Social credit company ni kampuni ya ukweli au magumashi?

KIATUE

Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
13
Reaction score
0
Nimepita mitandaoni nikapata link iliyonifikisha katika kampuni hii ya social credit compani link ni hii hapa
SOCIAL CREDIT COMPANY
so nauliza hawa watu wanasema wanatoa mikopo ila kuna masuala ya kulipa ada ya tsh 38500/= na mambo kiba katika site yaooo ebu cheki halafu tulijadili hili
 
Hawa ni 419

Msijaze hizo fomu hata kidgo!

Kuna viashiria vingi vinaonyesha kuwa ni matapeli na ama wanataka kuchukua details zako + accnt number ili wanunue vitu online au hiyo ada wanayoitaka, watu mia wakiwatumia....wana hela ndefu!

-fomu haina address, simu wala email au kuonyesha wapi walipo!
-kwanini watumie nembo ya taifa kama logo?
-Katika maelezo yao wameweka address na contacts, lakini number za simu ya meneja (landline) sio za mnazi mmoja, ni location ya posta! Mnazi mmoja (ninavyofahamu ingekuwa +255 22 218.... Location ya fax sio mnazi mmoja wala posta!
-Makosa ni mengi sana katika maelekezo yao n.k, lakini katika hali ya kawaida nani atakupa hela yake bila kukupima uwzo wako wa kulipa!

Hawa ni matapeli wakubwa sana!
 

hmm kweli lakini mbona eatv wametuthibitishia kua hii kampuni ni ya kweli?
 
hmm kweli lakini mbona eatv wametuthibitishia kua hii kampuni ni ya kweli?
Umejuaje kuwa ni account ya EATV, hawa watu ni wajanja sana kuna kipindi walifungua account kwa jina la Zitto kule facebook na kuwahadaa watu, pia wanaweza kuhack account za watu wengine na kupitasha ujumbe wao huo, ni muhimu uwe makini sana, na mambo ya mitandao, mtu anaweza kufungua Account kwa jina lolote au company kwa nia ya kujinufaisha
 
hawa ni matapeli watupu.
Hakuna taasisi ya fedha itakukopesha bila kujua uwezo wako kulipa.
 
ndugu yangu umenena kwani mie nilitaka nijiunge kwa ajili ya mkopo toka kwao asante kwa kuniweka wazi hapa nisingesoma coment ihii ningeingia mkenge
 
du mi nimejaza form yao wakanipigia kwamba wameaprove mkopo wangu wa 5milion nilioomba lakin mpaka nideposit 45000 thousand watanitumia lakin nikaanza kujihoji maana mhhhhh,
 
du mi nimejaza form yao wakanipigia kwamba wameaprove mkopo wangu wa 5milion nilioomba lakin mpaka nideposit 45000 thousand watanitumia lakin nikaanza kujihoji maana mhhhhh,

Vp ulipata huo mkopo?
 
mungu alisema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maharifa.

hivi ni sehemu gani duniani upewe mkopo kirahisi hivo bila kujirizisha kama unaweza kuulipa?
 
KWENYE BLOG HII HAPA NIMEKUTANA NA UJUMBE HUU: PASCAL MZEE WA CHIMBO
INA MAANA NA HUYU MWENYE BLOG NI MWANACHAMA WA HII TAASISI YA KIFEDHA?
RIDHIWANI KIKWETE AMFUNGUKIA MH.MBOWE NA TANZANIA DAIMA YAKE


