`SMZ rudisheni hati za kusafiria`

Lakini hao mafisadi Muungano wao unawanufaisha vipi?

Kwa sasa sidhani kama wananufaika na chochote ukiondoa uwezekano wa hao mafisadi kuwa shareholders katika makampuni ya simu yaliyowekeza visiwani, lakini yakipatikana mafuta visiwani (kuna rumours kwamba yameshapatikana) basi mafisadi ndiyo watakaonufaika kuliko mwananchi mwingine yeyote, kama wanavyonufaika sasa hivi ni rasilimali zetu mbali mbali ikiwemo dhahabu.
 
nilitaka zaidi muone ni upi uelewa wa cuf kwa ndugu zao wa bara.

chama cha cuf kikipata kinatarajia kabisa kuuvunja muungano na sijui itakuwaje maana vile vile hawaivi na ndugu zao wa unguja.

sasa sijui mambo yataendaje kwa kweli hatari sio ndogo

wenzetu hawa ukifatilia mazungumzo yao yawe baraza la uwakilishi au bungeni au kwenye majimbo yao ni rahis kufahamu nini mission yao underground.

watu sasa wanasonga mbele nakuangalia kutafuta suluhisho la matatizo yao bila ya kutengana wao wanaona kutengana ndio tiba ya matatizo yetu/
 
Akufukuzae hakwambii TOKA!

UKIMWI Tanganyika,UFISADI,UJAMBAZI,MADAWA WANAYOBWIA KILA SIKU NK!

Kila tatizo limetoka Tanganyika.

Ushoga nao wa TANGANYIKA?

Hivi hizi ni prapaganda za MAFISADI NINI?
MAANA HAIJAKAA SAWA KABISA!

KUSAFISHANA!
ccm NI MOJA!

BE IT YA TANGANYIKA,ZANZIBAR AMA TANZANIA.

BE IT KARUME,KIKWETE,AMA NYERERE MTUPU(MKAPA).

Na kama kauli hizi zinatokea kutoka kwa wanachama wa ccm...Then hakuna cha unguja,pemba,bara wala whatever.

WOTE NI MAFISADI,MADAWA YA KULEVYA NI BIASHARA YA ccm AMA TANGANYIKA VS ZANZIBAR?

KAMATENI MAFISADI KWANI SASA MMEKOSA LA KUONGEA!

NA KAMA ccm HAMNA LA KUONGEA...THEN NI BORA MKAE KIMYA TU KWANI NI AIBU TUPU!
 
Mtu wa Pwani,
Hata kama watarudisha pasi, majambazi yanayotoka Bara yatatumia hizo pasi. Kwani ujambazi umeandikwa usoni?
 

Bahati mbaya wakati upatikanaji wa mafuta ni rumours lakini bara traces zimepatikana Mkuranga. Kuna uwezekano mkubwa mafuta yakapatikana bara kabla ya Zanziba. Ndiyo hapo utakapowasikia wakidai mgawo wa 50/50 wa mapato!
 
Mi naombea huu muungano uvunjike ili hawa wajinga wajitawale wenyewe. Tuwakatie Umeme hawa.

Hii CUF mi siku zote nasisitiza ni wajinga sana. Ndo maana sisi (CCM) tutaendelea kuwatawala milele!
 
Mtu wa Pwani,
Hata kama watarudisha pasi, majambazi yanayotoka Bara yatatumia hizo pasi. Kwani ujambazi umeandikwa usoni?

hawa ndugu zetu kina mwiba ni watu wana undani sana, ni watu wenye sura mbili anachokizungumza sicho kilichomo ndani ya roho yake

hawa wao wanaamini bara ni washenzi na wanaamini wazanzibari ni waarabu

sasa utajaza doti.
 
Imani ni kuwa bara wanautaka na wa visiwani hawautaki!

Ahsante.

Na samahani kwa maswali yasiyo isha.

Sasa, huku Bara ambako tunautaka, ni majority au minority wanautaka?

Bubu Ataka Kusema nae ana wonder, kama mimi pia, kama ni minority tu wanautaka, kwa nini bado uko imara?

Inawezekana ni kwa sababa hao minority ni the elite class, political and economic. Lakini hawa Wakulu wa Bara, Muungano wao unawalinda vipi?
 
Bahati mbaya wakati upatikanaji wa mafuta ni rumours lakini bara traces zimepatikana Mkuranga. Kuna uwezekano mkubwa mafuta yakapatikana bara kabla ya Zanziba. Ndiyo hapo utakapowasikia wakidai mgawo wa 50/50 wa mapato!


