justin mwanshinga
Senior Member
- May 22, 2014
- 179
- 621
Kabla ya wakati wetu wa kawaida, Mwaka 399BC Socrates Mgiriki alihukumiwa kunywa kikombe cha sumu aina ya Hemlock kwa kosa la kuwafundisha vijana uasi dhidi ya dini na serikali.
Kimsingi hukumu ya kesi hii ilikuwa si ya haki kwani uasi ambao Socrates aliwafundisha vijana wakiwemo wakina Plato, Xenophon na wengine wengi ulikuwa si uasi bali ilikuwa ni elimu ya kujitambua kwa vijana juu ya mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye viunga vya mji wa Anthes huko Ugiriki.
Kati ya mambo aliyowafundisha yaliyoonekana ni uasi ni falsafa (mchezo wa kufikiri na kuhoji) hivyo Socrates aliwafundisha vijana kufikiri na kuhoji ili kupata uhalisia wa kila jambo badala ya kubweteka na kupata uharo wa kila jambo.
Ikumbukwe kuwa uko Anthes miaka ile watu walikuwa wanaabudu sanamu hivyo wakitaka mvua walienda kuziomba sanamu walizozichonga, wakitaka kupona walikwenda kuziomba sanamu, hapa ndipo uasi wa vijana ulipojitokeza.
Vijana wa Socrates walianza kuhoji kila kitu moja wapo ni hilo la kuabudu sanamu kama Mungu wao, katika hili walihoji "Inawezekanaje na kwa vipi kitu ulichokitengeneza kwa mikono yako ukakiita Mungu?''
Hivyo kwa hoja hiyo wazee wa sheria potofu kwao waliamini ulikuwa uasi mkubwa na hatima yake ilikuwa kushitakiwa kwenye mahakama ya umma.
Alikamatwa akawekwa gerezani, Akiwa gerezani rafiki yake Mkubwa aitwaye Crito mtu tajiri huyu alimshawishi Socrates atoroke kwani alikuwa na uwezo wakuwahonga walinzi wa gereza, katika hili Socrates alijibu;
1. Kukimbia itakuwa ni ishara ya kuogopa kifo, jambo ambalo wanafalsafa hawapaswi kuogopa.
2. Ikiwa nitakimbia, mafufundisho yangu hayatakuwa na maana kwenye nchi zingine.
3. Nimeishi chini ya sheria za mji, Mimi mwenyewe nimezifanyia uhalifu, kukimbia nitakuwa navunja taratibu za jamii na za nchi.
4. Ikiwa nitakimbia kwa msaada wa marafiki,marafiki zangu mtawajibika kwenye sheria za nchi (mtanunua kesi).
Akiwa gerezani alimuona mbebaji wa kikombe cha sumu ambayo alipaswa kunywa, cha ajabu badala ya kunung'unika yeye kwa furaha alimwambia ''wewe ni mtu mwema kwangu hivyo utanifundisha taratibu zote za kunywa"
Socrates hakuhofia kifo kwani aliamini kifo ni tiba inayotoa Uhuru wa nafsi toka kwenye utumwa wa mwili (mwili ni gereza na nafsi ni mfungwa) lakini vile vile hakuwa na hakika kipi bora kati ya maisha na kifo alishuku pengine kwa kuendelea kuishi ndivyo binadamu tunavyojinyima raha iliyopo katika kifo.
Baada ya kupata maelezo alijichukulia Kikombe akaigugumia sumu pasi kuitua mpaka alipojihakikishia sumu imekwisha kabisa.
Maneno ya mwisho ya Socrates alimwambia rafiki yake "Crito kumbuka kulipa deni''.
Deni hilo kwa rafiki yake ni kuwa na msimamo kwa kile unachokipigania, kwa kile unachoamini kiasi kwamba uwe tayari kwa lolote hata kwa kufungwa ama kuuawa muhimu kiwe na faida kwako na kwa kizazi pamoja na jamii yako.
Yamkini Socrate aliamini dunia haitufunzi lolote isipokuwa kutukumbusha jitihada za kujaribu kuwa wema, yaani kuwa wadaiwa / wadeni wakimatendo (Deni ni matendo ya wema).
Miaka michache baadae nae Yesu pasi lawama yoyote naye alijibebea msalaba mpaka Golgotha tayari kukabili kisichomstahili.
Hivyo basi Asili ya ulimwengu ni kuwataabisha waliowema.
Mwagona