Nimesikitishwa sana na habari iliyochapishwa na Kaka
Freeman Mbowe wa CHADEMA ambae ndie mmiliki
halali wa gazeti hili. Nimetumiwa Softcopy ya gazeti hili
na kurasa zake na nigazeti la muda kidogo tangu
litoke ila sikubahatika kulisoma nimetumiwa asubuh ya
leo.
Gazeti hili limeniandika ndivyo sivyo kwa madai kua
Taasisi yangu ya Utoaji mikopo SOCIAL CREDIT
COMPANY inatoa mikopo ya kibinafsi kitu ambacho sio
kweli na ninadhani wameandika hivi kwa chuki tu za
kisiasa.
SOCIAL CREDIT COMPANY ni taasisi inayotoa mikopo
bila ubaguzi wowote mwananchi yoyote ambae ni raia
wa Tanzania anaweza kujiunga na SOCIAL CREDIT
COMPANY na akapatiwa mkopo wa pesa wenye
marejesho rahisi yasiyokua na RIBA na hata ukipitia
maelezo ya SOCIAL CREDIT COMPANY katika tovuti
mikopo imewalenga wananchi watanzania ambao ni
masikini sasa hawa CHADEMA wao wamepata wapi
ujasiri wa kuandika vitu hivi bila kua na uhakika wa
jambo?! Kiukweli sijapenda hata kidogo.
SOCIAL CREDIT COMPANY sijaianzisha kwa upendeleo
mtu yoyote anaetaka mkopo anaweza akajiunga na
akapatiwa mkopo, mikopo inatolewa bila upendeleo
kila mtanzania anaruhusiwa kujiunga na kuomba
mkopo katika Taasisi yangu, kujiunga ni rahisi bofya
hapa: http://socialcredit.wapka.mobi soma maelekezo
jaza fomu fanya malipo ya ada za kujiunga na
utapokea mkopo wako ndani ya dakika45 au kama
upo karibu na ofisi za SOCIAL CREDIT COMPANY
zilizopo mnazi mmoja mtaa wa uhuru, jengo namba
360 ghorofa la Tamwa jirani na NBC karibu sana
ujiunge.
Kama uko mbali na ofisi za SOCIAL CREDIT COMPANY
bofya hapa: http://socialcredit.wapka.mobi kila
mtanzania anaruhusiwa kujiunga hakuna ubaguzi
wowote.
 
AHA UZURI PIA MIMI NASOMA MASUALA YA FEDHA NA UHASIBU.NA UTARATIBU WA MTU KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA LAZIMA UWE UMESAJILIWA BOT NANUKUU MANENO YA HIYO WAPSITE YA."SOCIAL CREDIT COMPANY IMESAJILIWA NA TRA
Taasisi / Kampuni ya Social Credit Company sio taasisi ya kienyeji imefuata taratibu zote na kusajiliwa na TRA. Picha hapa chini inaonesha Cheti cha usajili wa Taasisi / Kampuni hii ya SOCIAL CREDIT COMPANY.MAKAMPUNI HAYASAJILIWI NA TRA BALI UNASAJILI TIN NUMBER TRA NA LAZIMA UKUANGALIA ORODHA YA MAKAMPUNI KWENYE WASAJILI WA MAKAMPUNI NA BIASHARA YAANI BRELA,NDIO WATAKUONESHA KWAMBA KWAMBA HIYO KAMPUNI IPO AU LA.MTAATAPELIWA MCHANA NA BOT WALISHATOA TAMKO
 
Pia hata website ya kampuni ni yakitoto haiwezekani shilika likawa na domain ya kugongea kama ile
 
Welcome to Companies Search Page

[TABLE="width: 803"]
[TR]
[TD]Search counter: 00408222
[/TD]
[TD="align: right"]Search Count.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Search by : Company Name Registration Number Date(dd/mm/yyyy)
Company name Does not EXIST in our DATABASE!
 
Jaman hao ni matapeli wanazingua wanaweza sajili Tra na bado wakaiba mim kuna jamaaa wang alitapeliwa na hawa jamiii ya kampuni feki watanzania tupige vita utapeli watu wafanye kazi kihalali na wapate kihalali Ucdanganyikeee
 
Ukweli ni Upi juu ya hawa Jamaa social credit
 

Kutoa mikopo huna haja ya kibali cha BOT kwakuwa unatumia fedha zako mwenyewe.

Ukianza kukusanya pesa ya wananchi hapo ujue BOT inakuja fasta kukuchukulia hatua kali sana!!!!
 
Kutoa mikopo huna haja ya kibali cha BOT kwakuwa unatumia fedha zako mwenyewe.

Ukianza kukusanya pesa ya wananchi hapo ujue BOT inakuja fasta kukuchukulia hatua kali sana!!!!

ni kweli nimekupata nilikuwa niechanganya madawa.ila hawa jamaa bado si kweli
 
Nimesikia Ali Kiba alichukua mkopo kwa hawa jamaa kwa ajili ya kumalizia nyumba yake. Au naye ni mdau anafanya promo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…