Fundi Mchundo, wanaweza kudai mgawo wa 50/50, swali je wataupata? Sasa hivi mgawo wa dhahabu hata bara tunaupigia kelele na sidhani kama unawanufaisha visiwani ikiwa bara kwenyewe haturidhiki. Yakigundulika mafuta ambayo yanaweza kuuzwa kibiashara basi hapo ndipo kutakuwa na kizaa zaa nguo kuchanika.
 

Hamna tatizo,Mkuu!
Key word ni imani. Kwa vile hatujafanya referendum, hakuna anayejua idadi kamili, ni makisio tu. Sitoshangaa kama ikifanyika referendum ikakutwa kuwa hali sio hii.
 

Mkuu, kwa watu ambao hawana hata punje ya dhahabu, chochote wanachopata ni icing kwenye keki. Mafuta yakipatikana bara ni lazima watapata mgao. Kazi,yakipatikana Zanziba, maana bado kuna usongo wa utajiri wao wa karafuu ambao wana amini bara ilifuja.
 

Bara hakuna hata mmoja anaetaka muungano huu ,maana walifikia kuunda umoja wa kuidai Tanganyika irudishiwe Uhuru wake pale bungeni wakati wa siku za mwisho mwisho za Mwalimu Nyerere.
Na kila siku Mtikila anasikika akipiga makelele kuwa Tanganyika lazima irudi na iwepo kama zamani ila hajaitwa mhaini halafu nimesikia kuwa wapemba mambo yao mazuri ,ikiwa kura itakayopigwa UN itakuwa na wao basi watapatiwa kajisehemu chao kama East Timor.
Kuna mpango ambao utajulikana kama UNTAP (UNITED NATIONS TRANSITIONAL ADMINISTRATION IN PEMBA)
 

Hii wazungu wanaiita 'witch hunting', someone should tell this mama aachane na hizi ndoto za alinacha kwa kuwa pasi za watu za kusafiria hazionyeshi status za HIV wala ujambazi. Cha muhimu ni serekali ya mapinduzi kupanga mikakati ya jinsi ya kupunguza maambukizi ya ukimwi na kukabiliana na vitendo vya ujambazi.
 
Soma maandishi ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi toka CUF ,aliyoyasema leo.

Akichangia bajeti hiyo Mwakilishi wa Viti Maalumu (CUF) Zakia Omar Juma amesema hakuna mtu mwneye akili timamu ambaye atataka muungano huu wa tanganyika na zanzibar uvunje.
Alisema pamoja na kuwa wazanzibari wengi wanapenda muungano udumu lakini kumekuwepo na dharau fulani ambayo inaoneshwa na upande mmoja kwa kuwa inaonekana zanzibar ni sehemu ndogo na yenye idadi ndogo ya wakaazi wake.
Mwakilishi huyo amesema ipo haja ya kufanyika kwa vikao vya wazi ambavyo wayakaoshiriki ni wazanzibari na watanzania bara ili kutoa dukuduku bila ya kujali tofauti za vyama kwani kinachowaunganisha ni uzanzibari na sio vyama.
 
..suala la mafuta haswa yanapopatikana off-shore ni uwembamba wa mkondo wa bahari kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.

..sheria za bahari na matumizi ya rasilimali za baharini ni ngumu kutukelezeka ktk mazingira ya mpaka kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.

..mgogoro wa fedha kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ulishapelekwa kwa msuluhishi wa kimataifa. huko ndiko kulikotokea mapendekezo ya Zanzibar kupata 4.5% ya mapato ya Muungano, na kuanzishwa kwa akaunti ya pamoja kati ya SMZ na SMT.

..nina mashaka sana kama huyu mtaalamu aliyetafutwa sasa hivi atakuja na mapendekezo ambayo Zanzibar watakubaliana nayo kuhusu mgawo wa mafuta, gesi,na rasilimali nyingine. tatizo la Wazanzibar ni kudai kila kitu kiwe 50/50 ktk Muungano.
 
Ukiniuliza tangu nimezaliwa mpaka leo nini faida za Muungano..SIJUI ATA MOJA!!!!
Kama wakitaka kuvunja Muungano wauvunje tuu...
 
Ukiniuliza tangu nimezaliwa mpaka leo nini faida za Muungano..SIJUI ATA MOJA!!!!
Kama wakitaka kuvunja Muungano wauvunje tuu...

Mimi nadhani majority of the people, Bara na Visiwani respectively, hawataki huu Muungano. Mme analalamika sitaki ndoa, Mke analalamika sitaki ndoa.

Lakini una survive, na kushamiri, na kudumu. Sijui kwa nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…