Tky
JF-Expert Member
- Oct 1, 2012
- 439
- 140
[h=2][/h]Ikumbukwe wanafunzi wengi walio mwaka wa pili vyuoni walikosa mkopo kutoka bodi ya mikopo (HESLB) na bodi ikaagiza kwamba wakifika vyuoni waombe tena (appeal) kwa shilingi elfu tano na hakuna hata mmoja aliye pewa na wakati bodi ilijua kwamba haina pesa, wanafunzi hao wakafanya kuomba tena mkopo kwa mwaka wa masomo 2012-2013 lakini bodi ikatoa kwa mwaka wa kwanza tu na kuagiza wanafunzi wanao endelea majina yao yatumwe kutoka vyuoni ili kuhakikisha kwamba ni wanafunzi wa kutoka vyuo husika, lakini kwa chuo kikuu cha dodoma imekuwa ndivyo sivyo na chuo hakitoi mchango wowote kuwasidia wanafunzi hao ili kufikisha majina yao LOAN BOARD kwa uhakiki kama vyuo vingine mfano UDSM, SAUTI, ARDHI n.k, walivyofanya na hatimaye wakapewa mkopo. SERIKALI TUNAOMBA ILITAMBUE JAMBO HILI KWANI WANAOUMIA NI WANAFUNZI NA SIO CHUO.