Sober house ya kidijitali: Kwa mwezi mzima kaa mbali na smartphone, laptop, game, Internet, n.k. utapunguza uteja na utapata faida zifuatazo

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Afya ya akili

kuongeza utulivu wa kihisia - Simu zinachangia sana kutibua hisia, upo whatsapp / instagram mara unakutana na status za watu mnaojuana wametoboa huku wewe unajitafuta, wameoa / kuolewa wewe bado, timu yako imefungwa inataniwa, kuna sherehe imefanyika hujaalikwa, n.k.

Kuongeza umakini - Unapokuwa kwenye shughuli zako notifacations huwa ni usumbufu, kuna presha ya kutaka kufuatilia kurasa za mitandaoni, n.k.

Afya ya usingizi - watu wengi wanaharibu ratiba zao wakiingia na simu vitandani, mtu anacheza playstation mpaka saa tisa usiku

Afya ya mwili

Macho yanaimarika - kuongalia screen kwa kkaribu kwa muda mrefu hupunguza afya ya macho

Kunyoosha mgongo na shingo - kuinamisha shingo kwa muda mrefu ukiwa unatumia simu, ps, laptop, n.k. kunaweza kuleta kibiongo

Kuongeza shughuli za kimwili - Ukikaa mbali na electronics utapendelea zaidi kuwa nje, kutembea, kufanya mazoezi, n.k.

Socializing

Inasaidia kutoka nje kujichanganya na watu -mitandao ya kijamii na magroup yamesaidia kujichanganya kidijitali lakini hayawezi kuchukua nafasi ya kukutana physically uso kwa uso, ni muhimu kutoka nje mara kadhaa kujumuika.

Kuongeza communication skills - kuna watu ni keyboard warriors lakini ukikutana nao ni tofauti kabisa, Kuchangamana physically kunaisaidia kuwaongezea uzoefu wa kuzungumza na watu.

Uchumi

Kupunguza matumizi - Internet imekuwa na uraibu mkubwa kama ilivyo kwa ugoro na bangi, watanzania wengi wenye vipato vya kawaida bajeti ni ya kuunga bando la buku kwa siku lakini addiction inamfanya mraibu ajiunge vifurushi vya buku mara tatu au zaidi
 
Mie nikiamka asubuhi huwa sigusi simu mpaka nitoke kuoga, na kuoga kwenyewe ni baada ya mazoezi. So huw a nakua na karibu saa nzima tangu kuamka sijagusa simu.

Nikiishika simu huwa naplay muziki tu, siangalii chochote, jf huwa naperuzi nikiwa njiani kuelekea kazini.

Simu yangu haina app za insta wala tikitoko, ni jf na youtube, X niliinstal baada ya Elon kuinunua twitter thou siangaliagi mara kwa mara.

Pongezi kwa mama.
 
Afya ya akili

kuongeza utulivu wa kihisia - Simu zinachangia sana kutibua hisia, upo whatsapp / instagram mara unakutana na status za watu mnaojuana wametoboa huku wewe unajitafuta, wameoa / kuolewa wewe bado, timu yako imefungwa inataniwa, kuna sherehe imefanyika hujaalikwa, n.k.

Kuongeza umakini - Unapokuwa kwenye shughuli zako notifacations huwa ni usumbufu, kuna presha ya kutaka kufuatilia kurasa za mitandaoni, n.k.

Afya ya usingizi - watu wengi wanaharibu ratiba zao wakiingia na simu vitandani, mtu anacheza playstation mpaka saa tisa usiku

Afya ya mwili

Macho yanaimarika - kuongalia screen kwa kkaribu kwa muda mrefu hupunguza afya ya macho

Kunyoosha mgongo na shingo - kuinamisha shingo kwa muda mrefu ukiwa unatumia simu, ps, laptop, n.k. kunaweza kuleta kibiongo

Kuongeza shughuli za kimwili - Ukikaa mbali na electronics utapendelea zaidi kuwa nje, kutembea, kufanya mazoezi, n.k.

Socializing

Inasaidia kutoka nje kujichanganya na watu -mitandao ya kijamii na magroup yamesaidia kujichanganya kidijitali lakini hayawezi kuchukua nafasi ya kukutana physically uso kwa uso, ni muhimu kutoka nje mara kadhaa kujumuika.

Kuongeza communication skills - kuna watu ni keyboard warriors lakini ukikutana nao ni tofauti kabisa, Kuchangamana physically kunaisaidia kuwaongezea uzoefu wa kuzungumza na watu.

Uchumi

Kupunguza matumizi - Internet imekuwa na uraibu mkubwa kama ilivyo kwa ugoro na bangi, watu wana vipato vya kawaida, mtu kajipangia kuunga bando la buku kwa siku lakini addiction inamfanya aunge mpaka mara tatu
Hili ni andiko muhimu sana.
 
Back
Top Bottom