SLAB ya shimo la choo

SLAB ya shimo la choo

Duniatunapita man

Senior Member
Joined
May 5, 2024
Posts
181
Reaction score
252
Habari members,

Naomba kufahamu kias Cha material ya kufunika choo (slab),. Nilishachimba SHIMO la square Kwa vipimo vya futi 5 Kwa 5 na kimo ni futi 12. Hapa naomba kujua nondo ni ngapi, kokoto ndoo ndogo ngapi, na siment mifuko mingapi?

Na kama kunachochote kinahtajika naomba nifahamu , Ili niweze kushauriana na fundi. NB: sio haya mashimo ya kisasa
 
Umesahau mbao za sahani (1x8 au 1x10) na Binding wire

Hiyo 5ft kwa 5ft ni kipimo cha ndani kwa ndani, ama nje kwa nje?
 
Mbao sawa, futi 5 Kwa 5 ni Kwa ndani baada ya kujenga
- Nondo 3 zinatosha kwa spacing ya 175mm kati ya chuma na chuma, japo kwa upande wangu nakushauri utumie spacing ya 150mm ambapo utatakiwa uwe na nondo 4 (japo itabaki, ili isibaki tumia spacing ya 125mm)

- Binding wire kilo 1

- Mbao za sahani, 1x6 nunua mbao 5 za futi 12 (hizi lazima ununue kwa sababu ukishamaliza matumizi huwezi kuzitoa, zinabaki huko huko chini)

- Mbao za kingo pembeni, 1x8 (hizi unaweza ukakodi ili kuokoa gharama sio lazima ununue, kodi mbao 4 za mita mbili mbili ambapo utatumia kama sh 6000 @ 1500/pc

- Cement, hapa sasa inategemea na ratio ya zege na unene wa slab yenyewe. Kwa ratio ya grade 15, utatumia mifuko miwili na robo, chini ya hapo zege yako itakuwa chini ya grade 15. Kwa kuwa hardaware wanauza cement kwa mfuko, itabidi ununue mifuko mitatu ambapo ukichanganya mifuko yote mitatu, zege yako itakuwa inacheza kwenye grade 15 kwenda grade 20. Unene wa slab tumia nchi 6

- Mchanga, nunua ndoo kubwa 12

- Kokoto, nunua ndoo kubwa 24

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ubarikiwe kiongozi,. Imeeleweka sana
 
Kwanini mbao za ndani ya shimo hazitolewi wakati slab ikishakauka inakuwa na uwezo wa kujishikia yenyewe?.
 
Zinawekwa mbao na juu yake inamwagwa zege. Kwahyo Zinakua chini ya hiyo zege, hivyo huwezi kuzichomoa.
Mantiki yangu ni kwanini kwenye shimo zisiondolewe huku maeneo mengine kama kwenye veranda huwa zinaondolewa?.
 
Huwezi kuzitoa kwa sababu zile mbao huwa zinalala juu ya kuta za karo ndipo zege inamwagwa.

Kama utataka uzitoe, basi katika uwekaji wa hizo mbao inabidi usitumie kuta za karo kama support ya mbao za sahani, mbao zako inabidi ziflash na nyuso za kuta kwa juu. Chini ya mbao za sahani kunakuwa na mbao za 2x4 zinalazwa perpendicular na mbao za sahani. Zoezi la kung'oa hizo mbao tena ukiwa chini ya shimo sio zoezi jepesi ndio maana wengi wanaziacha tu zikae huko huko

Kitaalam inabidi ile zege ya karo ilale juu ya kuta na sio juu ya mbao kama wengi wanavyofanya maana mbao ikishaanza kuoza, slab inashuka chini kuzifata kuta hivyo inaacha ufa katika maungio ya slab na kuta
 
Hoja yangu ndiyo ilikuwa hapo sasa. Maana sijawahi kuona hizo mbao zikiachwa bila kutolewa.

NB: Kwanini umeshauri kwa mtoa mada kutoziondoa hizo mbao baada ya kulifunika kwa zege shimo lake?.
 
Akiweza kuzitoa ni sawa pia na ndio vizuri, mimi sijamkataza asizitoe, point hapo ilikuwa ni kumpa idadi ya mbao za kununua na mbao za kukodi maana hawezi akakodi mbao na kuziacha huko chini kwa wiki mbili mpaka tatu then azing'oe azirudishe kwa wahusika, gharama yake itakuwa ni ile ile tu kama ya kununua mbao
 
Back
Top Bottom