wa dini mbalimbali.

"Serikali haina dini, Watanzania ndio wenye dini. Ni wajibu wa serikali kuwalinda, wafanye ibada bila bughudha. Tumuunge mkono kupinga udini na kudumisha amani ili tuishi kama ndugu," alisema Dk. Slaa.

Chanzo: Tanzania Daima
 
huyo ndiyo Doctor wa ukweli. wengine wa kuchakachua, wa kupewa degree za heshima as if wana-deserve
 
Magamba wanatapatapa. Lakini mwaka 2015 mabadiliko ni lazima!!

 
Huyu chapombe isango huwa ananikera sana
 
Uandishi njaa huu kusifia ujinga plus
 
huyo ndiyo Doctor wa ukweli. wengine wa kuchakachua, wa kupewa degree za heshima as if wana-deserve

unasifia ujinga,mtu anapora wake za watu, hupati posho yako leo.
 
Hamalali bila kuitaja ccm, mwalimu wenu wa demokrasia na ustaarabu
 
Kazi za UN au COMMONWEALTH ni pamopa na kuhakisha WANANCHI wa nchi hizo wanakuwa na DEMOCRACY ktk KUCHAGUA kiongozi wamtakae na MAPENDEKEZO wananchi yanapewa kipaumbele.# CCM iiache tume iwe huru kwelikweli kwani hayo ni mapendekezo ya WATANZANIA WOTE, <chakachua mpk rasimu>
 
huyu IFWEELO naona njaa itamuua,namshauri tu atafute kazi ya kufanya na si hiyo ya kutetea utumbo unaofanywa na magamba kwa ujira wa bk 7 kwa siku,ni aibu kwa dume zima kuishi kwa upambe ili tu uwezeshwe kwenda choo,NI AIBU KWAKO NA FAMILIA YAKO
 
Watz tunapongelea suala la katiba tuache upuuzi,hili si taifa la wapuuzi na kama ni upuuzi komeeni hukohuko LUMUMBA,UKUMBI WA PIUS MSEKWA DOM.mambo ya msingi kama raslimali za taifa,maadili ya uongozi,haki za binadamu,tume huru ya uchaguzi na serikali 3 hayachakachuliki na wananchi tupo tayari kwa lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…