Snura: Ukweli Nimeumia Sana na Mwaka Huu Umekuwa ni Majanga Kwangu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
BAADA ya hivi karibuni kufungiwa video ya wimbo wake, staa wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi amesema ameendelea kuandamwa na majanga ambapo hivi karibuni alipata msiba wa babu yake huku mdogo wake akipata ajali.
Akizungumza kwa huzuni, Snura alisema mwaka huu umekuwa wa majanga kwake kwani babu yake huyo alimlea na kushika nafasi ya baba yake tangu alipozaliwa hadi kufikia utu uzima.

“Ukweli nimeumia sana na mwaka huu umekuwa ni wa majanga kwangu kwani babu yangu huyo nilikuwa namuita baba kwa sababu yeye ndiye aliyenilea mpaka nikafikia umri huu nilionao, mdogo wangu naye alipata ajali mbaya yuko hoi hospitali, utumbo ulitoka nje na kwenda kufanyiwa oparesheni, nimechanganyikiwa,” alisema Snura.
 
Ndio dunia kila na mtu na majanga yake
Tukisema tuyaweke wazi kila mtu majanga hamna atakaemsikiliza mwenzie
 
Reactions: Luv
unajuwa huyu mtoto mimi nilishamsahau, mama yake tumesoma wote primary school sasa jana nimekutana naye ndio ananiambia huyu Snura ni mwanaye, kwakweli huyu binti amsaidie mama yake maana mkorogo umemuharibu ngozi imekuwa kama ya chatu na si mweupe tena bali mwekundu mweusi, kwakweli ukimuona Dotto Sanzagara anasikitisha sana. Snura msaidie Mama yako.
 
ngoja afulie totally aanze kupitisha maombi ya kusaidiwa....

They dont save these people...

What they is only ponda mali, kufa kwaja!
 
Pole sana snura,lakini huo mzigo wako ni original au mchina?samahani nauliza tu....
 
ngoja afulie totally aanze kupitisha maombi ya kusaidiwa....

They dont save these people...

What they is only ponda mali, kufa kwaja!

Amsaidie mama yake kwanza anatisha jamani mkorogo umemuharibu.
 

Kumbe we Matola ni mtu mzima hivo.Shikamoo ..
 
Last edited by a moderator:
Kumbe we Matola ni mtu mzima hivo.Shikamoo ..

Siyo mkubwa sana kivile, huyu mama yake aliishia darasa la saba kwahiyo wanazaaga mapema sisi wengine shule ndio tulitumia muda mwingi, huyu mama yake Snura pacha wake kulwa alikuwa mke wa Muddy Control mpiga gita wa sikinde ambaye amefariki mwaka jana kama sikosei.
 
Last edited by a moderator:

nilichogundua matatizo yao ni elimu ya kujitambua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…