Snura,Jux na Madee wana stahilii adhabu hii kutoka kwa BASATA?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam Wanajamvi.

Bila shaka wapenda burudani mnajua fika BASATA nini na wanafanya kazi gani.Bahati mbaya au nzuri hawa BASATA wamekuwa wakionekana wakipaza sauti zao kwenye matukio makubwa, pengine tuseme yanaweza kuwa na manufaa zaidi kwao.

BASATA wamekuwa wakiandaa Tunzo za wasnii hapa nchini kupitia beer ya Kilimanjaro na kuziita Tunzo hizo Kilimanjaro Music Awards.

Toka Tunzo hizi zimeanzishwa Sauti ya'kulinda maadili na kupelekea nyimbo za wasanii kuenguliwa sikuwai kuisikia lakini nimeisikia Mwaka huu 2014 tena kipindi cha hiki cha Mchakato wa Tunzo hizi.

Ni ukweli usiopingika kabisa music wetu hasa bongo fleva umekosa wasimamizi na watu wa kuchuja nyimbo zenye mantiki na kulinda maadili yetu na ndio maana hata wengine wanamua kutukana kabisa kwenye nyimbo zao.

Tukiangalia nyimbo zilizo tolewa nje ya mchakato wa kuwania Tunzo za kili pengine zina stahili kabisa kwa vigezo vyao vya maadili.
Mfano Nimevurugwa -Snura
Tema mate-Madee.
Uzuri wako- Jux

BASATA NA ULINZI WA MAADILI YA WATANZANI KWA MSIMU

BASATA wanaonekana kulinda maadili ya watanzania kwa msimu na si nyakati zote na ndio maana nyimbo wanazo zi zuia kupewa tunzo bado zinaendeleo kuoneshwa kwenye vituo vya luninga.
Na wana sahau kuwa watu wanaendelea kuziangalia lakini wana subiri msimu wa Tunzo ndio waseme Maadili kwakweli huku ni kukosa msimamo.

Basata wana sahau kuwa maadili yetu yana paswa kulindwa wakti wote si wa tunzo tuu?
Mfano.
Hivi kwa nini Video ya Sugua gaga- shaa inaendelea kuoneshwa kwenye runinga? Pamoja na yaliyomo?

Hivi kwa nini Wimbo wa Roma pamoja na kupambwa na matusi bado unaendelea kupigwa kwenye radio?
BASATA ina maana macho yenu na masikio yana fanya kazi lipingi cha Tunzo tuu?

Kwanini msianzishe utaratibu wa wasanii kupeleka nyimbo na video zao kwenu kabla ya kuzipeleka kwenye vituo vya Radio na Runinga?

Kwa mazingira haya ni wazi mmewaonea kuwaengua Kwa kigezo cha kulinda madili wakti video zao zinaonekana kwenye vituo vya Runinga.
Kibaya zaidi zile ambazo hazikuingia kwenye mchuano wa kuwania Tunzo mmeziacha pengine amzioni kabisa.

Pengine kuna swali tuanaweza kujiuliza hivi kuziengua nyimbo na video fulani kuwania Tunzo ni suluhisho?Kwanini zisifungiwe moja kwa moja kuonekana na wahusika wapigwe faini?

Hivi BASATA mmefungia Filamu za Kitanzania zilizo kinyume na maadili? Au hakuna?

Ni vyema BASATA mkafanya kazi yenu kwa wakati hili muonekane mnatenda haki.

Karibu wana jamvi.
 
Umechambua sio mbaya sana,ila mimi na swali na jibu mwenyewe ila lakimtazamo wangu zaidi.Mf video ya Jux,ile ya Snura viuno,Kuna ile ya Dully video unatumia nguvu sana tunajua Tanzania ukishamweka mwanamke na bikini tayari unaleta taswira flani hivi sio nzuri kiafrica.Kwa nini hao madirector wasiwape mawazo mengine kumbuka hapa ni TZ sio USA hata kama video itavutia kuna vitu vinakuwa sio utaratibu na mila zetu.Je ukifungia ni kosa la basata mbona video za zamani walikuwa hawakatishi na vichupi?Mimi kama mimi BASATA big up fungia na kuna hii ya Shilole ipo youtube nayo tutainasa tunafungia.Usije sema haki za binadamu.Nchi zile zinazoruhusu nude video pia wanasheria zao zivunje uone moto wake mfn mzuri Ribery na Benzema kdg waende jela.
Hiyo ya shaa bahati yake tuu ishachuja ila wembe ule ule umekurupuka fungia kbs.
 
