SoC02 SoC 2022

Stories of Change - 2022 Competition

MWK4t

New Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Vijana wa sasa katika ulimwengu huu kuna umuhimu wa kuangalia kesho yetu kwa jicho pana zaidi badala ya kuishi maisha kama mchezo wa kamali ujui lini unaweza toka kimaisha zaidi ya kusubiri kuajiriwa. Tukija chuo uwa na matarajio na maono makubwa kuhusu maisha yetu lakini kadri muda unavyo zidi kwenda tuna endekeza uzembe, bila kuwajibika na kuwa nidhamu ya fedha ni ngumu sana kufanikisha malengo yetu.

Vijana tunao soma vyuo mbalimbali hapa nchi wengi wetu tunajiona bado ni watoto au muda bado kuanza kufikiria utunzaji wa akiba, hatuna utamaduni wa kuifadhi hela kwa ajili ya kutusaidia kuanzishia au kuwekeza katika nyanja tofauti, wakati tukiwa tuna soma hata baada ya kumaliza kusoma wengi wetu tume jidhatiti kwenye kusoma, kuishi maisha ya maigizo, kushindana, mazoea, kula bata na kufata mikumbo ambayo inaishia kutufanya kuwa na maisha magumu hata kabla ya kumaliza chuo. Wanasema wazo ni muhimu lakini ni muhimu zaidi kuweka hivi vitu pamoja wazo la kibiashara pamoja na mtaji angalau uweze kusaidia katika kuanza halafu kama hikitokea msaada inakua si katika kuanza bali katika kuendeleza kile kilicho anzishwa.

Tukimaliza vyuo uwa tunarudi ma kwetu kwa ndugu na jamaa na kama tunavyojua familia zetu za kimasikini, wakulima lakini wazazi bado walijitahidi wakafanya katika nafasi yao ambapo inakua ni ngumu katika kupitisha ombi la msaada wa kifedha kwenda kwao ukiangalia gharama walizo tumia kutusomesha mpaka kumaliza ni sawa na kusema wapo hoi kifedha sio tu kifedha bali hata hela ya kukupa au kukuunga mkono katika wazo lako, pia kuna wadogo zako nao wanaitaji kuwezeshwa kufikia ulipo wewe kwaio wa wazazi wao uwa wana amini kutokana na nguvu walio tumia katika kukusomesha na ukiangalia kwa mfano mkopo wa chuo ulikua hauna basi utumie elimu yako katika kupambana na kuwasaidia wao pia.

Kwaio Akiba ya kifedha ni swala la kulidhingatia sana wakati tunaishi na kupambana na maisha ya chuo, kuna umuhimu kujiwekea utamaduni wa kuifadhi kile kidogo ulicho nacho huku tukiendelea kufikiria na kutengeneza mawazo ya kujiajiri.

Kuna msemo unasema mwenye nacho ataongezewa zaidi na asie nacho hata pokonywa hata kile kidogo alicho kwahiyo vijana tutengeneza utamaduni wa kutafuta vya kwetu kwanza kabla ya kutaka kusaidiwa maana hao wakutoa msaada uamua kutusaidia na uwa ni rahisi wakijua wana fanya nyongeza pale mtaji unapo lega au pungua, hata kwenye kuomba na kupata mkopo kuna tegemeana na kazi au mahali ulipo fikia, kwa sababu inaonesha una nia ya kufanya kitu kuliko mtu kukupa hela ya kuanzisha kitu.

Akiba ya kifedha ni hela ambayo imeifadhiwa kwa dhumuni maalumu na ina lenga kutoa msaada kama tunavyo jua kuna sababu tofauti tofauti za mtu kuitaji hela kama wakati wa dharura, kwa ajili ya matumizi ya kila siku, na kwa ajili ya kuwekeza.

Hapo kwenye kuwekeza ndo pana tushinda vijana kwa sababu atupendi kukubali kuwa wanyonge pia kuonekana hatuna hela kwaio tuna pambana na leo yetu tukisahau kesho yetu mfano wakati tuna soma uwa tunaishi maisha mazuri kweli ambayo pindi tu baada ya kumaliza kusoma mambo ubadilika sana kufikia hatua ya kukosa hata hela kufanya mambo madogo madogo kama kununua vocha, kunyoa, kusuka, kununua nguo mpya na mengineyo mpaka hapo tayari tunaona umuhimu wa kuwa na nidhamu ya kuweka akiba na si akiba tu bali tuki lenga hio akiba katika kuwezesha biashara zetu.

Maendeleo yoyote yanaaitaji hela aijalishi una wazo zuri kiasi na la aina gani, kujituma na kujidhatiti katika maswala ya kifedha wakati tukiwa vijana ndo kiwe kipaombele chetu kama vijana hakuna bahati katika kufanikiwa bali ni kuweka malengo na kujitihadi katika kuweka akiba hata hiki tokea fursa unakuwa katika nafasi ya kumchangamkia fursa na sio kubaki kuwa na mawazo ya kua kuna bahati katika kufanikiwa au unaitaji kushikwa mkono hili ufanikiwe kama tunavyo jua mtaji ni hela ambayo inaweza kuzunguka na kuzalisha katika shughuli yoyote hile bila kujali ni biashara gani kwaio kuifadhi hela ni muhimu sana kwa mtu kwa sababu inatoa msaada wakati biashara inataka kuanza.

Kuna namna mbalimbali za kuifadhi fedha mfano kufungua banki akaunti ambazo azi ruhusu kutoa hela mpaka upite muda fulani, kununua hisa za makampuni, pia kama mzunguko wako wa hela upo vizuri unaweza jiunga vicoba ambapo uwa wanavunja kila mwisho wa mwaka au baada ya muda fulani kutokana na makubaliano.

Kupitia hivyo ni rahisi kupata msaada wa kifedha kwa sababu kama vicoba, hisa hela uwa tayari imejiwekeza yenyewe kwa sababu lazima itakua inaongezeka pia kwenye hisa kuna faida unaipata kama kampuni hikifanya vizuri, vijana tujikite zaidi na mambo ya msingi kwa sababu tusipo shutuka saa hivi ni sawa na kupoteza dira yetu mapema sana na kuanza kubaki katika wigo wa kusubiri kuajiriwa na tukifikia hapo jua tuna tengeneza maisha kuwa magumu baada ya kumaliza chuo na ukiangalia kuajiriwa uchukua muda na ni sawa na kusema ni bahati tuna maliza wengi wanao itajika ni wachache “Akiba binafsi ni chachu katika mapambano na harakati za kimaisha kabla na baada ya kumaliza masomo ya vyuo vikuu”.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…