Slumdog Millionaire: Filamu ya kihindi inayoonyesha maisha ya masikini wa India

Slumdog Millionaire: Filamu ya kihindi inayoonyesha maisha ya masikini wa India

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Ni filamu ya kihindi iliyotengenezwa mwaka 2008 inayoonyesha maisha ya kijana aliyekulia mtaani na kuwa tajiri kwa bahati tu

Filamu ilianza kwa kumuonyesha muhusika Jamal, akiwa kwenye kipindi cha ‘who wants to be a millionaire’ kipindi kilikuwa kinauliza maswali mengi tofauti na atakaye patia majibu yote basi anapesa hela za kutosha za kuuaga umasikini

Kitita cha takribani Tsh milioni 600 kingetolewa kwa mshindi. Kijana Jamal alipata maswali mengi kiasi ambacho mwenye, shindano lake akaona anaibiwa na Jamal alikamatwa ili aseme ni kwa namna gani ameweza kupatia maswali mengi

Hapo ndipo kwenye filamu kwa kuwa maswali mengi aliyokuwa anaulizwa yalikuwa yanalenga kwenye maisha ya mtaani ambayo amepitia. Kwa kuwa hakupitia shule za kawaida alikosa swali moja kuhusu bendera ya nchi yao

Hii ni moja kati ya filamu iliyoonyesha maisha mabovu ya India, yale ya chini kabisa kuliko yale maisha ya uswahilini ya Tanzania. Je wewe ni filamu gani unaipenda?

1588075664444.png
 
Kwa Indian movies naikubali sana Three Idiots.

Imelenga kwenye mapinduzi ya kifikra na kielimu.
Jamaa anapambana kubadilisha education system ya india kutoka kuthamini grades za ufaulu ambapo huishia kukariri notes za vitabu kufaulu mtihani badala yake wathamini ubunifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo promo uliyopiga naenda kuitafuta japo movie za kihindi na kijapan sijawahi kuziangalia
 
Bwana mdogo maisha aliyopitia yalikuwa na majibu yote ya maswali anayoulizwa simple kawa millionaire wakahisi anacheat ni filamu nzuri tofout na ile yakuchezacheza zina bore kishenzi.
 
Back
Top Bottom