Fungia Kabisa Yan Nimeka Nakatoto Kangu Cha Miaka Kumi Na Angalia Wimbo Wakiswahi Nianze Kuona Wanakulana Ndimi Au Vibikin Uchwara Ata Kuviva Hawajui Fungia Kabsa Kan Kuna Ulazma Gan Tz Kutaka Kujifananisha Na USA akat sibado sana tupo nyuma,
Basta fanye yenu, achaneni nahawa vikoba,
 
Ndio wataelewa kuwa wana baraza la sanaa tanzania, sio mtengeneze video mbovu kwa jamii yetu
 
Ndio wataelewa kuwa wana baraza la sanaa tanzania, sio mtengeneze video mbovu kwa jamii yetu
Mkuu Andybird ukinisoma vyema utagundua kwamba tatizo lilopo hapa ni BASATA kutokuwa na msimamo kwenye maamuzi ya kufungia nyimbo na video ambazo zina kiuka maadili.

Kwanini nyimbo na video zifungiwe wakti wa tunzo tuu na ni kuondolewa kuwania Tunzo wakati tukiendelea kuziona na hayo Maadili kwanini kwenye tunzo tuu?
Kwanini ziendelee kuonekana na huku hazina maadili kama BASATA walivyo sema?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu JUSTINE Dimee hata mimi naunga mkono video na nyiombo zisizo na maadili zifungiwe lakini ninacho jiuliza kwanini ni kipindi cha Tunzo na huku hizo video zinazo semwa hazina Maadili bado zinaendelea kupigwa? Kwanini tusiseme wameonewa.
 
Last edited by a moderator:

MKuu theki hivi kwanini hizo zinazo hitwa hazina maadili zinaendelea kusikilizwa na kuangaliwa?
 
Last edited by a moderator:
Wangeanza na video zile za nje ambazo hazina maadili maana kama wanazuia hizi za ndani wakati bado tunaburudika na video za nje naona wanachofanya ni kazi bure
 
Kweli Video ya Jux haina madili kashoot kama anataka kumtia huyo demu matiti nz punyenye nje nje, na anamtia madole
 
Kweli Video ya Jux haina madili kashoot kama anataka kumtia huyo demu matiti nz punyenye nje nje, na anamtia madole
naomba niichek hyo video ya jux!kumbe nimeptwa
 
MKuu theki hivi kwanini hizo zinazo hitwa hazina maadili zinaendelea kusikilizwa na kuangaliwa?
Wanasema mbona za marekani hazina maadili lakini zinaoneshwa au kusikilizwa.Akili ya kwako sio ya kuambiwa unaweza kuzuia zisiangaliwe.Hizi za ndani ni raisi sababu ni home made na ikishatoka pia ni ngumu kuizuia tena isiangaliwe au kusikilizwa.Leo kuna sehemu za kurekodi kibao nyingine hata usajili hazina.Ni Basata kuwapa meno tuu tutanyooka.
 

Sasa hivi tunatumia decoder aka ving'amuzi haina haja ya kufungia wasanii kwani watoto na vijana wetu wanayoangalia kwenye mitandao ya kijamii kupitia simu zao ni machafu zaidi ya hizo nyimbo. Basata na serikali wanachemka kumulika tu wasanii.
 
mwanasheria bhana sasa hizo nyimbo zina kasoro gani waache waimbe watakacyo
 
wangeanza na video zile za nje ambazo hazina maadili maana kama wanazuia hizi za ndani wakati bado tunaburudika na video za nje naona wanachofanya ni kazi bure

alaf bado wanasema wana linda maadili.
 
Maadili siku hizi hayapo waachie tu tuoneee siee
 
Wangeanza na video zile za nje ambazo hazina maadili maana kama wanazuia hizi za ndani wakati bado tunaburudika na video za nje naona wanachofanya ni kazi bure

Tusi la kizungu haliumi...........TAFAKARI!
 
Jiulize kati ya Chris Brown na Diamond nani ana influence kubwa kwa vijana wengi(majority) wa mitaani.....Jamii yetu huwa sensitive zaidi na mambo yatendekayo ndani.....ndio maana Elton John,tunasikiliza nyimbo zake na hatujali habari zake lakini Anti naniliu akiji'expose',mishipa itatutoka sababu ni threat ndani ya Jamii Yatu yenye desturi zetu.....ni kweli BASATA inapaswa kutenda haki lakini kwa usawa ule ule na wembe ule ule na si kwa kulinganisha 'wao na sisi' kitu ambacho kwa jamii yetu kipo established tayari.....Niseme hiviii,Mashabiki wengi wa snura,shilole na wengineo ni wale ambao hawana time na umagharibi na wachache ambao wako na western exposure,ni rahisi ku'identify' absurdity ya culture ya wenzetu.....Unless iwe ni mapenzi binafsi.
.......Dada zetu huku wakivaa kama Rihanna haimaanish they get her style ila ni vile tuuu,Wema Sepetu alitinga jana yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…