Smartphone ya msanii wa kike yaokotwa Club na kunadiwa kwa $15,000

Mwana Ilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
1,287
Reaction score
486
Hallo Wana JF.

Napenda kutoa RAI ya tahadhari kwa wale wanaomiliki vilongalonga aina ya Smartphones kwa kile wanachohifadhi katika simu zao.

Umezuka mtindo hivi sasa,naweza kusema kwa baadhi ya watu wasiokuwa na maadili kutumia simu zao na kujirekodi wakati wakiwa Faragha/Jamiiana/tifuana na wapenzi wao.

Tabia hii naweza kuiita ni Highest degree ya UJINGA. Kwa sababu haileti maana kwa yule unayemuita ni Mpenzi/Mme/Mke umrekodi wakati mnashughulika na kuhifadhi picha kama hizo kwenye simu yako/zenu. Kwa sababu yule ni Mpenzi/mwandani wako, mda wowote unapomuhitaji unampata. Sasa iweje leo hii utembee na Video mlizojirekodi mkiwa mnajamiiana/tifuana!?

Ok, acha niongelee madhara ambayo unaweza kuyapata kama na wewe ni mmoja ya watu wanaojirekodi na wapenzi wao mkiwa faragha.

Moja, Madhara ambayo unaweza kuyapata ni hili la kuachana na huyu unayemuita Mpenzi/Hawara/Mke au Mume. Akiamua kukudhalilisha kwa kusambaza utupu wako kwa Marafiki zako na hata wale wasiokujua, Utaificha wapi sura yako!?

Pili, Kuna suala la Simu kupotea/kuibiwa. Ukiibiwa simu leo hii na ikatokea kuwa ulikuwa umehifadhi huko picha kama hizo!? Utakuwa Mgeni wa nani!?
Mfano, Nchini Philipine,Jamaa mmoja alipokuwa night CLUB aliokota Simu ya Mdada Msanii Maarufu wa Tasnia ya Drama, aliporudi nyumbani kesho yake akamsimulia rafiki yake kuwa ameokota smartphone na anataka amtafute mwenye nayo amrudishie.

Rafiki yake alikuwa ni mtundu sana wa simu akichukua na kuifungua kuangalia contents zilizomo Ndani. Wakagundua kuwa ilikuwa ni simu ya msanii maarufu wa sinema na Mbaya zaidi alikuwa amejirekodi video nyingi na picha kadhaa za UCHI akiwa faragha na mpenzi wake.Akamshauri kuwa hapo umaskini ndio bye bye.

Wakatoa tangazo la kuinadi kuwa kuna simu ya Msanii imeokotwa ila mwenye nayo atalazimika kuikomboa kwa 12M za kibongo. Waandishi wa habari wa udaku huko Philipine walipoliona hilo tangazo wakajua moja kwa moja hiyo itakuwa ilikuwa na kitu cha zaidi haiwezani simu iokotwe kisha inadiwe kwa hela nyingi hivyo.

Waliookota hiyo simu wakavutiwa uzi/simu kutoka kwa waandishi wa habari za udaku(Let's Say GLOBAL PUBLISHER ya huko kwao) kutaka kujua ni nn hasa mpaka hiyo simu ikombolewa kwa bei kubwa hivyo.

Waandishi wa habari wakapanda dau hadi $18,000. Msanii aliyepoteza simu akafikia $15,000.
Waliookota simu Wakawa na utu wakampatia mwenye nayo badala ya waandishi wa habari.

Tatu, hasara ya tatu, Rafiki yako anaweza akakuibia picha/Video zako bila ya ww kujua, halafu siku mkigombana unashangaa picha zako zina-whatsappiwa kila kona ya Mtaa unakoishi bila kujua chanzo ni nani.

Nne, Ukipeleka simu kwa fundi, hata kama umezifuta au umezihamisha hizo picha ndio ukaamua kumpelekea Fundi. Uwezekano wa kuzi-recover ni mkubwa sana. Au let's assume kuwa simu yako imezima ghafla kabla hujazihamisha. Si lazima umpelekee fundi!? What will happen kwa Fundi!?? Jibu unalo Mwenyewe

Nnatoa wito wa tahadhari kwa watumiaji wa smartphone kuwa na matumizi yaliyo sahihi katika simu zao. La sivyo zitawaondolea utu wenu.

Kumradhi kwa kichwa cha habari kukuvutia na kuisoma hii TAHADHARI. Najua umeelimika na. Simu yako utaitumia kwa umakini na Usahihi.

Thanks wana JF.
 
Wewe kweli ni kanjanja .kichwa cha habari unasema msanii wa bongo movie na ndani unasema msanii wa uko filipino.

Huo ni ukanjanja unaofanywa na makanjanja. Hadithi yako nzuri tatizo ni huo ukanjanja
 
Hajasema msanii wa bongo movie jamani!!!™
Kwan ufilipino hakuna wasanii??
 
Wewe kweli ni kanjanja .kichwa cha habari unasema msanii wa bongo movie na ndani unasema msanii wa uko filipino.

Huo ni ukanjanja unaofanywa na makanjanja. Hadithi yako nzuri tatizo ni huo ukanjanja

unaweza kusoma kwa ufasaha kweli?soma vizuri kichwa na habari mkuu
 
Asante mkuu ujumbe umeeleweka hao wanaohangaika na kichwa cha habari achana nao
 
Asante mkuu ujumbe umeeleweka hao wanaohangaika na kichwa cha habari achana nao

Kichwa cha habari ni lazima kiendane na habari yenyewe.

Alikuwa ameandika smartphone ya msanii wa bongo movies kunadiwa $15000 harafu ndani inaonyesha ni ufilipino.

Siwez kuona uchakachuaji wa hivi ukiendelea apa siyo magazet ya udaku.

Lazima kichwa cha habari kiendane na habari yenyewe ila naona washarekebisha kichwa cha habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…